SONGWE: Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mlowo ajinyonga baada ya kutapeliwa Tsh milioni 118

Protector

JF-Expert Member
May 20, 2019
414
877
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mlowo Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, Meshack Mwambogolo amekutwa amejinyonga katika msitu uliopo kitongoji cha Iyenga Kijiji cha Shaji Kata ya Mlangali baada ya Rafiki yake aitwaye Joseph Muhume ambaye wanafanya nae biashara pamoja kutoroka na Tsh. Milioni 118.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amesema mwili wake umekutwa ukiwa umening'inia kwenye mti leo Aprili 24, 2023 asubuhi ambapo alijinyonga kwa kamba ya manila huku akiacha ujumbe kuwa Familia yake imsamehe kwa maamuzi aliyofanya.

Kamanda amesema jana Mwambogolo alitoa Tsh. Milioni 118 na kuziweka kwenye akaunti ya Joseph Muhume kwa ajili ya kununulia kahawa ambapo baada ya kumuingiza fedha hizo Joseph alitoroka.

“Baada ya Mwambogolo kupewa taarifa kuwa Joseph ametoroka alichukua kamba na chupa ya sumu ya kuulia wadudu na kutoweka ndipo mwili wake ulikutwa asubuhi ukiwa unaning'inia kwenye mti huku akiwa ameacha ujumbe ambao unaiomba Familia yake imsamehe kwa uamuzi alioufanya wa kujinyonga”

Katibu wa CCM mkoa wa Songwe, Juma Mpeli amesema wamepata taarifa hiyo ambayo imewasikitisha huku taratibu nyingine zikiwemo za kipolisi zikiendelea.
 
Mil 118 nimuwekee mtu kwenye account uchawi upo.
Wew hata buku la karbu hutakag KuliToa

Ila na yeye alitoa kwa zote kwa pamoja asee
FB_IMG_1641357181145.jpg
 
Mil 118 nimuwekee mtu kwenye account 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 uchawi upo.
niliwahi pewa m278 nikalipe wakulima wa pamba, nikaombwa nichukue ulinzi wa polisi nikawaza hawa hawana(ga) akili wataniua na mzigo wabebe

nilifanikisha walipa nikapendekeza malipo kupitia akaunti jamaa yaligoma hadi leo sijui wanalipanaje kama bado ni cash ama kwenye akaunti
 
Wafanyabiashara wote wa mazao nk wanatumia middle men wanawapa pesa za kutosha then wanamsubiria mzigo..

Huyo bwana amestuka hasa Kwa kupigwa na mtu aliyemuamini so hakutegemea
 
niliwahi pewa m278 nikalipe wakulima wa pamba, nikaombwa nichukue ulinzi wa polisi nikawaza hawa hawana(ga) akili wataniua na mzigo wabebe

nilifanikisha walipa nikapendekeza malipo kupitia akaunti jamaa yaligoma hadi leo sijui wanalipanaje kama bado ni cash ama kwenye akaunti
Mambo ni cash tu, ukiweka kwenye account utalipa na yakutolea
 
Back
Top Bottom