Mbeya: Atuhumiwa kumuua baba yake kwa kumpiga na ubao

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia kijana aitwaye HUMPHREY FRANCIS KIHALI [25] Mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya baba yake mzazi aitwaye FRANCIS JOHN KIHALI [50] Mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya.

Awali Septemba 10, 2023 majira ya saa 10:45 jioni huko eneo la Ilemi mtuhumiwa alimvizia baba yake mzazi FRANCIS JOHN KIHALI akiwa chumbani kwake na kisha kumpiga kwa kutumia ubao ambapo alikimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na kufariki dunia leo Septemba 11, 2023 majira ya saa 1:30 asubuhi.

Pamoja na uchunguzi wa awali kubainisha kuwa mtuhumiwa ana tatizo la akili, uchunguzi unakamilishwa ili hatua zingine za kisheria zifuate.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wazazi na walezi ambao wana changamoto ya watoto wenye matatizo ya Afya ya Akili kuchukua tahadhari kwa kuweka uangalizi madhubuti na kufuata maelekezo ya utumiaji wa dawa wanazopewa ili kuzuia madhara makubwa kama haya yasitokee.
 
Ingekuwa moro au chuga ningesema mibangi ila uko nyanda za juu kusini huwa mnaloga sana watoto wenu ili mtajirike saa kuna kipindi fyuzi zunakaa sawa saa dogo ameona ngoja saa tumalizane mzee
 
Back
Top Bottom