George J Minja
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 289
- 203
Mbatia amsema kuwa hakubaliani na mitalaa iliyowasilishwa ambayo ni ya elimu ya awali, msingi na sekondari.
Alisema kilichowasilishwa siyo alichokidai bungeni, mtalaa alioudai ulikuwa wa mwaka 1997 hadi mwaka 2005 wakati uliowasilishwa ni wa mwaka 1998 hadi 2008 ambao unasema ni kwa ajili ya Tanzania Bara.
"Huwezi kusema Mtalaa wa Elimu ya Sekondari ni wa Tanzania wakati huu uliopo unaonyesha ni wa Tanzania Bara wakati hata mtihani unaofanyika wa darasa la saba ni wa Tanzania.
"Kasoro nyingine ni kwamba katika vitabu vya mwongozo inatakiwa kuwa na Alama Ubora (ISBN) kwa kuidhinishwa na Bodi ya Maktaba, sasa mtalaa wa jana hauna hayo yote."
Kasoro ya tatu, Mbatia alisema alikataa muhtasari kwa kuwa haukuwa na saini ya Kamishna wa Elimu.
Alisema kuwa bado anasimamia hoja yake kuwa hakuna mitalaa ya elimu Tanzania na atasimamia hapo na atamwomba Spika suala hilo lijadiliwe na Wabunge wote kwa masilahi ya taifa, kwani mtalaa wa taifa hauwezi kutolewa kwa waraka