Mbadala wa DSTV

Mbadala wa DSTV

Nyetk

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
1,648
Reaction score
1,701
Heshima kwenu wakuu.
Mimi ni mteja wa miaka mingi wa DSTV, huduma za MultiChoice Africa na kwa kweli napenda sana chaneli zao nyingi. Kama ilivyo kwa watanzania wengi mimi ni mpenzi mkubwa wa mpira na michezo kwa ujumla na bila shaka tunajua kwamba kampuni hii imejiuza zaidi kupitia chaneli zake murua za Super Sports.

Hivi sasa nimechoshwa mno na ukiritimba wa kampuni hii unaotokana na wao kuwa ndio wauzaji pekee (wanaojulikana huku) wa chaneli kipenzi cha wengi. Nakerwa sana ninapokuwa nimelipia mwaka mzima halafu wananikatia matangazo wakati wowote wanapojisikia eti salio lako limekwisha hata kama bado miezi sita. Ni kweli ukienda kulalamika watakuongezea kwenye akaunti yako zile siku walizokata, lakini hiyo hairejeshi adha unayoipata na watumiaji wenzako (wageni, wateja, nk) mathalani kama kulikuwa na tukio live muhimu kulifuatilia likipita limepita na hicho ndicho kinakera. Wakati mwingine unaleta fundi abani kama shida ipo kwenye network yako na unalazimika kumlipa.

Ni nafuu "monopoly" hii katika bidhaa hizi ingeondoka manaa Tanzania inakuwa motoni sasa; kila mahali tumebanwa na "monopoly zisizo na tija – kwenye siasa kero, kwenye uchumi kero, hata kwenye burudani pia? Wanabodi anayejua kampuni mbadala wa DSTV anijuze niwapige chini hawa haki ya nani!
 
pole mkuu,,
ila binafsi sioni tatizo lolote la dstv ukiondoa pale hali ya hewa inapokuwa mbaya,,ila kama una uwezo mzuri kiuchumi dstv is all you need,,pia kuhusu kukatiwa huduma,suluhisho lake inatakiwa uwe na namba ya huduma kwa wateja multchoice dsm,hawa watu huhudumia vizuri,hakikisha kabla hujapiga una no za kadi yako,,but dstv is the best!!!
 
kaka wavumilie hawa jamaa wapo vizuri angalau, ukijiunga na startimes, sijui na ving'amuzi gani utacheka mwenyewe! channel nne, mala igande, mala no signal,ni zaidi ya ubabaishaji
 
Huku ulipo wewe ndo pazuri kuliko kwingineko. Kwa sasa sijui mbadala mwenye huduma bora kuliko hao DSTV
 
pole mkuu,,
ila binafsi sioni tatizo lolote la dstv ukiondoa pale hali ya hewa inapokuwa mbaya,,ila kama una uwezo mzuri kiuchumi dstv is all you need,,pia kuhusu kukatiwa huduma,suluhisho lake inatakiwa uwe na namba ya huduma kwa wateja multchoice dsm,hawa watu huhudumia vizuri,hakikisha kabla hujapiga una no za kadi yako,,but dstv is the best!!!
You speak well mkuu, DSTV are the best. Namba za customer care ninazo. Kabla ya kusitisha matanganzo huwa wanatuma SMS kukukumbusha ulipe kabla ya kukatiwa. Nilipopokea notifications hizo niliwapigia na kuwaeleza kuwa there is something wrong with their system maana mi nimelipia mwaka mzima. Tukacompromize kwamba there was a mistake on their side na wakaahidi hawatanikatia. Cha kushangaza bado walikata! Kufunga safari hadi ofisi za DSTV na foleni za Dar ni kero nyingine. Unafika wanakwambia afu wamebana pua "Oh, labda kalete decoder hapa!" Huo muda natoa wapi?
 
Mkuu ulipo ndo mbinguni, kwingine ahera...! So tulia ule raha, hali ya hewa inapokuwa mbaya ni kawaida satellite kuzingua zingua. hata nege huwa hazipai wala kutua kama hali ya hewa ni mbaya kiongozi.

Kuhusu kukata, sina experience hiyo kwa sababu hata mimi nalipia kwa mwaka mzima ila sijawahi pata hilo tatizo. Nakushauri uwe na namba zao, ikikata wapigie immediately ili usikose uhondo especially sasa ambavyo BBA inaanza na watanzania tumemtoa sadaka binti yetu Feza.
 
Popote kwenye monopoly tarajia ukiritimba, uonevu na kunyonywa!
 
Mkuu ulipo ndo mbinguni, kwingine ahera...! So tulia ule raha, hali ya hewa inapokuwa mbaya ni kawaida satellite kuzingua zingua. hata nege huwa hazipai wala kutua kama hali ya hewa ni mbaya kiongozi.

Kuhusu kukata, sina experience hiyo kwa sababu hata mimi nalipia kwa mwaka mzima ila sijawahi pata hilo tatizo. Nakushauri uwe na namba zao, ikikata wapigie immediately ili usikose uhondo especially sasa ambavyo BBA inaanza na watanzania tumemtoa sadaka binti yetu Feza.

Mkuu Brooklyn labda hukunisoma hapa

You speak well mkuu, DSTV are the best. Namba za customer care ninazo. Kabla ya kusitisha matanganzo huwa wanatuma SMS kukukumbusha ulipe kabla ya kukatiwa. Nilipopokea notifications hizo niliwapigia na kuwaeleza kuwa there is something wrong with their system maana mi nimelipia mwaka mzima. Tukacompromize kwamba there was a mistake on their side na wakaahidi hawatanikatia. Cha kushangaza bado walikata! Kufunga safari hadi ofisi za DSTV na foleni za Dar ni kero nyingine. Unafika wanakwambia afu wamebana pua "Oh, labda kalete decoder hapa!" Huo muda natoa wapi?

In addition ni miaka 13 sasa tangu niwe mteja wa DSTV. So I'm talking of a shoe I know!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kwa usumbufu; japo Dstv haina mbadala ukanda huu wa dunia! tatizo la monopolies the world over ndilo hilo!! it gets to their heads kwamba hapo ni "Mtakuja" huna pa kwenda!!

So visit them in person; give them a piece of your mind in the strictest words you can possibly conjure-up! kwamba wamelewa sifa na ukiritimba which is siucidal on their part; and you are disapointed; then uwape ultimutum ya kuwamwaga! good luck
 
Your sympathy well appreciated. I did almost the same last year but the cycle of probs goes on again! May be it's part of what we (Tzns) haave'n created for.
 
Mie ni mtumiaji wa huduma ya DSTV na sijawahi kukutana na hilo tatizo hata mala moja ndio kwanza nasikia kwako mkuu, tatizo ambalo wanalo DSTV ni kipindi cha mvua huwa inasumbua wakilekebisha hilo DSTV is the best among the Best hana mpinzani TZ.
 
Back
Top Bottom