Mbabe SATANA alikufa au bado yu hai?

Mbabe SATANA alikufa au bado yu hai?

Kwa wanaokumbuka miaka ya 80 kulikua na bwana akiitwa Santana. Huyu jamaa alikua mbabe sana akicheza karate. Kutwa nzima akishinda stendi za mabasi sanasana kituo cha manzese (msufini). Akiamua aliweza kupora chochote pasipo kufanywa chochote. Kuna wakati alisaidia wanafunzi kuingia kwenye mabasi makonda wakimuogopa kwelikweli. Ni zaidi ya miaka 25 sijamsikia tena
Kama kipindi hicho alikuwa na miaka ishirini na tano, hadi leo ni kwamba atakuwa na miaka hamsini, nahisi upara utakuwa umeenea kichwa kizima huku nywele zake za kwapani zikiwa zimejaa mvi.
Ubabe kwishney
 
Kwa wanaokumbuka miaka ya 80 kulikua na bwana akiitwa Santana. Huyu jamaa alikua mbabe sana akicheza karate. Kutwa nzima akishinda stendi za mabasi sanasana kituo cha manzese (msufini). Akiamua aliweza kupora chochote pasipo kufanywa chochote. Kuna wakati alisaidia wanafunzi kuingia kwenye mabasi makonda wakimuogopa kwelikweli. Ni zaidi ya miaka 25 sijamsikia tena

Alikuwepo na Cool 9 pia, huyu alikuwa noma sana, miaka ya tisini hiyo, walikuwepo watu wanajiita KIBOKO MSHELI nao walikuwa wanatisha sana, sasa hivi yupo jamaa anaitwa IDDI BONGE huyu ndo kanjanja wa watoto wa kihuni wote wanao fanya shughuli zao za kihuni kuanzia Ubungu, Magomeni yote, Manzese, Kinondoni, Ilala na Mburahati. Jamaa ni kwere!
 
mkuu game zipo nyingi weka wazi unamanisha ipi...tehe tehe teheeee

Mie sio mliberari mkuu nilikuwa namaanisha Karatee nina black belt sasa hivi nilikuwa nataka kumwonyesha kazi huyo jamaa
 
Mbabe toka manzese hyo ila aliyakanyaga kwa wachina
Alafu kulikuwa na mbabe mmoja anaitwa wandiba
Kulikuwa na mbabe mmja anaitwa juma ndedere
Kulikuwa na mbabe mmoja alikuwepo pia enzi hzo anaitwa stiba Dah Umenikumbusha longtime watu Hawa

Ova
Leo jioni nataka nikapige misele Manzese saa 2 hivi
 
Huyo Santana wako ni feki.
Nikifikiri unaongea Carlos Santana- the Great.
Ni wa siku nyingi sana na rekodi yake moja itakayokuacha hoi ni- Black Magic Woman

Mim mwenyewe nikajua ni huyo mkali wa Samba patie kumbe wa kichina china
 
swala 5 na guest house wapi na wapi
mkuu naona kama unachanganya madawa
 
ukweli ni kwamba watu wa zamani walikuwa Waoga halafu wote mnajuana. nakumbuka zamani askari mmoja anaweza kamata maskani mzima akawafunga mashati na akawaswaga hadi kituoni maana ana wajua hadi wazazi wenu. sasa leo hili linawezekana? nasema kama kijana wa zamani mzee wa sasa
 
vijana wa siku hizi(millennials), wanashinda gym kufanya mazoezi ili wawe na vifua vipana vya kuvutia wasichana kimapenzi.

enzi zetu vifua vipana vilikuwa vinaendana na utemi, ubabe sambamba na kuwa mtu wa msimamo thabiti.
Ah wa babe wakina Paul siza
Hyo kdg niyakanyage naye hapo langata enzi hzo maana wengine tulikuwa tnaonekana mabaharia
Siza aanatamani cheni nkaona ohooo
Sema aliishiaa kuwa mkabaji
Badaye akaingia kwenye ujambazi akayanyaga sehemu raia waakammaliza
Siza alikuwa bondia mzuri heavyweight
Alikuwa anakosa mapambano

Ova
 
Akina Dame
Ayubu mpuz tu miguvu yote ile Unga umemmaliza ila naye aliyakanyaga kwa mshikaji mmja anaitwa Razak alichezea
Ila ukoo wao wote Wana miguvu wale
Nature
Mzee wao alikuwa anaisimamia msikiti wa sinza pale mahali fulani kna siku ilitokea ngumi ikabidi mzee amuite damme ayubu kuwapa tag ilikuwa shida
Unga tu umemaliza jamaa

Ova
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom