Mbeya: Jeshi la Polisi lapiga marufuku maandamano ya Mdude na Mwabukusi, yasema yanalenga kuhatarisha usalama

In short unapambania vitu vya kijinga! Ulitegemea polisi waruhusu maandamano ya kipumbavu hivyo? Tafuta kazi ya kufanya!
 
Ndugu zangu majira ya asubuhi leo 3rd November 2023 tukiwa katika mkutano wetu na waandishi wa habari tulivamiwa na kukamatwa na askari kadhaa wakiongozwa na Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi kutoka ofisi ya RPC Mbeya. Askari hao walitukamata sisi pamoja na waandishi wa habari tuliokuwa nao katika press conference.

Masaa matano baada ya kushikiliwa tuliitwa ofisi kwa RPC kwamba tulikamatwa ili tupewe barua ya inayotuzuia kuandamana kwa amani tarehe 9 Nov 2023.

RPC alidai kuwa OCD hajui tunapopatikana ili atuletee barua ya majibu ya maandamano hayo hivyo ikalazimika tukamatwe ili tupewe barua ijapo OCD huyo alikuwepo wakati wa ukamataji wetu.

Kwa sasa tupo tunaandaa barua ya rufaa kwenda kwa waziri wa mambo ya ndani kupinga zuio haram la OCD na baada ya hapo tutatoa tamko rasmi.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

View attachment 2802412

Polisi gani? Hawa waliiba milioni 90?. Polisi hawana ubavu wa kuzuia maanadamano ya Wananchi.
 
Kwa hivyo?



Unaandaa barua kwenda kwa Waziri. Hii ni sawa unamwambia Hamas aende kwa Biden akaombe chakula.
Dahhhh?

Unaelewa maana ya taratibu?. Wanafuata taratibu ili policcm wasije kupata sababu za kijinga. Halafu maanadamano ni ya amani.
 
Taratibu ni kwenda mahakamani, sio barua kwa waziri, jkifika kwa waziri hiyo barua ataichoma moto halafu ajikalie kimya.

Ndio taratibu zenyewe hizo. Mahakamani huendi kila wakati, Kuna principle ya exhausion of Local remedies, lazima uhakikishe umemaliza ngazi zote za Chini ndio uende mahakamani Kama last resort. Sio unaenda mahakamani unapigwa Chini kisa hukufile appeal kwa Waziri.
 
Hizi nguvu mnazo zitumia kufanya harakati na mpaka Leo sijajua ni nini mnacho kipambania......

At least 😇 mngekua mnaelekeza hizi nguvu kumobilise vijana kujikomboa ki uchumi na maendeleo ki ujumla....

R.i.p Alphonce mawazo pumzika Kwa amani brother

Punguza lawama na unafiki. Kuanzia kata yupo afisa maendeleo, afisa baishara mpaka mkoani. Hao hawajatosha mpaka uwageukie wanasiasa Tena wa upinzani?. Mmejaza wabunge wa CCM na madiwani wa CCM lakini kutwa lawama kwa wapinzani.
 
Tuondoshee ujinga wa maandamano.

Hizo pesa unazochangiwa ungeanzisha miradi vijana wapate kazi za kufanya.

Wewe kwanini usianzishe hiyo miradi na izee wako?. Punguza unafiki. Unamwambia mtu afanye kitu ambacho wewe hujawahi kukifanya?.
 
Back
Top Bottom