Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,876
- 2,744
ni ndoa chache zenye uwezo wa kuishi bila mitafaruku ya ajabu katika kipindi chote cha kuwa wawili. vipindi vya mapenzi na uchumba huwa tofauti na kipindi cha kuwa ndani ya ndoa. watu husema mengi tu juu ya wenza wao ikiashiria kuchokana ila kwa vile wako ndoani hawana namna. sijaoa ila hayo maisha nimeshayapitia. kipindi cha mitafaruku ya hapa na pale kimbilio huwa ni kitulizo nje ya ndoa (uzinzi). i wish mke na mume wasingekuwa wanakaa nyumba moja kwa lazima kama mfumo wa sasa wa ndoa unavyodai. mume anaweza kuishi kimara na mke tabata na wakawa wana maisha mazuri tu. kinacholeta wivu ni ile hali ya kujua sasa huyu yuko ndani ya himaya yangu (si mwanamke wala mwanaume). kila mmoja yuko kwenye himaya ya mwenzake. kwa nini mtu anafurahia kuwa na hawara? mke kaachwa, wanandoa wamepigana, mume kaachwa, mke/mume kazini, watoto wanateseka, mtoto hamjui baba/mama. imebaki kuvumiliana tu. why? hakuna mbadala wa mfumo huu wa ndoa? kwani ndoa ni kanuni isiyobadilika? hapa jamvini najua mpo mliohitilafiana na wenza wenu. kwa nini mnaishi kimungumungu hadi kifo kiwatenganishe? raha mara nyingi ndani ya ndoa ni suala ma masaa na siku, ila wakati wote mwingine ni kuwindana. tujadilini labda tunaweza kupata mfumo mbadala wa maisha ya sasa ya ndoa. try to think