Mbeya : Chadema yadai Tamaa ya viongozi wa Halmashauri ya Mbeya Mjini imechangia timu ya Mbeya City kuboronga

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,768
218,389
Akizungumza mbele ya Maelfu ya Wananchi wa Kata ya Igawilo , Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini John Mwambigija , Amedai kwamba , Kufanya vibaya kwa timu ya soka ya Mbeya City kumechangiwa na tamaa ya viongozi wa Halmashauri hiyo ya kutafuna posho za wachezaji kwa lengo la kujigharamia wao kwenye safari zote za Timu hiyo.

Huku akishangiliwa na wananchi hao , Mwambigija anadai kwamba kuna kundi kubwa la madiwani na viongozi wa Halmashauri wanaoambata na timu hiyo kila inapokwenda kama sehemu ya kula bata , huku wakiambatana na mahawara zao , amesema timu inashuka daraja kwa sababu viongozi waliopaswa kuihudumia wameamua kutumbua hela za Timu .

Mwambigija amempongeza Mbunge wa zamani wa jimbo hilo Joseph Mbilinyi kwa kujitolea kununua kila goli ambalo Mbeya city watashinda kwa Tshs mil 1

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Kutumia pesa za jiji kuendesha timu ni matumizi mabaya ya pesa. Timu iuzwe na pesa zitumike kwenye shughuli za maendeleo ya jiji, timu zote za jiji. Labda watuletee hesabu zikionyesha majiji yanaingiza pesa nyingi kupitia timu hizo kuliko wanazotoa.
 
Back
Top Bottom