Mbatia: Rais Magufuli si msafi

Mbatia: Rais Magufuli si msafi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
RAIS John Magufuli anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, jambo hilo linamwondoa kwenye orodha ya watu wasafi kama anavyotaka ifahamike hivyo,anaandika Pendo Omary.

James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi amemtaka Rais Magufuli kujisafisha kutokana na kashfa ya kuhusika katika kuuza nyumba za serikali kabala ya kusafisha watuhumiwa wengine wa ufisadi.

“Rais Magufuli anapaswa kujisafisha mwenyewe kwanza kutokana na kashfa inayomuhusu ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mbatia amesema “tumeona ni kwa namna gani Rais Magufuli anahangaika kupambana na ufisadi au uhujumu uchumi kwa kutumia nguvu kubwa kwa vidagaa na kuacha mapapa kama wale wa Tegeta ESCROW, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere ‘Terminal III’, makontena bandarini, IPTL, Richmond na Mradi wa Umeme wa Kinyerezi.

“Hivyo rais anapaswa kujisafisha kwanza kwa kuwa na yeye anatajwa kuhusika katika kashfa ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.

Mbatia amesema, katika kufanikisha hayo Rais Magufuli anapaswa kuacha kuongoza nchi kwa matamko badala yake aongoze kwa kufuata Katiba, Sheria na Kanuni za Nchi.

“Demokrasia imeendelea kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa. Kutokana na hali hiyo, nchi sasa iko kwenye hali mbaya katika; bunge kuingiliwa, hali ya maisha ya Watanzania kiusalama iko njia panda hususani Zanzibar.

Pia, kuna ukiukwa kwa haki za wananchi kutafuta na kusambaza taarifa na matumizi ya nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kwa kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani.

Aidha, amesema Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) imebaini athari za kiuchumi zitokanazo na uamuzi wa viongozi kufuatia matamko mbalimbali ya serikali.

Miongoni mwa athari hizo ni kupungua kwa mzigo bandarini ikiwa ni sambamba na watumiaji wa bandari wakihamia nchi jirani.

Chanzo:
Mwanahalisi
 
Ni nani alimwambia Rais Magufuli ni msafi?

Common sense inatuambia hakuna binadamu hapa duniani aliye msafi.

Kinachonifurahisha ni kwamba, kwa sasa Mbatia amechukua cheo cha Tumaini Makene bila ridhaa ya vikao vya CHADEMA huku NCCR-Mageuzi ikimfia polepole.

Huu wimbo wa kusema Rais Magufuli siyo msafi haukufanya kazi wakati wa kampeni za Urais lakini kwa vile hakuna nyimbo zingine mpya, ndio maana bado anaendelea nao.

Nadhani Mbatia hafamu kuwa siasa zinabadilika na kama habadiliki, basi siasa zitambadilisha na kumuweka yeye na NCCR-Mageuzi katika sehemu mbaya kisiasa.
 
RAIS John Magufuli anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, jambo hilo linamwondoa kwenye orodha ya watu wasafi kama anavyotaka ifahamike hivyo,anaandika Pendo Omary.

James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi amemtaka Rais Magufuli kujisafisha kutokana na kashfa ya kuhusika katika kuuza nyumba za serikali kabala ya kusafisha watuhumiwa wengine wa ufisadi.

“Rais Magufuli anapaswa kujisafisha mwenyewe kwanza kutokana na kashfa inayomuhusu ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mbatia amesema “tumeona ni kwa namna gani Rais Magufuli anahangaika kupambana na ufisadi au uhujumu uchumi kwa kutumia nguvu kubwa kwa vidagaa na kuacha mapapa kama wale wa Tegeta ESCROW, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere ‘Terminal III’, makontena bandarini, IPTL, Richmond na Mradi wa Umeme wa Kinyerezi.

“Hivyo rais anapaswa kujisafisha kwanza kwa kuwa na yeye anatajwa kuhusika katika kashfa ya uuzwaji wa nyumba za serikali,” amesema Mbatia.

Mbatia amesema, katika kufanikisha hayo Rais Magufuli anapaswa kuacha kuongoza nchi kwa matamko badala yake aongoze kwa kufuata Katiba, Sheria na Kanuni za Nchi.

“Demokrasia imeendelea kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa. Kutokana na hali hiyo, nchi sasa iko kwenye hali mbaya katika; bunge kuingiliwa, hali ya maisha ya Watanzania kiusalama iko njia panda hususani Zanzibar.

Pia, kuna ukiukwa kwa haki za wananchi kutafuta na kusambaza taarifa na matumizi ya nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kwa kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani.

Aidha, amesema Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) imebaini athari za kiuchumi zitokanazo na uamuzi wa viongozi kufuatia matamko mbalimbali ya serikali.

Miongoni mwa athari hizo ni kupungua kwa mzigo bandarini ikiwa ni sambamba na watumiaji wa bandari wakihamia nchi jirani.

Chanzo:
Mwanahalisi
Mbatia ni bonge la kiongozi mahiri wa kisiasa
 
Mh Rais leo nakupongeza sana kwa kutumbua majipu wale waliohusika kulitia hasara taifa na kulifanya taifa kuwa shamba la bibi. Kila mahali kulikuwa na hewa mh Mtukufu Rais endelea na kasi hiyo. Moto wa NSSF tumeona.

