Mbatia aibwaga NCCR Mageuzi mahakamani

Mbatia aibwaga NCCR Mageuzi mahakamani

Tut
View attachment 3348690
Aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ameshinda kesi aliyoifungua dhidi ya chama hicho, akipinga kuondolewa kwenye uongozi na kuvuliwa uanachama wake.

Mbatia aliemnguliwa madarakani kufuatia mkutano mkuu wa NCCR Mageuzi uliofanyika Septemba 24, 2022, ambapo pia ulimvua uanacama, jambo alilopinga katika shauri la madai nambari 18/2023 (Judicial Review) alilofungua Mbatia dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya chama hicho.

Akitoa hukumu hiyo leo Mei 28, 2025, Jaji Jaji A. Kagomba wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Kuu Dodoma, ametengua uamuzi wote wa Mkutano Mkuu wa NCCR-Mageuzi wa Septemba 24, 2022 uliopindua uongozi wa Mbatia na kukubaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo Jaji Kagomba amesema hoja ya kwamba, Ndugu James Mbatia hakuwa mwanachama wa Chama cha NCCR-Mageuzi kwa sababu kadi yake ni ya mwaka 1992 wakati usajili kamili ni wa mwaka 1993; haina mantiki yoyote kwa sababu mwaka 1992 ilikuwa ni usajili wa muda wa vyama vya siasa na ndio wanachama hao waliowezesha chama kupata usajili wa kudumu hata Katiba ya NCCR-Mageuzi ni ya mwaka 1992.

Kuhusu uamuzi ya mkutano Mkuu wa Septemba 24, 2022 Jaji amesema haukumpatia haki ya msingi (Natural Justice) Mbatia ya kusikilizwa hivyo ulikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya chama cha NCCR-Mageuzi na sheria za vyama vya siasa.

Pia, Jaji ametengua maamuzi yote yaliyofanywa na Mkutano huo ya kumuondolea Ndugu Mbatia uanachama na Uenyekiti wa Chama, akikitaka pia chama hicho kulipa gharama zote za kesi.

Akizungumzia hukumu hiyo, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Joseph Selasini amesema wataikatia rufaaa.

“Sisi tumepokea uamuzi huo, lakini tutaukatia rufaa. Ieleweke kwamba Mbatia aliondolewa kwenyekiti na tutafanya utaratibu asirudi kwenye uenyekiti kwa kukata rufaa,” amesema Seasini.
Tutaona mengi
 
Una uhakika huu utumbo uliuouandika?

Msajili ndiye aliyetambua uamuzi wa Mkutano Mkuu feki wa NCCR-Mageuzi na kumtambua Mhaini na Msaliti Joseph Selasini kuwa Mwenyekiti halali wa Chama.
Asante kwa ufafanuzi. Maana jamaa kaandika full lugha gongana. Anakubali na kukataa mtawalia.
 
Mbatia alimlalamikia nani kwamba ^amebariki mkutano uliomvua uanachama^?

Unaposema ^msajili alikuwa upande wa NCCR,^ unazungumzia nini au akina nani?
Umekuja mbio sana, ila ungeanza kusoma nilipo mquote hugo mtu.
Alisema ni aibu,
nikamuuliza aibu kushinda kesi?,
Akajibu msajili anahusika.

Mitazamo yetu ilikuwa tofauti, mimi naongelea alieshinda kesi kumbe yeye anamuongelea alieshindwa kesi.
 
Asante kwa ufafanuzi. Maana jamaa kaandika full lugha gongana. Anakubali na kukataa mtawalia.
Tatizo mnakurupuka sana.
Hoja ilikuwa msajili kuhusika kwenye ushindi wa Mbatia mahakamani ndio nimepinga.
 
Halafu utasikia NCCR imekata rufaa halafu watambwaga yeye mahakamani hivyo ndivyo wanataka na sisi CHADEMA tuwe hivyo lakini so far wameangukia pua mpaka wanamtuma Msajili feki aifute CHADEMA 🤣🤣
 
Tatizo mnakurupuka sana.
Hoja ilikuwa msajili kuhusika kwenye ushindi wa Mbatia mahakamani ndio nimepinga.
Jamaa amekuuliza iwapo msajili ndiye alichochea na kubariki mapinduzi ya Mbatia, ukasema hapana na ndiyo kwa wakati mmoja (rejea hapa chini).

Sasa umegeuza gia kwamba ulikuwa unazungumzia ushindi??!

Au umeonja kidogo leo?
1748436776315.png
 
Kwani kuna swali hapo? 🤣🤣👋 Watu ving'ang'anizi. Baadhi tulishasahau shauri hili. Kha!
 
Akitoa hukumu hiyo leo Mei 28, 2025, Jaji Jaji A. Kagomba wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Kuu Dodoma, ametengua uamuzi wote wa Mkutano Mkuu wa NCCR-Mageuzi wa Septemba 24, 2022 uliopindua uongozi wa Mbatia na kukubaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa
Pigia mstari :

uamuzi wote wa Mkutano Mkuu wa NCCR-Mageuzi wa Septemba 24, 2022 uliopindua uongozi wa Mbatia na kukubaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa

Msajili wa vyama vya siasa chali, anatumika vibaya sana.
 
