Jeshi la polisi ni jeshi la wanananchi wote.Kama mazoezi wanayofanya kwa bidii yote ili tu kukabiliana na waandamaji kwa nguvu kubwa basi litakosa sifa ya kuwa jeshi la umma,bali ni jeshi la kikundi fulani cha upinzani.Jeshi la polisi wanachotakiwa ni kulinda tu waandamanaji kwa usalama bila kuongozwa na mihemko ya kisiasa.Itakuwa ni aibu kubwa kufanya mazoezi ya nguvu kwa ajili ya UKUTA wa septemba mosi halafu maandamano yakawa hayapo.Hizi nguvu pale si pa kuzitumia,wakazitumie mahali pake.Jeshi ni la wote.
Umesema nguvu kubwa isitumike kuadabisha waandamanaji! Kutuliza ghasia ni kutumia nguvu kubwa? TPDF jeshi la ulinzi wa umma,ndiyo "nguvu kubwa", umeona limehusishwa pale? Intelijensia yako imekueleza dhamira ya maandamano siku hiyo,ukiacha blahblah za demokrasia, intelijensia yako imeshushua nyuma ya pazia kuna nini? Maandamano yatakuwa na ukubwa gani? Je maandamano yatakuwa ni ya amani100%? Vibaka na majizi,intelijensia yako imekuaminisha kuwa siku hiyo watageuka na kumpokea bwana awe mwokozi wa maisha yao?
Serikali siyo "njinga" kuchukua tahadhari kwa "inshu" kama hiyo. Mazoezi yanayofanyika ni kuonesha uhalisia wa namna watakapokabiliana na hali halisi itakapotokea.
Ulitaka wajiandae kwa mazoezi ya kugawa pipi siku hiyo pendwa?
Tena mazoezi menyewe nimeyaona. Ngao na virungu vya plastiki visivyovunjika,hata vipigeje,mabomu ya machozi na maji washa. Burudani tupu wanayo isubiri watu sikuhiyo. Mtu unapigwa mwili unachangamka ad unafurahi,mambo ya mwanaume hayo. Maji ya upupu,starehe tupu,maana kuwashwa ndiyo burudani yenyewe! Haujasikia mtu anaugua mapele hadi ananuka,kuyatibisha hataki sababu yanamstarehesha kuyakuna! Starehe tupu nakuambia!
Chakula cha umma ulikila mwisho shule za bweni,lkn sasa utalishwa bure na serikali ukiwa mahabusu,acha kushiba tu,hadi unanenepa,kuna shida gani? Viongozi wa Ukuta wamegawana maeneo siyo kwaajili ya kuandamana,hapana. Waandamanaji niwewe. Wao ni kukaa na kusubiri kupokea maandamano na kutoa tuzo kwa wataokuwa washindi wa kwanza kumaliza "ruti" ya maandamano waliyopangiwa kama ifanyikavyo kwenye riadha.
Kakini "kukutoa" ama kuongezewa damu utatafuta ndugu zako, maana kwenda jela mtu hatalazimishwa,ni suala la hiyari,wala hutasikia kiongozi anakuja kukulazimisha kwenda kuandamana na hiyo michubuko uliyoipata wala siyo siyo sana,ni suala la kutafuta burudani,wala haujavunjika,ni lako mwenyewe!
Akili za kuambiwa? Changanya na zako!