MBEYA: Kanisa kutoa orodha ya wauza unga


Hii habari naiona imekaa kimagamba magamba..ikiazimia kumletea ahueni raisi..OK ngoja awataje tuone..ila cha ajabu kama kweli Rais alipewa listi hiyo tangu 2006...amefanya nini?? TZ eeehh x2....
 
Duh!!??nimefuatilia kastori katamu haka.na hadithi ya jk ikaishia hapo.
 

Mimi sikuwa nikifahamu kuwa hicho kifupisho cha TEC kinatumika pia kisheria na dhehebu jingine lililojisajili Tanzania zaidi ya Tanzania Episcopal Conference (TEC) yaani Baraza la Maaskofu wa katoliki Tanzania. Yaelekea habari nzima inalenga kuwagombanisha wakristu na serikali na nadhani hiii imefanywa kwa makusudi ili ku Divert attention.

Pamoja na kwamba mimi si CCM wala siupendi uongozi wa JK bado sioni tatizo kwa yeye kutamka kwamba baadhi ya viongozi wa dini wanajihusisha na madawa ya kulevya. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Wafadhili wa madawa ya kulevya katika jamii yetu wapo katika kila nyanja; wapo wafanyabiashara, wachungaji, Maaskofu wa madhehebu yanayoota kama uyoga na ambao hawana wa kuwadhibiti, masheikh, maaskari, mawaziri, wanamichezo, madereva mpaka wasukuma mikokoteni.

Sasa kuna ubaya gani kwa mtu aliyepewa dhamana ya kuangalia usalama kupiga kelele kwamba kuna watu wachche wabaya miongoni mwetu? Jukumu la kujiangalia walivyosimama katika safu zao kwamba ni nani anayewatia dosari viongozi wa madhehebu ni lao na si serikali.

Kwa hiyo Masheikh, Maaskofu, Wachungaji, Maimamu na viongozi woote wa kiroho watusaidie, wajisafishe kwa kuwataja hadharani wanaoichafua safu yao ili kuiokoa nchi hii yetu sote.
 
atuna aja na kanisa lake sisi majina 2 ya ao watu
 
Mtamsaidiaje huyo mjinga hana maamzi hata siku moja ya ni mwanamke kwa lugha nyingine uanaume wake nipale anapokuwa amevaa nguo za kiume mimi sioni haja ya kulumbana au kutaja maana kila kitu anajua kama majina anayo anataka msaada wa nini?
 
Kesho mimi natoa orodha yangu.........Wamo mawaziri,makatibu wakuu,mabalozi,masheikh,wabunge,wafanyabiashara wakubwa, stay tune
 
mmmh tutasikia mengi..na nyie viongozi wa dini hebu fanyeni kazi ya mungu huko na mzidi kuwaombea kondoo wenu sio madawa madawa :shut-mouth:
Hpana sister,waache waendelee na harakati hizo,kwa kuwa kauli ya rais ina utata mkubwa sana!!
 
Aangalie wasijewaka mchifupa kabla hajawataja
 

Ndugu yangu,
Ninaona kama serikali na kikwete wake wamejitisha mzinga wa nyuki kichani ndani yake kukiwa na kila aina. Tusubiri huo mzinga udondoke kama utakuwa salama.
 
Waangalie wasije wakapoteza maisha yao, biashara ya madawa ya kulevya inahusisha watu hatari na wenye nguvu kwenye serikali. Hawa pia ni wachangiaji wakubwa kwenye vyama tawala vya nchi wanayofanyia kazi, wana watu wao kwenye vyombo vya usalama, serikalini na mahakamani....

Hata hivyo tunamtakia kila la heri Mtumishi wa Mungu na wenzeka ili walisaidie taifa kupambana na aibu hii!
 
Mbona inasemekana huyu mchungaji wa Mbeya hana kanisa wala nini ni mwanaharakati tu kama Mtikila. Tena ni kihere here kinachojipendekeza kwa dola. Na ni huyu aliyeitoa hiyi listi mnayodai Jk kukabidhiwa tangu 2006 na akausugua.
Rais yeye katika ile hutuba yake ya tareha 02 asingelaumiwa na kupewa saa za kwataja wauza unga kama engesema, 'baazi wa viongozi wa dini wanajihusisha na dawa za kulevya' tatizo lake lilikuwa ni ku- generalise kwa kusema 'viongozi wa dini wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya' maana yake ni kwamba wote ni wauza unga. Hivyo ni busara raisi kuirejelea ile hutuba yake ilii kubaini kosa lake. Ni uchaguzi wake kuomba radhi ama kukaa kimya na kuendelea na zoezi lake la kupropagate kwa kuwavuta viongozi wa dini kwenye mchezoo wa propaganda za siasa.
.
 
Kuna taarifa zozote za kutanjwa hao wauza unga mpaka sasa?
 
Kwa kweli katika hili kanisa inabidi kujidhatiti sana maana laweza kutaja hata wateule wa mzee wa kaya hivyo bidhaa zao zaweza anza kutozwa ushuru.Pia utajikuta hao wachungajin baadhi wakawa ndo wahusika wakuu.
 
Aangalie wasijewaka mchifupa kabla hajawataja
Waki mchifupa tutataka zaidi kikwete awataje! Si alishapewa orodha? Hapa anasaidiwa, wanaomsaidia wakichifupwa yeye ataisaidia polisi, maana wauaji lazima wawe toka hiyo orodha! Lakini subiri kidogo! Hivi kumbe Bongo hatuna polisi.. Mwena ni mkuu wa kitengo cha usalama cha ccm...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…