Dodoma: Rais Samia afanya mkutano na Wanawake ukumbi wa Jakaya Kikwete

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879

Wanawake zaidi ya 10,000 Mkoa wa Dodoma makundi mbalimbali wanatarajiwa kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan Juni 8 mwaka huu katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Hayo yamesemwa leo Juni 6,2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, amesema Rais Samia atazungumza na wanawake wa Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya kina mama wa mikoa yote.

Wakina mama kwa uwakilishi wao wa makundi mbalimbali kutoka wilaya za Dodoma na maeneo ya karibu wamepewa mwaliko wa kushiriki kwenye mkutano huo,” amesema Mtaka.

Aidha, ametaja makundi hayo kuwa ni pamoja na wabunge wanawake bila kujali wapo chama gani, madiwani na makundi kama wajasiriamali, mama ntilie na kila aina ya kina mama watapata nafasi ya kuwakilishwa na wenzao.

=====

RAIS SAMIA: WANAWAKE NI CHACHU YA MAENDELEO, HATUTAKIWI KUWA WANYONGE

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema hakuna Taifa linaloweza kupiga hatua pasipo kuwategemea Wanawake kwasababu wao ni Taifa kubwa (wengi kuliko Wanaume) na wanailea Dunia

Ameeleza hayo leo wakati akizungumza na Wanawake Jijini Dodoma ambapo ameongeza kuwa, mchango wao ni mkubwa katika shughuli za Maendeleo

RAIS SAMIA AWATAKA WANAWAKE KUJITATHMINI

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wanawake kutathmini jitihada zinazofanywa kuwawezesha Kiuchumi akisema Mifuko 61 ya Uwezeshaji imeanzishwa tangu Uhuru

Ameeleza, "Jumla ya Trilioni 2.2 zimetolewa kwa Wanawake, waliofaidika ni Milioni 5.3. Kama pesa yote hii iliingia mikononi kwa Wanawake toka Uhuru hadi leo ni vema kutathmini zimefanya nini? Tuna Maendeleo gani? Je, zote zimeingia mikononi kwa Wanawake?"

RAIS SAMIA: PENGO LA KIDIGITALI KATI YA WANAWAKE NA WANAUME LAZIMA LIZIBWE

Rais Samia Suluhu amesema ili Tanzania iweze kwenda na Uchumi wa Viwanda, lazima pengo la kidigitali kati ya Wavulana na Wasichana lizibwe

Amesema, "Dunia ya leo inaendeshwa kwa Mifumo ya Kidigitali. Tafiti zinaonesha kuna pengo kubwa kwenye matumizi ya mifumo hii kwa Wanawake na Wanaume. Wao ni wepesi zaidi kutumia mifumo ya kidigitali kuliko Wanawake"

RAIS SAMIA: WANAWAKE KUMILIKI MALI BADO CHANGAMOTO

Amesema licha ya kutungwa Sera na Sheria mbalimbali, Wanawake wengi hawana uwezo wa kumiliki mali ikiwemo Ardhi na Nyumba kwasababu mbalimbali ikiwemo Mila na Desturi

Amesema, "Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni 7.4% ya Wanawake ndio wana umiliki wa nyumba ya peke yao ikilinganishwa na 25.6% ya Wanaume. Wanaomiliki Ardhi peke yao wapo 8.1%"

Ameeleza, hali hiyo imekuwa ikiwakwamisha Wanawake kujiinua kiuchumi kwani Nyumba na Ardhi ndio hutumika kama dhamana Benki

WIZARA YA AFYA YAAGIZWA KUWEKA MPANGO MZURI WA MADENI KWA WANAOFARIKI

Rais Samia Suluhu Hassan amemwagiza Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima kuweka Mpango mzuri kwenye suala la kudaiwa pale Mgonjwa anapofariki dunia

Amefafanua, "Nataka Wananchi wanielewe, sio kwamba deni lisilipwe. Kuwekwe Mpango mzuri bila kuzuia maiti. Moja kati ya mpango ni kutoa gharama za matibabu wakati yanaendelea bila kusubiri siku ya mwisho. Hiyo sio sawa"
 
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anafanya mkutano na wanawake wa makao makuu ya nchi jijini Dodoma na kuzungumza na taifa.
Mkutano huu unafanyika leo tarehe 08/06/2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete (Jakaya Kikwete Convention Center).

Muda mfupi kutoka sasa Rais anatarajia kuwasili. Mwanamke ni nguzo ya maendeleo.

Fuatilia hapa matangazo ya moja kwa moja
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amekiri kuwa kushindwa kwa Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulitokana na kuweka wagombea dhaifu kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo uraisi na hivyo wamejifunza na uchaguzi ujao wataweka wagombea wenye nguvu na ushawishi watakaozunguka nchi nzima kunadi sera na ajenda za wanachi.

Mbowe amesema Chadema haijawahi kuishiwa ajenda za kupambana na ccm.

My take.

Watakiri yote waliyomsingizia mwendazake laana ya kumtukana imeanza kuwatafuna.

Kumbe waliweka wagombea dhaifu alafu wakasingizia wameibiwa kura na mwendazake. Hovyo kabisa.

Kapimwe akili
 
So lissu ni dhaifu fainali ukweli unasemwa..
 
Kazi Inaendelea
 
Dada Etwege huu uzi ni kuhusu mama samia kuongea na wanawake wenzio huko dodoma
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amekiri kuwa kushindwa kwa Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulitokana na kuweka wagombea dhaifu kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo uraisi na hivyo wamejifunza na uchaguzi ujao wataweka wagombea wenye nguvu na ushawishi watakaozunguka nchi nzima kunadi sera na ajenda za wanachi.

Mbowe amesema Chadema haijawahi kuishiwa ajenda za kupambana na ccm.

My take.

Watakiri yote waliyomsingizia mwendazake laana ya kumtukana imeanza kuwatafuna.

Kumbe waliweka wagombea dhaifu alafu wakasingizia wameibiwa kura na mwendazake. Hovyo kabisa.

Laana imempata aliyeiba uchaguzi hadi kafa!
 
HII BAND INAYO PIGA LEO INA PIGA NYIMBO ZA TAIFA GANI ?
BAND IMECHEMKA SANAA
 
Huo ukumbi seating ni watu max 3,000.. hao 10,000 wanakaa wapi?? Kwenye kenchi?? 😂

Everyday is Saturday................................😎
 
Back
Top Bottom