View attachment 3348690
Aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ameshinda kesi aliyoifungua dhidi ya chama hicho, akipinga kuondolewa kwenye uongozi na kuvuliwa uanachama wake.

Mbatia aliemnguliwa madarakani kufuatia mkutano mkuu wa NCCR Mageuzi uliofanyika Septemba 24, 2022, ambapo pia ulimvua uanacama, jambo alilopinga katika shauri la madai nambari 18/2023 (Judicial Review) alilofungua Mbatia dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya chama hicho.

Akitoa hukumu hiyo leo Mei 28, 2025, Jaji Jaji A. Kagomba wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Kuu Dodoma, ametengua uamuzi wote wa Mkutano Mkuu wa NCCR-Mageuzi wa Septemba 24, 2022 uliopindua uongozi wa Mbatia na kukubaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo Jaji Kagomba amesema hoja ya kwamba, Ndugu James Mbatia hakuwa mwanachama wa Chama cha NCCR-Mageuzi kwa sababu kadi yake ni ya mwaka 1992 wakati usajili kamili ni wa mwaka 1993; haina mantiki yoyote kwa sababu mwaka 1992 ilikuwa ni usajili wa muda wa vyama vya siasa na ndio wanachama hao waliowezesha chama kupata usajili wa kudumu hata Katiba ya NCCR-Mageuzi ni ya mwaka 1992.

Kuhusu uamuzi ya mkutano Mkuu wa Septemba 24, 2022 Jaji amesema haukumpatia haki ya msingi (Natural Justice) Mbatia ya kusikilizwa hivyo ulikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya chama cha NCCR-Mageuzi na sheria za vyama vya siasa.

Pia, Jaji ametengua maamuzi yote yaliyofanywa na Mkutano huo ya kumuondolea Ndugu Mbatia uanachama na Uenyekiti wa Chama, akikitaka pia chama hicho kulipa gharama zote za kesi.

Akizungumzia hukumu hiyo, Mbatia amesema ataanza kuchukua hatua mapema kuitekeleza.

"Hiyo ni judicial review (mapitio ya mahakama) haina haja ya kusubiri wakate rufaa, kwa hiyo nitachukua hatua mapema," amesema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Joseph Selasini aliyesema kuwa ameiona hukumu hiyo, amesema kwa maoni yake Mahakama haijamrejeshea uenyekiti Mbatia, bali inataka apewe muda wa kujitetea.
"Kwa mujibu wa hukumu ile, Mbatia hakupewa nafasi ya kujitetea katika mkutano mkuu, maana yake ni kwamba ni lazima uitishwe mkutano mkuu ili aitwe ajitete. Haimaanishi kwamba Mahakama imetengua uamuzi wa mkutano mkuu uliofanyika pale Jeshi la Wokovu (Dar es Salaam)," amesema.

Amesema uamuzi wa kukata rufaa utafikiwa na vikao vitaka'vyotafakari hukumu hiyo.
"Ni lazima tuitishe kikao cha kamati kuu haraka kujadili hiyo hukumu, halafu kwa ushauri wangu chama kiitishe mkutano mkuu ili Mbatia apewe nafasi ya kujitetea na kisha chama kitatafakari. Lakini Jaji hakutengua uamuzi wa mkutano mkuu na kwa hiyo Mbatia hawezi kuingia ofisini kutekeleza majukumu yake," ameongeza.

Ccm washaona fursa ya kumtumia
 
Bashiru Ally kakurwa alimuingiza chaka.

Kama ambavyo Chaumma wameingizwa
Mbatia mwenyewe mwaka 2020 aliingizwa chaka na Magufuli ya kupewa majimbo, akapewa na ulinzi lakini akaja kumgeuka. Hawa ni watenda dhambi wanakaangana wenyewe kwa wenyewe. Bado na CHAUMMA litawafika tu.
 
Umekuja mbio sana, ila ungeanza kusoma nilipo mquote hugo mtu.
Alisema ni aibu,
nikamuuliza aibu kushinda kesi?,
Akajibu msajili anahusika.

Mitazamo yetu ilikuwa tofauti, mimi naongelea alieshinda kesi kumbe yeye anamuongelea alieshindwa kesi.
Wewe ndiye ulikurupuka rudia tena kusoma , mimi nilisema post #9 aibu nyingine kwa msajili, umekimbilia kumwaga matusi ya nguoni kwa kukuelekeza kuwa umenukuu vibaya.
 
Kwa namna akina Mbatia walivyomuondoa Mrema Augustino na Mbatia alivyomuondoa Marando na matendo yake mengine ya kichawa kwa Serikali,siwezi kumuunga mkono.
Ule msemo wa "What goes around comes around" ndiyo unadhihirisha.
 
Kama yanayomkuta Mrisho Gambo kule Arusha, ni yale yale alimfanyia Godbless Lemma.
 
Back
Top Bottom