Mazuri na Mabaya ya Serikali ya Awamu ya Nne!

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Naamini kabisa hakuna serikali isyo kosa mazuri yake na mabaya yake japo uwiano kati ya mazuri na mabaya ndiyo hutofautiana. Vivyo hivyo naamini serikali ya awamu ya nne haikosi mazuri yake na mabaya yake. Ningependa tupambanue na tuchambue ni yapi mafanikio ya serikali ya awamu ya nne na ni yapi imeshindwa. Binafsi nitaanza mimi kuonyesha yapi naona ni mafanikio na yapi siyo. Haimaanishi najiona nipo sahihi asilimia mia kwa mia na nipo tayari kusahihishwa.

Mafanikio:

1.Kuinua msisimko wa watu: Hakuna serikali iliyopita ambayo iliweza kuinua hisia kubwa za wananchi iwe kwa mazuri au kwa mabaya. Huwezi kuwa neutral na serikali ya JK. Ni aidha unaipenda sana au unaichukia sana. Kwa kiasi kikubwa awamu hii imeamsha wananchi washiriki zaidi au kufuatilia zaidi siasa za nchi yao. Hatukuona hii kwenye awamu zilizo pita.

2. Uwazi (transparency): Katika awamu zote hii ndiyo awamu ambayo mambo ya serikali yanaonekana na kujadiliwa wazi wazi. Najua wengi watasema ni upinzani ila pia tukumbuke pia kuwa hata awamu ya Mkapa kulikua na upinzani. Pia kumekuwa na uhuru zaidi wa vyombo vya habari na havibanwi kama awamu zilizo pita.

3. Dipolomasia:
Katika diplomasia tumefanikiwa na hii inawezekana ni kutokana na historia ya JK kuwa waziri wa mambo ya nje. Hapa siongelei safari za nje! Tanzania ilipewa heshima ya kuwa mwenyekiti wa AU, raisi alichaguliwa kuwa mmoja wa wasuluhishi wa Ivory Coast na pia tuliweza kuikomboa Comoro.

Wapi wameshindwa:
1. Rushwa: Rushwa bado ni tatizo kubwa na mpaka sasa kuna watu wamekua "untouchables". Ndiyo kuna walio kamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma mbali mbali kama wakina Basil Mramba, Daniel Yona, Mgonja nk lakini mpaka sasa ni dagaa tu wanaokamatwa na kutuhumiwa huku mapapa wakiwa bado hawashikiki.

2. Umoja: Nadhani kwa kiasi kikubwa amawu hii imeshindwa kuleta umoja. Kuanzia kwa wananchi kwa kujaribu kuhubiri udini kwa manufaa ya kisiasa mpaka mipasuko ndani ya chama chenywe ambapo kuna makundi mbali mbali. Nilikua namuona JK kama raisi atakae kuwa "The Great Unifier" ila amekua the great divider.

3. Uchumi: Labda mambo yailiyo nje ya uwezo wa serikali yamechangia ila kusema ukweli serikali imeshindwa kutekeleza ilani yake ya uchumi. Sasa hivi kila kitu kimepanda bei toka awamu ya kwanza na baadhi ya vitu muhimu vimeanza kuadimika kama umeme na mafuta nk.

4. Umeme: Mh mgao wa sasa haujawahi kuonekana Tanzania. Japo serikali ilijua tokea 2006 kuwa kima cha maji kinashuka na kitaendelea kushuka bado hakuna njia mbadala zilizo tafutwa kupunguza adha ya ukosefu wa umeme. Hakuna nchi inayoweza endelea bila nishati ya umeme. Biashara zina athirika, viwanda vina athirika na mwisho wa siku UCHUMI una athirika.

Nipo tayari kusahihishwa. Yote ni katika kujifunza zaidi kuhusu serikali yetu ya sasa.
 
Ni kweli kila serikali haikosi mazuri na mabaya yake. Zingine mazuri yanazidi mabaya na zingine mabaya yanazidi mazuri. Ila mkuu haujatueleza kiujumla je unaona serikali ya awamu ya nne imefanikiwa? Kwa maana mazuri yamezidi mabaya au mabaya ndiyo yamezidi mazuri?
 
Mkuu kabla ya kusema mazuri yamezidi mabaya au la ni lazima kwanza tuchambue yapi tunaona mazuri na yapi tunaona mabaya. Hayo niliyo ainisha ni ya kuanzia mada tu na nipo tayari kusahihishwa kwa lolote. Kwa kuangalia michango ya wana JF ndiyo tuta ona yapi yamezidi yapi.
 
Mwanafalsafa1,

..unajua hayo yote uliyoyataja[mazuri / mabaya] naona kama hayana uzito mkubwa sana kwa shangazi yangu aliyeko kijijini.
 
Maisha bora kwa kila Mtanzania yako wapi jamani? Yaani sijaisikia tena hii kauli mbiu. Mara ya mwisho nyinyi wenzangu kuisikia ilikuwa lini?
 
