Mbeya: Aliyeoa Yatima Mlemavu Gumzo, Wanavyoishi Utashangaa

Wakati nasoma hii habari hadi nilipoimaliza nilipata hamasa sana, lakini nimevunjwa moyo kwa maoni ya wachangiaji walio wengi!

Watu wamekosa ustaarabu na utu kwa kiwango cha kutisha, nimesikitika sana.

Yeyote uliyechangia kwa maneno ya kejeli ktk thread hii... imagine Salome ni ndugu yako na Mungu kamjaalia mwanaume tena kijana mzuri tu wa kumpenda pasi na kujali hali yake, ungesema sawasawa na ulichokisema hapa? Kwanini mmekuwa wanyama kiasi hiki?
Kwanini mnajisahaulisha Mungu wetu ni huyuhuyu mmoja aliyempa Salome ulemavu na sisi utimilifu?
Hiki kiburi na majivuno kinatoka wapi ilhali hakuna aliye na uhakika wa kesho yake ikoje?

Mimi nimewapenda, nimefurahi zaidi kuona wapo wanaume wenye maoni chanya juu ya ulemavu. Timotheo anaweza kuwa na elimu ndogo kuliko wanaume wengi waliochangia hapa lakini ameonesha uelewa mkubwa sana.

Mungu awasaidie kutatua tatizo lao la kipato pamoja na kudumisha upendo baina yao, kwa maana huu ndio upendo wa kweli.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Ni kweli hata mimi nimeshangaa sanaa..ni sawa na kumcheka mgonjwa wa ukimwi au wa malaria,hakuna anaeijua kesho unaweza kupata ajali ukawa mlemavu zaidi hata ya huyo dada.
 
MLEMAVU-3.jpg


WAKATI wanandoa wasiyokuwa na ulemavu hata wa kidole gumba wakiishi maisha ya kutwangana makonde na kununiana, hali ni tofauti kwa kijana Timotheo Mwazembe aliyeoa mlemavu.



Maisha ya ndoa ya Timotheo (29), mkazi wa Ilemi jijini Mbeya aliyemuoa Salome Msomba (30) ambaye ni mlemavu yamekuwa gumzo kwa jinsi kijana huyo anavyompenda na kumheshimu mkewe.



Taarifa za wengi kushangazwa na ndoa hiyo zilipozidi kusambaa, Risasi Jumamosi likaona ni vyema kuitembelea familia hiyo iliyobahatika kupata mtoto wa kiume hivi karibuni ili kujua mawili matatu kuhusu maisha yao.





Akizungumza na Risasi Jumamosi, Timotheo alisema anajisikia fahari kuishi na mkewe ambaye ni mlemavu licha ya kupata vikwazo vingi kutoka kwa ndugu zake.

MLEMAVU-5.jpg


“Mimi na Salome tulikutana katika Kijiji cha Nanyala Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe nilipokuwa nafanya biashara ya kuuza mayai.

“Mtu ambaye nilikuwa namtegemea kunikusanyia mayai ni Salome, ndipo tukaanza urafiki mpaka hivi tumekuwa mume na mke,” alisema Timotheo.



Siku zote mapenzi ni mafuriko, huwezi kuyazuia kwa mikono; ndivyo ilivyokuwa kwa kijana huyo ambaye aliamua kuziba masikio asisikie kelele za ndugu na marafiki zake waliokuwa wakimuwekea pingamizi la kumuoa Salome kwa sababu ya ulemavu wake.



“Mwanzo tulikuwa tukiona kama Timotheo siyo wa kawaida lakini kwa jinsi wanavyoishi maisha ya furaha na kupendana wanatupa funzo kubwa katika maisha ya ndoa.

“Mimi nawaombea mema sana kwa Mungu, azidi kuwabariki na kuyafanya mepesi maisha yao,” alisema Samson kijana aliyejitambulisha kuwa ni rafiki wa Timotheo.

MLEMAVU-7.jpg


Kwa upande wake Salome akielezea historia fupi ya maisha yake alisema alipata elimu ya msingi, Katumba Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.

“Wakati nasubiri matokeo nilifiwa na wazazi wangu wote na kubaki yatima.

“Baada ya hapo alinichukua mama mdogo aliyekuwa akiishi eneo la Igurusi ambako nilifaulu kwenda kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Jangwani Mkoa wa Dar es Salaam,” alisema Salome.



Aliongeza kuwa kutokana na mama yake mdogo kukosa fedha za kumsomesha alishindwa kuendelea na masomo.

Aidha alidai kuwa mama yake huyo alimshauri kurudia darasa la sita jambo ambalo hakulikubali hivyo kutakiwa na mama yake kuondoka na kwenda kuishi Itumba Ileje Mkoa wa Songwe.

Akiendelea na maisha Itumba, Salome anadai alitengwa na ndugu kwa madai kuwa amekataa kusoma na hivyo kuonekana kama mzigo wa familia.

MLEMAVU-2.jpg


“Maisha ya machungu yalipita, Mungu akanipatia Timotheo ambaye kusema kweli tunapendana na mtoto wetu tumempa jina la Emmanuel, hadi sasa ana miezi mitatu,” alisema Salome.

