Mbeya: Mgomo wa daladala Mbalizi -Sokomatola na Mbalizi- Mwanjelwa

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
7,813
10,828
Siku ya jana daladala ziligoma hapa Mbeya na baadhi ya makonda na madereva wakileta vurugu kwa baadhi ya magari yaliotaka kubeba abiria na sababu ni kwamba hawataki bajaji zipite njia kuu. Hii ni dalili tosha kwamba Waafrika ni wabinafsi na hatupendi maendeleo ya wenzetu, bajaji zimetoa ajira kwa vijana wengi hapa mjini na zinanamba za biashara na kutambulika. Kuwanyima kupita njia kuu ni dalili tosha kwamba daladala hawajui nini maana ya biashara huria na wamekosa ubunifu, wanakaa standi mda mrefu na kutuboa wasafiri.
 
Wehu kweli hao,kwani wenye bajaj nao si wanawahudumia wananchi hao hao??

Kama vp wauze mikweche yao nao wanunue biashara,kwa sasa huwezi kuuzuia upepo wa bajaj,ndio usafiri wa haraka zaidi na wa bei nafuu
 
Washindani wa bajaji ni wagomvi sana huku boda boda nao hawawataki watu wa bajaji wapaki maeneo walipo wao fikra mbovu kabisa za kibiashara kama usalama upo wapige kazi tuu...mnagoma kwa sababu ya ushindani ila sishangai ndio uzao huo wengine walitimua coaster baadhi ya njia Dar ili mwendokasi isiwe na mpinzani kule nako Bombardier zilipofika fast jet ilitafuta Nchi ya kwenda ....
 
Back
Top Bottom