Tt4tat boy
Member
- Nov 26, 2015
- 45
- 11
Heshima kwenu wakuu, nina wasiwasi mkubwa sana hapo baadae katika hizi ajira za ualimu maana nikichunguza kuna shule kwa sasa walimu wanagawana maada za kufundisha hali hii inanipa shaka kidogo na kuniaminisha kuwa huenda walimu wametosha, nasema haya kwa sababu kuna mdogo wangu yupo chuo na aliniomba ushauri kuhusu kozi ipi asome mimi nikakurupuka kwa mbwembwe na mkwara mzito kuwa akasomee UALIMU sasa nikijaribu kuchunguza wadau wanavyo sema duu nakata tamaa kabisa maana nilikuwa sitaki dogo ahangaike kusaka ajira na ndo kwanza tupo first yea mwaka huu all in all Mungu yupo , kazi ni kazi, mnasemaje wadau kuhusu hili swala