Kuhusu kukabiliana na changamoto za maisha, Salome alisema amekuwa akijishughulisha na uuzaji wa mkaa huku mumewe akifanya shughuli za udobi.

Pamoja na kuwepo kwa maisha ya furaha katika maisha yao, mwandishi wetu alishuhudia baadhi ya changamoto ambazo wanandoa hao wanakabiliana nazo.



Mfano katika kipindi hiki Timotheo amekuwa mstari wa mbele kusaidia malezi ya mtoto na kukosa muda wa kwenda kutafuta mahitaji ya familia.

Aidha, ukosefu wa baiskeli ya wenye ulemavu nayo ni tatizo ambalo linamlazimu Timotheo anapotaka kuongozana na mkewe kumpakiza kwenye baiskeli ya kawaida huku akiwa amembeba mtoto mgongoni.

Kutokana na changamoto hizo gazeti linawaomba wasamaria wema kujitokeza kuisaidia familia hiyo kwa hali na mali ili izidi kuwa na furaha na kujijenga zaidi kimaisha.
Hawa kweli wanahitaji msaada
 
Try to reason out properly..... mtu mweusi bado ni mtu mshenzi tu
.. hata kwa karne hii.....narudia tena iko kitu hapo!!!...hiyo njemba haiwezi kutudanganya eti ima fall in love....that will be a joke of the century take it to your wallet...

Kama kuna namna au anamtumia mke wake ambaye ni mlemavu huku anamtunza na kuishi nae kwa amani na furaha basi huo ni utumiaji mzuri na nashauri watu wote wawatumie wapenzi wao hivyo kwa kuwajali katika kila hali. Kama mganga kamwambia lala na mlemavu huku ukimjali basi huyo mganga ni mzuri na anahitaji kuganga watu wengi zaidi hata wasio na ulemavu.
 
(Upendo, Ambwene)

Siku moja nilipigiwa simu,
Ilikuwa simu ya mwaliko,
J'pili tutamshukuru Mungu,
Kwa sadaka ya pekee,
Uje uimbe kanisani kwetu.

Muda ulipofika wimbo ukaimbwa,
Nao wakaja mbele,
Wametanguliza kijana na binti mmoja
Msemaji wao akaanza kutoa hotuba fupi kabla ya sadaka haijatolewa.

Mungu ninakushukuru sana Bwana,
Kwa kumponya binti yangu aliyeugua kichaa,
Pia ninakushukuru kwasababu kijana huyu alionesha "Upendo" wa ajabu
Nilipomwambia achana na mwanangu hakufai tena,
Yeye alijibu nimempenda nitaoa hivyo hivyo,
Sijawahi ona Upendo kama huu.

Upendo haupo katika maneno,
Unaonekana kwa matendo,
Hauonekani kwenye raha wathibitika wakati wa shida.

Daima upendo una sura mbili,
Japo wengi wanaijua moja,
Wakati wa raha, faraja na nyimbo na zawadi kedekede,
Wanaridhika na upendo huo
Ila upendo una kipimo chake
Wakati wa shida,wa raha na wakati wa magonjwa
Wakati ambapo waona tabia, kasoro na mapungufu hapo ndipo upendo hupimwa.

"Yule anayeweza kusimama na wewe,
Wakati wengine kwa kawaida wangekukimbia"

Tena awezaye kukufichia aibu wakati wengine kawaida wangekutangaza,
Yule ambaye hapendi kuona unaharibikiwa,
Hata mkikosana hapendi kuona unateseka,
Huyo ndiye mwenye upendo wa kweli.

"Watu duniani wanahangaika kupenda vinavyopendeza,
Wanasahau kupenda vinavyopendeza hakuna thamani isipokuwa kupenda visivyopendeka"
Kama mkiwapenda wale wawapendao mwafanya ziada gani,

Wapendeni waombeeni wanaowaudhi,
Baba yenu wa Mbinguni atawapa thawabu,
Na watu watasema huu ndio "Upendo wa kweli"
 
Wanakuwaga watamu sana hawa, halafu unakamua peke yako no sharing... Sasa unakutana na hawa mwezangu na mie wenye rangi mbili mbili, nywele bandia, kucha bandia, kule nako ni kama bwawani na lishimo likuubwa full kugawa na malingo mengi kumbe dah matatizo matupu kule ndani.. Mungu ambariki sana huyu jamaa.
 
Wanakuwaga watamu sana hawa, halafu unakamua peke yako no sharing... Sasa unakutana na hawa mwezangu na mie wenye rangi mbili mbili, nywele bandia, kucha bandia, kule nako ni kama bwawani na lishimo likuubwa full kugawa na malingo mengi kumbe dah matatizo matupu kule ndani.. Mungu ambariki sana huyu jamaa.
Ameen
 
kuna thawabu unaipata toka kwa Mwenyezi Mungu kama ukioa mlemavu, thawabu hiyo inaweza kuja kwako mwenyewe ama kwa kizazi chako utakachokipata; same as mjane.
 
Back
Top Bottom