Mbaroni kwa kumbaka mwenye mtindio wa ubongo

Mbaroni kwa kumbaka mwenye mtindio wa ubongo

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
Polisi mkoani Ruvuma inamshikilia mfanyabiasharaJamali Nassoro (67), mkazi wa eneo la Making'inda manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito msichana mwenye matatizo ya mtindio wa ubongo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma George Chiposi, alisema kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo kumetokana na wazazi wa msichana kubaini kuwa mtoto wao yupo tofauti kimaumbile na baada ya kumpima alionekana ana ujauzito wa miezi mitano.
Chiposi alisema wazazi hao walimhoji binti yao ambaye alieleza kwa shida kuwa alikamatwa kwa nguvu na kulazimishwa kutoa nguo yake ya ndani na Nassoro ambaye alimtaka ampelekeemaji ya kuoga chumbani kwake.
Alisema wazazi wa msichanahuyo ambao hakutaka kuwataja majina yao walifanya upelelezi wa kina ambao uliwaridhisha kuwa tukio hilo limefanywa na mfanyabiashara huyo ambaye alikuwa amekaribishwa kuishi kwenye nyumba yao baada ya kutengana na mke wake wakati akisubiri kugawana mali walizochuma.
Mtuhumiwa huyo hivi sasa anashikiliwa na polisi katika hospitali ya mkoa wa Songea, ambako amelazwa akidai kuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu kushuka.
Alisema kesho (Jumatatu) anatarajiwa kufikishwa mahakamani hata kama atakuwa hajaruhusiwa, atasomewa mashtaka yake akiwa kitandani.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Benedkto Ngaiza, amethibitisha kumpokea mfanyabiashara huyo ambaye alipelekwa hopitalini hapo akiwa chini ya ulinzi mkali.
CHANZO: NIPASHE
 
hizi kesi sizipendi ahasiwe tuuu,tuone kama atanyanyua kichwa tena kwa warembo
 
Back
Top Bottom