Mbatia 'aipa' CCM ushindi kuongoza Halmashauri ya Uvinza

Mbatia 'aipa' CCM ushindi kuongoza Halmashauri ya Uvinza

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Kitendo cha Mkiti wa NCCR James Mbatia kukataa makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa kati ya NCCR na CHADEMA kuongoza halmashauri ya Uvinza yamesababisha CCM kutumia mwanya huo na kutwaa nafasi ya Makamu Mkiti wa Halmashauri hiyo.

Kwa upande wa nafasi ya Mkiti uchaguzi umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena baada ya vyama vyote vitatu kushindwa kupata theluthi mbili ya kura.

Katika nafasi ya Mkiti vyama vyote vitatu viliweka wagombea ambapo CCM ilipata kura 8 CHADEMA kura 7 na NCCR kura 6.

Nafasi ya Makamu Mkiti mgombea wa CCM hakuwa na mpinzani na alipita bila kupingwa.

Katika makubaliano ya awali ngazi ya wilaya na mkoa vyama vya NCCR na Chadema vilikubaliana kuachiana nafasi ambapo ilukubaliwa CHADEMA igombee nafasi ya Mkiti na NCCR Makamu Mkiti.

Katika hali ya kushangaza siku ya kurudisha fomu vyama vyote viwili vilirudisha fomu nafasi ya Mkiti na NCCR ikakataa kugombea nafasi ya Makamu Mkiti hivyo mgombea wa CCM akapita bila kupingwa.

Inadaiwa Mkiti wa NCCR James Mbatia ndiye aliingilia kati kuvunja makubaliano ya vyama hivyo na hatimaye ushindi ukawa upande wa CCM
 
War has rules,mud wrestling has rules..!!politics has no rules...!!!Ross Perot..!!!
 
Mbatia analipa fadhila kwa Mwenyekiti wa CCM-Taifa kwani suala la kuteuliwa kuwa Mbunge si dogo kwake.Hapo ndipo ninapokubaliana na Kafulila kwamba Mwanaume aliyeshindwa na Mwanamke katika nafasi ya Ubunge hawezi kukiongoza chama ipasavyo!
 
Inasikitisha kweli kulikuwa na ushindi wa wazi kwa nafasi zote mbili iwapo vyama hivi viwili vya upinzani vingeafikiana, hali ndo hiyo na najua mwisho wa siku na hiyo nafasi ya mwenyekiti itaenda ccm
 
Nampongeza mh mbatia kwa kulipa fadhira ya kupewa ubunge vitu maalum na hivyo kuepushwa kufa kwa njaa. Kwa hatua hiyo mbatia inajimaliza na kumaliza chama chake. Hongera mbatia kwa kuwaonyesha watanzania ya kuwa, CHADEMA ni wapinzani pekee.
 
asingeipa ccmn ushindi angekuwa hajatimiza kauli isemayo 'HUWEZI KUZUNGUMZA WAKATI UNACHAKULA MDOMONI NA UMEKAA NA WAZEE MEZA MOJA'
 
Inasikitisha kweli kulikuwa na ushindi wa wazi kwa nafasi zote mbili iwapo vyama hivi viwili vya upinzani vingeafikiana, hali ndo hiyo na najua mwisho wa siku na hiyo nafasi ya mwenyekiti itaenda ccm

Ni kweli inavyoonekana NCCR wataunga mkono CCM kwenye nafasi ya Mkiti pia.
 
Hivi wana jf na Chadema mlitegemea nini hapo,Mbatia kuipa CDM uongozi? hili suala lilikuwa wazi iwe hivyo chini ya M/kiti Mbatia,NCCR ingekuwa inaongozwa na mtu tofauti anayejua na kuheshimu upinzani hapo ingepasa tulalamike lkn kwa Mbatia,tuseme tu ila tusiumize vichwa CDM wajipange uchaguzi ujao wafanye kweli wakae chonjo na huyo mlipa fadhila.
 
Hizi ndo akili za ki-bavicha(a),yaani kumbe nyie wapinzani hamkuweka mgombea na mwenzenu wa ccm amepita bila kupingwa mnawalaumu NCCR kwa lipi?

Mashirikiano mmeyaona kwenye halmashauri tu? bungeni je? Kweli hii mijitu haina kumbu kumbu!
 
Na ni nani aliwaambia CDM wafanye makubaliano na NCCR?!!!
Tulishaamua kuwa nakuna tena mkataba na shetani... na hata mke wa Loti alipogeuka nyuma akawa chumvi, Loti hakuangaika kuizoa ile chumvi, eti kwa sababu "ilikuwa mke wake"... Vyama vyote vya siasa Tanzania vipo pamoja na vimeshikamana katika kuwadhulumu wananchi wa hii nchi, isipokuwa CDM peke yake.

Hivi CDM walisahahu NCCR walipoungana na CUF na CCM kubadilisha vifungu vya kanuni za bunge?!!!

Tusirudie tena hilo kosa....
 
Kwani hawa CHADEMA si ndo walikataa kuungana na vyama vingine vya upinzani kuunda kambi ya upinzani? Leo hii wanataka ndoa na NCCR MAGEUZI kwa ajili ya Meya wa Uvinza! wakumbuke kuwa ukiwa mchoyo basi ujifunze na kutoomba
 
kwani hawa CHADEMA si ndo walikataa kuungana na vyama vingine vya upinzani kuunda kambi ya upinzani? Leo hii wanataka ndoa na NCCR MAGEUZI kwa ajili ya Meya wa Uvinza! wakumbuke kuwa ukiwa mchoyo basi ujifunze na kutoomba

Kama unataka kupotosha, jua unapotosha tu waliozaliwa baada ya 2010... Vyama vyote vya upinzani vyenye wabunge ndivyo vilivyokataa kujumuishwa kwenye kambi rasmi ya upinzani. JF yenyewe inatosha kukukumbusha, nenda kwenye previous threads kama umesahau...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom