Eng. Zezudu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 7,814
- 10,834
Siku ya jana daladala ziligoma hapa Mbeya na baadhi ya makonda na madereva wakileta vurugu kwa baadhi ya magari yaliotaka kubeba abiria na sababu ni kwamba hawataki bajaji zipite njia kuu. Hii ni dalili tosha kwamba Waafrika ni wabinafsi na hatupendi maendeleo ya wenzetu, bajaji zimetoa ajira kwa vijana wengi hapa mjini na zinanamba za biashara na kutambulika. Kuwanyima kupita njia kuu ni dalili tosha kwamba daladala hawajui nini maana ya biashara huria na wamekosa ubunifu, wanakaa standi mda mrefu na kutuboa wasafiri.