Je yapi unaona yana uzito mkubwa mkuu? Kama unavyojua watu tunatofautiana. Sisi wengine inawezekana shangazi zetu wote wapo mjini. Ndiyo maana yana hitajika maoni yako mkuu.
 
Maisha bora kwa kila Mtanzania yako wapi jamani? Yaani sijaisikia tena hii kauli mbiu. Mara ya mwisho nyinyi wenzangu kuisikia ilikuwa lini?

Mara ya mwisho kuisikia hii kauli ni 2006. Sidhani kama hii kauli ilitumika uchaguzi wa 2010.
 
Naamini kabisa hakuna serikali isyo kosa mazuri yake na mabaya yake japo uwiano kati ya mazuri na mabaya ndiyo hutofautiana. Vivyo hivyo naamini serikali ya awamu ya nne haikosi mazuri yake na mabaya yake. Ningependa tupambanue na tuchambue ni yapi mafanikio ya serikali ya awamu ya nne na ni yapi imeshindwa. Binafsi nitaanza mimi kuonyesha yapi naona ni mafanikio na yapi siyo. Haimaanishi najiona nipo sahihi asilimia mia kwa mia na nipo tayari kusahihishwa.

Mafanikio:

1.Kuinua msisimko wa watu: Hakuna serikali iliyopita ambayo iliweza kuinua hisia kubwa za wananchi iwe kwa mazuri au kwa mabaya. Huwezi kuwa neutral na serikali ya JK. Ni aidha unaipenda sana au unaichukia sana. Kwa kiasi kikubwa awamu hii imeamsha wananchi washiriki zaidi au kufuatilia zaidi siasa za nchi yao. Hatukuona hii kwenye awamu zilizo pita.

2. Uwazi (transparency): Katika awamu zote hii ndiyo awamu ambayo mambo ya serikali yanaonekana na kujadiliwa wazi wazi. Najua wengi watasema ni upinzani ila pia tukumbuke pia kuwa hata awamu ya Mkapa kulikua na upinzani. Pia kumekuwa na uhuru zaidi wa vyombo vya habari na havibanwi kama awamu zilizo pita.

3. Dipolomasia:
Katika diplomasia tumefanikiwa na hii inawezekana ni kutokana na historia ya JK kuwa waziri wa mambo ya nje. Hapa siongelei safari za nje! Tanzania ilipewa heshima ya kuwa mwenyekiti wa AU, raisi alichaguliwa kuwa mmoja wa wasuluhishi wa Ivory Coast na pia tuliweza kuikomboa Comoro.

Wapi wameshindwa:
1. Rushwa: Rushwa bado ni tatizo kubwa na mpaka sasa kuna watu wamekua "untouchables". Ndiyo kuna walio kamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma mbali mbali kama wakina Basil Mramba, Daniel Yona, Mgonja nk lakini mpaka sasa ni dagaa tu wanaokamatwa na kutuhumiwa huku mapapa wakiwa bado hawashikiki.

2. Umoja: Nadhani kwa kiasi kikubwa amawu hii imeshindwa kuleta umoja. Kuanzia kwa wananchi kwa kujaribu kuhubiri udini kwa manufaa ya kisiasa mpaka mipasuko ndani ya chama chenywe ambapo kuna makundi mbali mbali. Nilikua namuona JK kama raisi atakae kuwa "The Great Unifier" ila amekua the great divider.

3. Uchumi: Labda mambo yailiyo nje ya uwezo wa serikali yamechangia ila kusema ukweli serikali imeshindwa kutekeleza ilani yake ya uchumi. Sasa hivi kila kitu kimepanda bei toka awamu ya kwanza na baadhi ya vitu muhimu vimeanza kuadimika kama umeme na mafuta nk.

4. Umeme: Mh mgao wa sasa haujawahi kuonekana Tanzania. Japo serikali ilijua tokea 2006 kuwa kima cha maji kinashuka na kitaendelea kushuka bado hakuna njia mbadala zilizo tafutwa kupunguza adha ya ukosefu wa umeme. Hakuna nchi inayoweza endelea bila nishati ya umeme. Biashara zina athirika, viwanda vina athirika na mwisho wa siku UCHUMI una athirika.

Nipo tayari kusahihishwa. Yote ni katika kujifunza zaidi kuhusu serikali yetu ya sasa.

Wee msumbufu sasa, jamaa ameona mazuri matatu na mabaya manne sasa aongeze nini????????
 
hapo kwenye mabaya yako hilo la nne ndio kubwa zaidi linasababisha kiasi cha kila kitu kuwa na mtafaruku.

na habari za leo humu ni ile ya mizengo anataka kupandisha bei ya umeme wakati hata kuwaka kwenyewe tabu mgao kila kukicha..

sululisho mi naona hawa jamaa (serikali) wakomae zaidi kwenye kutafuta njia mbadala ya chanzo cha umeme kuliko kutegemea maji tu na gesi ya kusadikika.
 
Back
Top Bottom