Mbagala-Posta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbagala-Posta

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mentor, Jul 13, 2011.

 1. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,712
  Likes Received: 8,264
  Trophy Points: 280
  Jumatatu asubuhi.
  Saa kumi na mbili kasoro nipo kituoni Mbagala kuu...
  Kinachonishangaza ni wingi wa wanafunzi waliopo hapo wakingojea magari kwenda mashuleni.
  Ni wengi sana kwa kweli..wangetosha kujaza madarasa mawili hivi...hapo sijaongezea tuliokutana nao vtiuo vilivyofuata;
  Njia panda, upendo, zahanati, kijichi, misheni!
  Tukaanza kugombania nao magari...
  Kuingia ndani nashangaa kuwaona wanasinzia huku wameshikilia chuma, wengine wamelaliana.

  Nikajiuliza swali..
  IWEJE HIVI? Yani mtu unatoka Mbagala kuu mpaka Posta kwenda shule tu?
  Na shule yenyewe ni hizi hizi za St. Kayumba?!
  Je, ni kutafuta elimu bora?
  Je ni shinikizo la wazazi ama watoto wenyewe?
  Je huko kote hakuna shule za kuwapeleka mpaka aende posta?

  Nikajisemea kabla sujahukumu, najua kuna wadau watakua wanao uelewa labda kwanini haya yanatokea.
  Naombeni mnisaidie jameni...

  Halafu mwanafunzi huyohuyo unakutana naye jioni akigombania magari...
  mara afukuzwe na kondakta
  mara apigwe kikumbo na mkaka anayegombania kuingia pia kwenye gari awahi kujipikia matembele yake ale apumzike ajiandae hekaheka za kesho pia,
  kufika kwake nyumbani mwanafunzi huyu ni saa mbili usiku.

  Akifika nyumbani anakuwa na uwezo kweli wa kusoma zaidi?
  au hata muda wa kukaa na kuongea na wazazi ataupata kweli?
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  This is a very important finding!!!. Kama ni shule zile za Kayumba, hakika hakuna mtoto kumpeleka mbali na nyumbani. Hii ni kwa sababu out put ya shule zote za kayumba iko sawa Tanzania nzima. Nasema kitu ambacho nakifanya. Mtoto wangu anasoma government primary school, siwezi kumtoa mbagala kwenda temeke kwa shule za aina hiyo hiyo.
  WAZAZI TFAKARI, CHUKUA HATUA
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,712
  Likes Received: 8,264
  Trophy Points: 280
  Na nadhani pia tofauti yao kwenye performance na maadili itakuwa tofauti pia.

  Wengine leo nimeona wakienda nao asubhi wanagombania magari wote..hiyo ni sawa, ila wanachosahau ni jioni watoto wanabaki wakigombea na kutukanwa wenyewe!!
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ni mateso sana, tuliosoma shule za mbali na nyumbani tunayaelewa vizuri hayo mateso.
   
 5. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli ufanyike utaratibu wa kupeleka watoto wetu katika shule zilizopo karibu na kwetu kupunguza kero hizi. Yaani baada ya pilika zote hizo mwanafunzi anaishia kupata IV ou zero. Yaani haileti tija hata kidogo. Wazazi na wanafuzi tafakaini suala hili kwa umakini wa hali ya juu
   
Loading...