Mazungumzo Usingizini

Mazungumzo Usingizini

Waterlemon

Senior Member
Joined
Sep 2, 2016
Posts
143
Reaction score
199
Wenye kuzungumza usingizini huwa kawaida hawasemi yenye kueleweka. Lakini wakati mwengine wanaweza wakasema mambo ambavyo yanachekesha sana.

Kipindi namtembelea binamu yangu huko kona za jijini alipokuwa akiishi na mkewe na mwana wao wa kiume. Siku moja mida ya jioni baada ya yeye kurejea toka kazini pamoja na mkewe tukakaa sebuleni baada ya mlo jioni kwa maongezi madogo madogo na kupumzika huku tukiangalia tv.

Shemeji akapitiwa na usingizi kwenye sofa, basi sie tukapunguza sauti ya tv na tukawa tunazungumza kwa sauti ya chini chini hivi ili tusimwamshe.

Basi baada ya kipindi, shemeji wakati bado macho bado kayafumba akiwa usingizini, aliinuka ghafla na kusema "ninja wanajitahada sana" huku akipiga makofi ya kushangilia.

Mie na binamu yangu tukaangaliana. Akanipa ishara nikae kimya kwa kuweka kidole mdomoni, ki masihara hivi akitabasamu (Nahisi alikuwa akimjulia mkewe kama hii ni desturi yake kuongea akiwa amelala) ... kisha akaanza kumzungumzisha zaidi...

Binamu: Wanajitihada za namna gani hizo baby?

Shemeji: Mitihani wanayoifanya migumu

Binamu: mitihani gani hiyo wanaifanya hao ninja darling?

Shemeji: Wanajifunza kunyoa kondoo lakini chura sio solution.

Binamu: Sasa honey, nini unahisi wewe wafanye?

Shemeji: I don't care if the sheep is in bed, lazima tumvalishe gauni jipya

Basi mie huku nagaragara kwa kicheko lakini najiziba mdomo nisicheke kwa sauti...

Binamu (huku akinisisitiza nisitoe sauti kwa kidole mdomoni): sasa gauni mpya tutaitoa wapi boo, sie tuna baby boy..

Shemeji: itabidi tuwaozeshe

Binamu akaona hapo sasa hatari... mwanae kuozeshwa na kondoo. Akainuka kumuamsha shemeji na kumsisitiza aende zake akapumzike chumbani...

Shemeji taratibu akaelekea chumbani macho akiyafinyanga finyanga hivi. Sie huku nyuma si vichecko hivyo.

Siku ya pili shemeji hakumbuki hata moja. Binamu ananiambia ndio tabia yake anapenda kumsemesha akiwa usingizini maana vituko vitupu..

Je kuna yeyote ambaye ashawahi kumsikia mtu akiongea usingizini. Kama ni ya kufurahisha basi iweke hapa tucheke...
 
Hahahahaha...mimi kuna jamaa chuo alikuwa Akiangalia muvi ya kikorea baadae anairudia tena yote kama ilivyo.

Ukimsikiliza unaelewa muvi nzima bila hata kuiangalia.

Utaskia aigooooo..pehaaaa.....ugumjiii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
We jamaa acha kutufunga kamba
 
Sio kamba mzee.....jumong na land of wind ndiye aliyeni inspire usingizini kuziangalia
 
Hahahahaha...mimi kuna jamaa chuo alikuwa Akiangalia muvi ya kikorea baadae anairudia tena yote kama ilivyo.

Ukimsikiliza unaelewa muvi nzima bila hata kuiangalia.

Utaskia aigooooo..pehaaaa.....ugumjiii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
duh!!!
 
ngoja siku aanze hivi
''fredy jana ulisahau pochi pale gesti...''
sijui mumewe ataendeleza vp hayo mazungumzo
 
Hahahahaaa...umenichekesha sana

Yaani inafurahisha mno. Binamu alinisimulia vituko vingi tu vya kuongea kwa shemeji usingingizi.

