Mbeya City Football Club - Special Thread!

Mkuu unakimbia mapema hewani,uwe unabakibaki kidogo,hapo sawa,kazeni bwana hata mkitolewa nusu c mbaya wasije wakasema ni nguvu ya home tu.
 
Tunashukuru kwa maombi yenu yaliyoiwezesha mbeya city kutinga robo fainali ya cecafa nile basin cup matokeo ya leo. Mbeya city 0 Enticelles 0 matokeo haya yanaipeleka mbeya city katika hatua ya robo fainal

viva mbeya city tumechoka na simba na yanga..... Piga mbombo wazee
 
Ndugu kesho 30 April 14 ni robo fainali kati ya mbeya city - Tanzania na victoria - Uganda. Huko Khartoum Sudan.
 
30 May 2014
Khartoum, Sudan

Michuano ya Nile Basin nchini Sudan, ngwe ya mtoano Robo Fainali leo 30 Mei 2014:

Host side El Merreikh will host Burundi's Academie Tchite, Ugandan club Victoria University will square off against Tanzania's Mbeya City, while another host team Al Ahli Shandi will tackle South Sudan's Malaika. Kenya's AFC Leopards against Ethiopia's Defence.

Source: Nile Basin Cup organizers CECAFA Nile Basin Cup Round up Results: Victoria (1)VSMalakia(0),Al-Merreikh(3)VS Police (0),Al-Shandi(2)VSDkhill(1), Mbeya City (3)VSAcademie(2),AFC Leopards (2)VSEtincelles(0)
 
MICHUANO YA MTO NILE: Mbeya City(TZ) O-1 Victoria(UG) Kwa matokeo haya Mbeya City wameyaaga mashindano kwenye hatua ya Robo fainali. Mbeya City wamecheza michezo 4;
-Wameshinda mchezo 1.
-Wametoka Sare mchezo 1.
-Wamefungwa michezo 2.
 
Tumewasili salama Dar tukitokea khatoum Sudan sasa ni safari ya kuelekea Mbeya.

sosi. Mcc fan page
 
Tumewasili salama Dar tukitokea khatoum Sudan sasa ni safari ya kuelekea Mbeya.

sosi. Mcc fan page
We ndetichia kila team inayoibuka wewe unashabikia tu, Mara Azam mara Manchester city na sasa hivi Mbeya city Sitashangaa siku nikikuta Stand United special thread ya mjini Shinyanga...
 
Last edited by a moderator:
....Kampuni ya Binslum Tyres Co. Ltd ....chini ya Mkurugenzi wake, Nassor Binslum .....imeingia mkataba wa miaka miwili wa shilingi 360 milioni na klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya....Katika mwaka wa kwanza, Mbeya City itapokea kiasi cha shilingi 180 milioni, na mwaka wa pili itapokea kiasi kama hicho....watavaa jezi yenye nembo ya RB ikiwa ni mabetri maarufu ya kampuni hiyo.

hongera sana binslum kwa moyo huo..
 
PRESS REALESE NO.03

MCHAKATO WA USAJILI 2014/2015. Kikao cha bodi kilichoketi tarehe 19/6/2014 kiliazimia kuwa klabu imefunga rasmi zoezi la usajili kwa msimu ujao wa 2014/2015. Hii ni kutokana na klabu kuwa na mipango ya kupunguza kikosi ili kuwa na kikosi kidogo na chenye ufanisi(tija) na kwa kuzingatia klabu kwa msimu uliomalizika na msimu ujao kutokuuza wachezaji wake. Baadhi ya wachezaji watapandishwa toka katika kikosi cha pili na wachezaji wawili wapya waliojiunga na timu kwa ajili ya msimu ujao 2014/2015 wanatosha. Mchakato unaoendelea toka tarehe 25/6/2014 ni kutafuta wachezaji kwa ajili ya kikosi cha pili (Juniour team) A na A2, mchakato huu utamalizika tarehe 2/7/2014.

Lengo ni kupata wachezaji wenye umri kati ya miaka 17-21. Wachezaji ambao muda wao wa kuendelea kuitumikia klabu umefikia tamati ni hawa wafuatao: Aziz Sibo(mkataba umekwisha muda wake 31/5/2014), Mohamed Suleiman(Kapangiwa majukumu mengine), Baraka Haule, Francis Casto, Jeremiah John Mangasini, Richard Brown, Yusuph Wilson(kutolewakwa mkopo), Geofrey Jackson(kutolewa kwa Mkopo). Watumishi ambao mikataba yao imekwisha muda wake na kwa sababu mbalimbali zinazojulikana kwa pande zote mbili imeshindikana kuihuisha ni Fredy Jackson aliyekuwa Afisa Habari(mkataba wake umekwisha tarehe 31/05/2014) na aliyekuwa Kocha msaidizi Maka Mwalwisi (Mkataba wake umeisha tarehe 30/06/2014).
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
29.06.2014
 
Club friendly match
13 - 09 - 2014
Dakika 90 zimekamilika Vipers Fc imeshinda 4-1 mcc fc

fanpage.
 
Back
Top Bottom