Mbunge wa CCM
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 475
- 22
Ndoa zinabadilika. Zamani, kabla dini hazijaingia, dhana ya ndoa ilikuwa tofauti sana na ilivyo sasa katika jamii nyingi za kiafrika (Tanzania ikiwemo).
Katika jamii nyingi, ndoa za wake wengi ilikuwa sio 'dhambi'. Ingawa mfumo huu ni mbaya na haukubaliki (kwa mawazo ya sasa), lakini ulikuwa unampa uhuru mwanaume kuoa atakavyo tofauti na sasa. Hivyo katika 'mji', baba (mwenye mji) alikuwa na nyumba yake na kila mke alijengewa nyumba yake na watoto wakubwa na nyumba yao (hivyo mji unakuwa na nyumba at least tatu!). Hii ilipunguza kwa kiasi kikubwa mwanaume kuwa chini ya himaya mwanamke mmoja (kama ilivyo sasa).
Jingine ni separation kati ya wanawake na wanaume. Kulikuwa hakuna kukutana kwa mara kwa mara kati ya wanawake na wanaume katika social activities kama ilivyo leo. Kumbuka hakukuwa na shule kwa maana tunayoijua leo au kazi za maofisini nk ambazo zinawakutanisha wanaume na wanawake katika njia ambayo inarahisisha sana kufanyika kwa zinaa. Kutengishwa huku kulifanya iwe vigumu kufanya zinaa kama ilivyo sasa. Kama umempenda binti route ya kumpata ilikuwa ni kuoa(hata kama ni mke wa pili au tatu) na si vinginevyo!
Nimesema hayo machache, kujaribu kuonesha kuwa huwezi kuitizama ndoa peke yake kama unataka kuleta mabadiliko. Ni lazima uangalie social system yote na mabadiliko ni lazima yawe kwenye system nzima. Mimi naamini mabadiliko haya yanatokea yenyewe taratibu kadri muda na driving factors zote kwenye social system zinavyobadilika.
great thinking hii mkuu, big up