Mbadala wa Mwenge wa Uhuru ni UPI?

Mbadala wa Mwenge wa Uhuru ni UPI?

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
40,161
Reaction score
51,348
Wakosoaji wanadai gharama za mwenge ni kubwa sana kuliko faida zake!

Napingana nao! Kwangu Mimi mwenge wa Uhuru naona kama bado thamani yake haijawahi kupatikana! Mwenge wa Uhuru ni moja kati ya Alama tano zinazolitambulisha Taifa hili!

Ukiachana na hizo nyingine 4, ambazo tukishakubali kuiondoa hiyo moja bila shaka nazo zitaonekana kero, watakuja watu na argument zao kudai bendera ya Taifa nayo iondolewe kwakua ni gharama kuitengeneza, au alama ya bibi na bwana nayo iondolewe kwakua haipendezi labda, au watasema tu, badala ya twiga alama ya taifa iwe mamba!

Binafsi thamani ya mwenge ni zaidi ya fedha! Tunu ya Taifa hakuna mbadala! Ni utambulisho wetu, ndio sisi! Taifa halina thamani!

Tunapoamua kukataa asili yetu, tuwe makini. Tukiondoa mwenge , nini utakua mbadala yake!

Mara zote wanaposema tuuondoe mwenge ambao moja wapo ya alama za taifa, nakumbuka kauli hii ya Mwl. Nyerere akisema;
" Tunataka kuuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu,ulete Tumaini pale ambapo Hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki, na heshima palipojaa dharau"

Ukisoma kauli hiyo ya Baba wa Taifa utaiona thamani halisi ya mwenge tunaouanza kuukana kama moja ya alama zinazotutambulisha!

Maendeleo ya kimagharibi na kujifanya ujuaji ndio kunakoleta hoja chochezi dhidi ya asili yetu. Ni mtu asiyejitambua pekee ndiye mwenge uwezo wa kukana hata asili yake!

Ni aibu kwa Mtanzania yeyote kuuona mwenge kama chukizo badala ya kuulinda kama moja ya utambulisho wake kama RAIA!

Ni rai yangu kuangalia namna ya kuboresha mbio za mwenge badala ya kuiondoa kabisa alama hii muhimu kwa Taifa letu!
 
Mtanzania wa kawaida anafaidika namna gani kimantiki?
Mtanzania wa kawaida anafaidika vipi na uwepo wa alama ya bibi na bwana, au bendera ya taifa, au wimbo wa taifa?
 
Mwenge umepitwa wakati. Ulikuwa na thamani wakati ule kwa sababu zile lakini mahali pake sasa ni katika jumba la makumbisho ya taifa. Kama jumba lile la Ikulu pale magogoni limepitwa na wakati (kulingana na JPM) na litakuwa jumba la maonyesho baada ya serikali kuhamia Dodoma, na kama majengo yote ya wizara yaliyoko Dar sasa yatauzwa, sembuse Mwenge? Mwenge ni tofauti na bendera, ni tofauti na nembo ile ya taifa. Ni wakati wa mwenge kupumzishwa mija kwa moja.
 
Malengo ya kuanzishwa kwake bado yanaishi! Aliyepitwa na wakati ni wewe!
 
Na mimi nauliza kwani utambulisho wake mpaka uzunguke nchi nzima kwanini usiwekwe makumbusho ili sisi tuharibu gharama zetu kwenda kuuona tofauti na sasa hivi maana tunakwepana nao ukiingia sisi tunatoka, ukitoka sisi tunaingia.

Bora uwekwe makumbusho ili tuwe tunaharibu fedha zetu kuufata huko makumbusho
 
Mwenge wa Uhuru hauna faida yoyote kwa nchi yetu, Mbio za mwenge zimekuwa ni mbio za kutafuna pesa za watanzania, kusumbua watu, kueneza ukimwi na kuwapotezea watu muda.

Sio lazima alama ya Taifa iwe inakimbizwa mitaani, mwenge upelekwe makumbusho tu.
Mbona hatuoni alama zingine za taifa zikikimbizwa mitaani?

Binafsi ningependa Tanzania tupate KATIBA MPYA na hiyo iwe ndio mbadala ya mwenge, na kila mtanzania atajivunia na Katiba ya nchi yake, na hiyo inaweza kuwa alama ya taifa letu.
Kama Wakristo wanaweza kujivunia kwa Biblia yao au waislamu wanaweza kujivunia kwa Quran yao, Kwanini watanzania tusijivunie na Katiba mpya?
 
sioni faida au hasara za mwenge kama utakimbizwa itaniathiri vp na kama hautakimbizwa nitafaidika,vp me naona sawa ilo fungu ambalo tunaisi linapotea kwa ajili ya mwenge sanasana litaishia kutafunwa tu na watu waliokaa kwenye uo mkondo! faida za mwenge bado ni utata ni kama ishu za kiimani ivi
 
Wakosoaji wanadai gharama za mwenge ni kubwa sana kuliko faida zake!