Nakuomba baba kuna huku nako tumepata hasara chonde chonde wahusika watumbue tu majipu haya hakuna namna tunakuombea sana.

1. Uuzaji wa nyumba za serikali
2. Vivuko vibovu
3. Meli ya Kichina ile MV Dar es Salaam haifanyi kazi licha ya kununuliwa kwa bil 8.
4. Pia wale wote waliohusika na mgao wa pesa za Escrow na zile chenji za za rada tujue zilifanyia nini.

Tuko pamoja kupinga ubadhirifu.a kutumbua majipu wale waliohusika kulitia hasara taifa na kulifanya taifa kuwa shamba la bibi. Kila mahali kulikuwa na hewa mh Mtukufu Rais endelea na kasi hiyo. Moto wa NSSF tumeona.

Nakuomba baba kuna huku nako tumepata hasara chonde chonde wahusika watumbue tu majipu haya hakuna namna tunakuombea sana.

1. Uuzaji wa nyumba za serikali
2. Vivuko vibovu
3. Meli ya Kichina ile MV Dar es Salaam haifanyi kazi licha ya kununuliwa kwa bil 8.
4. Pia wale wote waliohusika na mgao wa pesa za Escrow na zile chenji za za rada tujue zilifanyia nini.

Tuko pamoja kupinga ubadhirifu.
 
Watachonga weee lakini hawana jipya. Wamekosa cha kumkosoa Rais wangu JPM sasa wamebaki mara nyumba za serikali, mara mafisadi, mara amekandamiza demokrasia. Sasa ili mjue Rais wangu JPM anakerwa na ufisadi kaanzisha mahakama ya mafisadi.

Kuhusu kukandamizi demokrasia si kweli na pia demokrasia ni mikutano ya hadhara tu? Kwanza uzoefu unaonesha mikutano ya hadhara ya wapinzani imejaa uchochezi na matusi.

Uchaguzi umeisha mmeshindwa kaeni kimya subirini tena 2020. Mwisho hata huyo Mbatia naye si msafi mwambieni atoe boriti kwenye jicho lake kwanza ndo aone kakibanzi kwenye jicho la Rais wangu JPM.
 
JPM anahusika na kashfa nyingi tu, ikiwemo Meli Chakavu, kuhamisha fedha za umma kinyume na Mamlaka ya Bunge na kukandamiza Demokrasia ya Vyama vingi na Uhuru wa kupata Habari, kinyume na Katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea.

UUZWAJI WA NYUMBA ILIKUA NI SERA YA WAKATI HUO, KWAHIYO ULITAKAJE? NA HIZO PESA ALIPELEKA WAPI ? JE ALIFUNGUA AKAUNT NJE YA NCHI AU? JE ALIPELEKA CHATO, AU ZIMEFANYA MAMBO KWA MAENDELEO YA NCHI YAKE?
 
Watachonga weee lakini hawana jipya. Wamekosa cha kumkosoa Rais wangu JPM sasa wamebaki mara nyumba za serikali, mara mafisadi, mara amekandamiza demokrasia. Sasa ili mjue Rais wangu JPM anakerwa na ufisadi kaanzisha mahakama ya mafisadi. Kuhusu kukandamizi demokrasia si kweli na pia demokrasia ni mikutano ya hadhara tu? Kwanza uzoefu unaonesha mikutano ya hadhara ya wapinzani imejaa uchochezi na matusi. Uchaguzi umeisha mmeshindwa kaeni kimya subirini tena 2020. Mwisho hata huyo Mbatia naye si msafi mwambieni atoe boriti kwenye jicho lake kwanza ndo aone kakibanzi kwenye jicho la Rais wangu JPM.
fact
 
Mheshimiwa Mbatia unaheshimiwa sana tafadhali usijishushe hadhi yako kwa matamko ambayo hayatarajiwi toka kwako.

JPM hakuwahi kuwa na uwezo wa kuuza nyumba au mali yoyote ile ya serikali. Kwenye kuuzwa nyumba za serikali rightly or wrongly ilikuwa uamuzi wa baraza zima la mawaziri chini ya rais. Na hili lilifikiwa baada ya mjadala mrefu kuhusu nyumba hizo. Hivyo basi kumlaumu JPM eti kwa vile ametekeleza wajibu wake kisheria ni kutomtendea haki kabisa.

Kama unatafuta wa kumlaumu mbona Mzee Ben humchokozi? Tatizo la Escrow lilikuwa la kisheria mno na kwa mtu kama wewe unalifahamu vizuri sana.

Hisia zangu, rightly or wrongly ni kuwa huyu JPM anawanyima raha jinsi anavyokubalika na umma na kwa kiasi fulani mnahisi mkiendelea kunyamaza kimya basi mtakuwa hamna ajenda na hili ndiyo maana mara mnafunga midomo yenu, mara naibu spika hamumtaki[taratibu za kumng'oa mnazijua lakini hamfuati hizo].

Ushauri wangu ni kwamba kwa sasa tulieni. JPM yuko honeymoon. wananchi wengi wanamkubali na wanaamini kuwa muelekeo wa serikali yake ni mzuri kwao na honeymoon ikiisha mtapata tu mada za kuzungumzia.
 
Back
Top Bottom