Mbele ya Urusi, Marekani lazima ale kona!

Mbele ya Urusi, Marekani lazima ale kona!

Ukweli ni kwamba marekani ni waoga sana!! Saa wameshaanza kula kona! Eti wanadai hawajaamua bado wachukue hatua IPI kati ya nyingi zilizopo mezani pa Trump!! Wamesahau kuwa Trump ilikuwa awe kwenye ziara marekani ya kusini akaamua kuahirisha ili kusimamia mashambulizi ndani ya masaa 48! Hiyo ilikuwa ni siku ya jumamosi! Hayo masaa yaliisha mapema siku ya jumanne!! Baadaye wakasema ni ndani ya masaa 72! Hayo nayo yaliisha mapema jumatano! Leo alhamis wamekuja na ngonjera nyingine eti wanadai hawajaamua bado hatua za kuchukua!! Bila aibu wanasahau kuwa Trump aliiambia urusi ikae tayari maana missile ambazo ni "nice, new and smart" zinakuja!!! Lakini leo wameanza kula kona kwa aibu na kudai eti hawajaamua hatua za kuchukua kama wanavyodai hapa:
"The president has a number of options at his disposal and a number remain on the table," Ms Sanders said during a briefing on Wednesday evening."We haven't laid out any specific actions we plan to take," she added.
Ni punguani tu anayeweza kudhani marekani ana ubavu wa kuvuka mstari mwekundu uliowekwa na urusi!!
 
Zile S400 ni hatarii aisee ndio maana wanasita
Achana na hizo kwa sasa ana matoleo mapya ya S500 na juzi katoa jipya LA S600!!!
Anavyosema wakileta missile atazipangua hiyo lugha imewaingia vilivyo! Tusishangae Trump kula kona kiutu uzima!! Hapa wanadai eti marekani hawajaamua bado wachukue hatua zipi!!! Wakati trump alishatweet kuiambia urusi ikae tayari makombora yanakuja!! Kona ya marekani hii hapa!
"The president has a number of options at his disposal and a number remain on the table," Ms Sanders said during a briefing on Wednesday evening."We haven't laid out any specific actions we plan to take," she added.
Wenye akili zao washajua MTU mzima keshakula kona kitambo, chezea Putin wewe!!
Putin huwa habeep!! Anapiga!!! Kilichotokea Crimea wote mnajua!!! Alivamia akaitwaa na marekani akaishia kubweka tu!!
 
Nashindwa kuelewa umewaza nini ndugu, hivi kama muhanga(Syria) ingekua ndio nchi yako ungethubutu kuandika hivi, unaona ni jambo la mchezo kwa vile ww haikuathiri. Kumbuka kuna watu kule km ww wenye malengo km ya kwako wanaopenda kuishi kwa amani km unavyoishi wewe. Haikusadii chochote kwa Marekani ama Urusi akiwa mbabe kwa kuvuruga maisha ya wengine sisi sote ni Binadamu. Tafakari.
Kabsa kiongozi mm nahisi kuna baadhi yetu wanahisi kuwa Syria hawaishi binadamu kama sisi na wenye damu na malengo kama yetu. Inasikitisha kuona watoto wasiokuwa na hatia wakiangamia..
 
Nashindwa kuelewa umewaza nini ndugu, hivi kama muhanga(Syria) ingekua ndio nchi yako ungethubutu kuandika hivi, unaona ni jambo la mchezo kwa vile ww haikuathiri. Kumbuka kuna watu kule km ww wenye malengo km ya kwako wanaopenda kuishi kwa amani km unavyoishi wewe. Haikusadii chochote kwa Marekani ama Urusi akiwa mbabe kwa kuvuruga maisha ya wengine sisi sote ni Binadamu. Tafakari.
Mkuu uliyo yaongea ni kweli, lakini ushabiki unatoka rohoni so kuukataa ni mpaka ujitoe kwenye emotional feelings, mfano hata kama CCM inafanya mabaya lakini wafuasi hawakosi, lazima wawepo tu, I'm sorry bro.
 
Hivi hii vita tunayoishabikia haiwezi kutuathiri na sisi kwenye hizi nchi zetu maskini? Nauliza tu
 
Hivi hii vita tunayoishabikia haiwezi kutuathiri na sisi kwenye hizi nchi zetu maskini? Nauliza tu
Hatuna pa kuponea, hasa gonjwa hili la ukimwi linalohusu jamii nzima donor mkuu ni mmarekani sijui itakuwaje bajeti akiipeleka vitani
 
Putin kwa misimamo yake wananchi wake wanaweza wakabadirisha wenyewe katiba yao ili aendelee kuwa kiongozi wao kwa mda mrefu zaidi
 
Hatuna pa kuponea, hasa gonjwa hili la ukimwi linalohusu jamii nzima donor mkuu ni mmarekani sijui itakuwaje bajeti akiipeleka vitani
Hilo la ukimwi ni Miongoni mwa mambo mengi wanayotufadhili ndio maana nadhani si vizuri kushabikia hii mambo ya vita. Vile vile hata direct effeft(s) za hii vita zinaweza kutuumiza.
 
Back
Top Bottom