Napingana nao! Kwangu Mimi mwenge wa Uhuru naona kama bado thamani yake haijawahi kupatikana! Mwenge wa Uhuru ni moja kati ya Alama tano zinazolitambulisha Taifa hili!

Ukiachana na hizo nyingine 4, ambazo tukishakubali kuiondoa hiyo moja bila shaka nazo zitaonekana kero, watakuja watu na argument zao kudai bendera ya Taifa nayo iondolewe kwakua ni gharama kuitengeneza, au alama ya bibi na bwana nayo iondolewe kwakua haipendezi labda, au watasema tu, badala ya twiga alama ya taifa iwe mamba!

Binafsi thamani ya mwenge ni zaidi ya fedha! Tunu ya Taifa hakuna mbadala! Ni utambulisho wetu, ndio sisi! Taifa halina thamani!

Tunapoamua kukataa asili yetu, tuwe makini. Tukiondoa mwenge , nini utakua mbadala yake!

Mara zote wanaposema tuuondoe mwenge ambao moja wapo ya alama za taifa, nakumbuka kauli hii ya Mwl. Nyerere akisema;
" Tunataka kuuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu,ulete Tumaini pale ambapo Hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki, na heshima palipojaa dharau"

Ukisoma kauli hiyo ya Baba wa Taifa utaiona thamani halisi ya mwenge tunaouanza kuukana kama moja ya alama zinazotutambulisha!

Maendeleo ya kimagharibi na kujifanya ujuaji ndio kunakoleta hoja chochezi dhidi ya asili yetu. Ni mtu asiyejitambua pekee ndiye mwenge uwezo wa kukana hata asili yake!

Ni aibu kwa Mtanzania yeyote kuuona mwenge kama chukizo badala ya kuulinda kama moja ya utambulisho wake kama RAIA!

Ni rai yangu kuangalia namna ya kuboresha mbio za mwenge badala ya kuiondoa kabisa alama hii muhimu kwa Taifa letu!
we mtoto wa juzi unajua siri ya mwenge?
ukiijua siri, utajua pia kwanini % 60 ya watz ni wajinga nawe ukiwemo, ni asilimia 40 tu. wanajitambua kwa mujibu wa takwimu za NEC chini ya Lubuva
 
Hata aliyeuanzisha alikiri kwamba kuna mambo mengine yanapaswa kuachwa.Leo unatumia Bilioni 150 kisa kuutembeza Mwenge ambao hauna sura ya kitaifa wala hauna faida kwetu kama Taifa.Kwanini pesa hizo zisingeenda kununua madawa au kuilipa MSD deni lake la bilioni 100?

Mtu anayeutukuza Mwenge leo lazima awe kati ya wale wanne waliowekwa kwenye jambo leo...........
 
Ukishajitambua utaona faida yake!
 
we mtoto wa juzi unajua siri ya mwenge?
ukiijua siri, utajua pia kwanini % 60 ya watz ni wajinga nawe ukiwemo, ni asilimia 40 tu. wanajitambua kwa mujibu wa takwimu za NEC chini ya Lubuva
Yaani kama wewe unajitambua na unaandika hivi ni bora nibaki na ujinga wangu kuliko kuwa na "werevu wako"
 
Namuunga mkono mleta mada , wengi tumekuwa tukihoji gharama zinazotumika lakini tumekuwa hatuoni ujumbe wa amani , mshikamano na umoja unaopatikana ndani ya ukimbizwaji mwenge huo.. lengo hasa la kuwapo kwa mwenge ni uhamasishaji wa kulinda amani na kueneza upendo miongoni mwa zaidi ya makabila 120 kote nchini kwa kuwaleta pamoja kwa lengo la kudumisha na kuendeleza amani na mshikamano ni moja ya shughuli za mwenge ,, ikumbukwe amani ina gharama yake bila ya amani hakuna maendeleo yoyote yatakayopatikana .. kinachohitajika kuangaliwa ni kupanga njia bora yenye gharama ndogo na sio kuufuta au kuuweka mahali , kupanga ni kuchagua
 
Back
Top Bottom