The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,151
- 20,076
Nadhani kuna kitu huelewi.Unawajua Irish Republican Army (IRA)?Sicarii,Tamil tigers je?,kazi ilokuwa inafanywa na Knight templars unaifahamu,the list is long.ugaidi upo na umekuwepo kabla ya mtume kuja,wapo magaidi wakristo (IRA),wapo wahindu (tamil tigers),wapo waislamu (alshabaab,ISIS etc).
Najaribu tu kukufamisha kuwa ugaidi hauko specific kwa dini fulani,bali ni utashi tu wa kundi la watu lenye dhamira ovu.
Kama umesoma historia basi utakuwa unafahamu kuhusu vita vya msalaba a.k.a the crusade na ile Spanish inquisition unyama wote huu ulifanywa na wakristo,joseph kony na kundi lake la Lord Resistance Army wameshafanya matendo kibao ya kigaidi,kwa mwamvuli wa dini ya kikristo lakini husikii waislamu tukiwatuhumu ama kuwaita wakristo magaidi.Ni wasiokuwa na elimu na kujua historia pekee wanaoweza kunyooshea kidole waislamu kuwaita magaidi.
Ukisema IRA ni magaidi ya kikiriato basi hata FARC, kina Savimbi nk wote ni magaidi ya kikiristo.
Mtu anakua gaidi wa dini kama anapigania hiyo dini,anapigania maslahi ya hiyo dini.
Sasa naomba uniambie je IRA walikua wanapigania maslahi ya ukiristo,yaani kusimamisha dola ya kikiristo huko Ireland? Inawezekana kabisa kikundi cha magaidi wote ni wa dini flani, Mfano IRA wote ni wakristo, je walikua wakipigania maslahi ya ukiristo?
Vikundi vingine vyote vya kiislam vinahusishwa na ugaidi wa dini kwa maana kwamba vinapigania maslahi ya kidini sio ya kisiasa,vinapigana kulinda imani yao.