Mbeya: Joseph Mbilinyi(Sugu) akamatwa na Polisi kwa uchochezi, apewa dhamana

!
!
Vitambulisho Vya Bodaboda Vipo Jikoni..... Vitafiatiwa Na Vya Watembea Kwa Miguu. Mapaka Tutembee Na Mabegi Ya Vitambulisho.
Kurudi Kwa Kodi Ya Kichwa.
 
Tatizo ni vitambulisho vya kitapeli vya 20,000? Hawa polisi wanaogopa nimi mwakilishi kusikiliza kero hii mpya ya vitambulisho visivyo na utambulisho?
 
I know , but you must understand that from Mbeya to Katavi was Demotion , Kwa mtu wa mjini kama pedesheee Makalla kumtupa Katavi ( njia panda ya kuzimu ) ilikuwa ni kama adhabu
Demotion kama angekuwa mkuu wa wilaya lakini amebaki na cheo chake kile kile,kweli utasema demotion mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

KAULI YA KULAANI MBUNGE SUGU KUSHIKILIWA, KUNYIMWA DHAMANA KWA KUTIMIZA MAJUKUMU YAKE*


Leo Alhamis, Februari 21, 2019, saa moja asubuhi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu', aliitikia wito wa Jeshi la Polisi, aliopewa jana kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Mbeya na Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai (RCO), wote kwa nyakati tofauti, wakimtaka kufika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa ajili ya mahojiano.

Hadi jioni hii, tunapolazimika kutoa taarifa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limeendelea kumshikilia chini ya ulinzi Mbunge huyo na baada ya kwenda naye eneo la Ikuti jijini humo, ambapo inadaiwa alitoa maneno ya uchochezi siku ya Jumamosi, Februari 16, mwaka huu alipokuwa akijibu malalamiko ya kero mbalimbali za wananchi wa jimboni kwake, polisi wamemrejesha Mbunge Mbilinyi Kituo Kikuu cha Polisi na amenyimwa dhamana bila kuwepo kwa taarifa yoyote ya kunyimwa haki yake hiyo ya msingi kwa mujibu wa sheria za nchi.

Chadema kinalaanii vikali kitendo cha Mbunge kushikiliwa, kuhojiwa na sasa kunyimwa dhamana kwa kuwaahidi wananchi wake kuwa atakwenda kuhoji bungeni suala la Wamachinga kuuziwa vitambulisho, ambao ni wajibu wake akiwa mwakilishi wa wananchi.

Chama kinafuatilia jambo hili kwa ukaribu kupitia kwa wanasheria wa wake, kikilitaka Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kumfikisha Mbunge huyo mahakamani haraka iwezekanavyo kwa mujibu wa taratibu za nchi ili apate haki yake ya dhamana.

Kwa taarifa tulizonazo, mahojiano aliyofanyiwa yalijikita kutaka kujua tafsiri ya maneno aliyoyatumia Mbunge huyo siku hiyo ya Februari 16, ambapo akisikiliza malalamiko ya wapiga kura wake, baada ya kutoa msaada wa saruji, nondo na mabati, katika Shule ya Ikuti, aliwaahidi wananchi kuwa atakwenda kuhoji bungeni suala la vitambulisho wanavyouziwa 'Wamachinga' kwa bei ya shilingi 20,000/= ili kujua msingi wake na kwanini limeanza kufanyiwa kazi bila kuwashirikisha wadau ili kuwa na uelewa wa pamoja.

Mbunge Mbilinyi alitoa majibu hayo baada ya wananchi hao, hususan wafanyabiashara ndogondogo wanaojihusisha na uuzaji wa mboga kumlalamikia usumbufu wanaoupata kwa kulazimishwa na mamlala za kiserikali mkoani humo kununua vitambulisho vya wafanyabiashara ndogondogo kwa bei hiyo wasiyoweza kumudu kutokana na udogo wa mitaji, biashara yao na hata mapato wanayopata. Walihoji mantiki iliyotumika kuwapangia wauza mboga wanunue vitambulisho hivyo kwa bei hiyo moja, sawasawa na wafanyabiashara ndogondogo wengine wenye mitaji mikubwa kwa kuwalinganisha na wauza mbogamboga.

Imetolewa leo Alhamis, Februari 21, 2019 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

========

UPDATES:

Mbunge Joseph Mbilinyi (Sugu)CHADEMA, Muda wa saa 01: 03 PM, Amepewa dhamana kwa masharti ya kudhaminiwa na mtu mmoja ambaye amesaini bond ya shilingi Milioni 5 na atatakiwa kufika polisi kesho saa nne Kamili asubuhi.

A STUPID AND PRIMITIVE DICTATOR AT WORK.SHAME UPON YOU.
 

Ningekuwa mzee Mkuchika ningemfuata rais niongee nae kwa upole kabisa nimuombe ateue waziri mwingine wa utawala bora mimi nimechoka nataka kupumzika.

Huwezi kuwa waziri wa utawala bora awamu hii, ni kujitakia tu kujitengenezea historia mbaya.

Awamu ambayo kila mtu anataka kujimwambafy ni ngumu zana kuwa na utawala bora.
 
Back
Top Bottom