Alinipa hii moja wapo:

kuna siku usiku wa manane wakati aliinuka kwenda msalani, aliporudi kuingia kitandani shemeji akajigeuza akiwa usingizini akianza kumwita kwa jina huku akisema..

"... bandika birika la chai jikoni, njiwa wamesha amka"
 
Inategemea na mtu nakumbuka mke wangu siku moja nilimpiga na alitambua kosa lake ilikua mchana mm nikaondoka nikarudi usiku nikala na kulala tulipo lala yeye usingizi ukampitia mapema kabla yangu mm huku tukiwa wote kitandani ghafla nikasikia anaongea huku akijutia kosa alilo lifanya na kuonesha kua ananipenda huku akionesha kua atabadiloka ili tuishi kwa amani wakati huo mm nilikua nawaza kumtimua hivyo nikaghairi na ndipo nikagundua kua huyu huwa anaongea mpaka sasa kikitokea kitu kwake mchana ambacho si cha kawaida usiku huwa anaongea na ukimuiliaza huwa anabisha
 
Hahahahaha...mimi kuna jamaa chuo alikuwa Akiangalia muvi ya kikorea baadae anairudia tena yote kama ilivyo.

Ukimsikiliza unaelewa muvi nzima bila hata kuiangalia.

Utaskia aigooooo..pehaaaa.....ugumjiii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ha ha ha. Ha et aigoo peaaaa
 
Kweli hawa watu wapo nina mdogo wangu mkubwa tu anaongeaga huyo
Na watu wa hivyo wakiongea wanakua serious mno na macho wanatoa haswa
 
Kuna riwaya moja nilisoma kwenye jarida la sani. Mume alikuja kujua kuwa mkewe anamchit na shamba boy kutokana na mke kuwa na tabia ya kuongea usingizini..
 
ni ugonjwa unaitwa somniloguy ingawa hauna madhara lakini mtu akiwa nao unakera wengine, hasa wakati wa usiku wakati wengine wamelala. Kwa baadae wagonjwa wengi wa somniloguy wanaweza kupatwa na ugonjwa wa mshangao, na upweke (feeling loneliness) ambao unaweza kupelekea mtu kujinyonga.
 
Nawafahamu watu wawili, mmoja alikuwa mchumba wangu by then (ila hatukuitimiza ahadi, story tofauti hiyo), nilikuwa naishi nae, kuna wakati nilimpa likizo kwenda kwao Arusha kusalimia, aliporudi siku ya pili yake usingizini, akawa anaongea (na hii siyo kuota mjue), nasikia pia hutakiwi kumshtua ila unamlinda tu asitoke nje akasababisha madhara, sasa ongea yake ilinishtua, ni alikuwa akimtaja kidume mwenzangu kwa jina kabisa,, tena kwa sauti ile ya mahaba, huku akinyongeka kiana. Kulipokucha sikumuuliza maana niliwahi kazini, kurudi namuuliza alimkana jamaa katakata, nikaona isiwe ishu.

Siku nyengine, hakuwa amelala bali tukiwa 6x6 katikati pale, akalitaja jina lilelile, tena kwa mahaba ya nguvu - alikuwa akimaliza, mimi kumalizia japo kwa kujilazimisha, nikamuuliza, alipokana ni makofi juu yalifuata. Maana naitwa kwa jina la mwengine, wanaume wengi hatupendi hivyo. Nilikuja kugundua ni jamaa yake aliyemuingiza ukubwani, na hata akirudi kwao wanatafutana. Daah ukubwa huu tunayaona mengi.

Mwengine ni mdogo wangu wa mwisho kuzaliwa wa kiume, yeye hata alale mchana, ataongea tu.

Ahsante!
 
Duh! pole mkuu. Hii si ya kucheka maana nikicheka nitakuwa nacheka your struggle. Binti na vibao juu
 
Kwa hiyo huyo binti hamuwasiliani tena jamani? Nasikia uchungu mie
 
Back
Top Bottom