hebu tusaidie wewe sasa; mitaala ni nini?
bado Mbatia yuko sahihi; muda aliotaka Mtaala wa Elimu uwasilishwe Bungeni aukuonekana; kwa maana haukuwepo kabisa tangu awali; sasa huu uliowasilishwa juzi kuna uwezekano mkubwa umeandaliwa fastafasta ili kuliondolewa Taifa aibu.
Kwamaana hii,Mh Mbatia atakuwa sahihi hakuna kitu kinaitwa mtaala au kimeandika mtaala.Mh MBATIA aliuliza je ni mtaala gani unatumika hapa nchi.?
sramble umejiambulisha kwenye thread moja wapo kwamba ni mwalimu na uko na M.A nijitambulishe kwako na mbele ya wana jf mi ni curriculum specilist,nakuomba usome makala ya mkumbo kwenye gazeti la raia mwema la leo uone jinsi unavyopotosha watu kuhusu hili suala la mitaala. Nilieleza pia kwenye thread yako ya jmosi iliyopita kuhusu suala hili la mitaala, naomba uwe professional zaidi ukiwa unasoma makala ya mkumbo kwani huo ndo ukweli kuhusu sakata hili la mitaala
unadhani hili suala ili kueleweka linataka maprofesa!soma makala ya mkumbo kwenye gazeti nililokuambia ameeleza kila kitu. Kama watu hautaelewa nitakuja na maelezo kutoka kwa wataalam mahiri wa mitaala hapa nchini,prof osaki,prof njabiri,prof chonjo etc
Mitaala: http://hakielimu.org/files/publications/nani%20haumua%20watoto%20wetu%20wajifunze.pdf
Mtaala kwa kuzingatia mambo 12.
• Kile kinachofundishwa shuleni
• Seti ya masomo
• Maarifa
• Programu ya masomo
• Seti ya vitu vya kujifunza
• Orodha ya kozi
• Seti ya malengo ya ufanyaji kitu
• Kozi ya kujifunza
• Kila kitu kinachoendelea shuleni, ukijumuisha mambo yanayofanyika nje ya darasa, usimamizi, na uhusiano kati ya mtu mmoja na mwingine
• Kila kitu kinachopangwa na wafanyakazi shuleni
• Mjumuiko wa uzoefu mbalimbali anaoupata mwanafunzi awapo shuleni
• Kile ambacho mwanafunzi hukipata kikiwa ni matokeo ya kuwa shuleni
sasa haya hapa juu tunayo kweli? na kama ni kweli tunayo kwa nini basi iwe inabadilika badilika mara kwa mara na nani ana jukumu kisheria la kufanya mabadiliko haya?
au serikali imepeleka bungeni Muhtasari wa ufundishaji.
Samahani kama ninarudia posting hii, kuna kitu inabidi kijadiliwe kwa kina hapo. Tume ya wabunge inaundwa kuthibitisha mtaala. Hivi tumefikia kiwango cha kuunda tume kuthibitisha nyaraka zinazotoka serikalini- na hasa mtaala unaotakiwa uwe ulikuwa unatumika? Shule zipo, walimu wapo, wanafunzi wapo, wizara ya elimu ipo- kwa ufupi Elimu ipo kwenye motion nchini. Kwa hiyo tulitegemea serikali ikisema mtaala ni huu, iwe hivyo.ru.
Mtaala wa elimu umewakilishwa na kuundiwa Tume ya wabunge 6 itakayodhibitisha mtaala huo chini ya mama Magreth Sitta.
Tugemee nini kama itathibitishwa kwamba mtaala huo upo???
sasa kama huna nyezo za kufundishia utasemaje una mitaala? ni sawa na kuandika mambo kwenye makaratasi then who cares wanafunzi wanapata nini at the end of the day.mitaala na mihutasari iliyopo hapa nchini imekidhi vigezo hivi vyote. o labda ni nyenzo za kufundishia lakini haya yote yameandikwa na kuchambuliwa kiufasaha
Sidhani kama amewasilisha mitaala ambayo ni published. Ninachojua amewasilisha rasmu ya mitaala ya elimu ya Tanzania. Hiyo published curriculum document ya Tanzania haikuwahi kuwepo, tangu ile ya Elimu ya kujitegemea ilipo perish. So iwe na itakavyokuwa, kama kweli waziri amewasilisha mitaala halisi basi tutataka atupe na ISBN namba ya publication ya hiyo mitaala na si draft.Tatizo sio kuwa na mitaala tu. je iliyopo ni mizuri? na je hata hiyo iliyowasilishwa ilikuwapo kabla? inafaa?
sasa kama huna nyezo za kufundishia utasemaje una mitaala? ni sawa na kuandika mambo kwenye makaratasi then who cares wanafunzi wanapata nini at the end of the day.
MBATIA aliapa bungeni kwamba Waziri wa Elimu atakapowakilishwa mtaala wa elimu atajiuzulu ubunge kwani haupo tangu tupate uhuru.
Mtaala wa elimu umewakilishwa na kuundiwa Tume ya wabunge 6 itakayodhibitisha mtaala huo chini ya mama Magreth Sitta.
Tugemee nini kama itathibitishwa kwamba mtaala huo upo???
My Take:
Nilimsikia MBATIA kwa kinywa chake akitoa ahidi na kuapa kupitia TBC live kutoka bungeni kwamba ataachia ngazi.
Mdomo nyumba ya maneno. Huwezi kuisukuma gari ukiwa ndani ya gari.
Mbatia hilo unalo timiza ahadi yako endapo itathibitishwa kwamba ulilidanganya bunge na Watanzania. Kama atagoma kujiuzulu basi bunge litumie busara kumfukuza ubunge ili ahadi yake itimie.