Bwana mkubwa, maziwa ya soya ni bora kuliko hata ya ng'ombe, si unajua soya ni moja kwa moja mmea, unachukua chakula na madini moja kwa moja toka kwenye udongo, na sisi wanadamu tumeumbwa kutokana na udongo hivyo kitu kinachotoka mojakwamoja udongoni kinatufaa zaidi kuliko kile kinachotoka kwenye nyama. maziwa ya ng'ombe si mazuri, kwanza kwasababu ng'ombe wanalishwa madawa mengi sana kila siku ili watoe maziwa mengi ambayo ni artificial wala si natural (naongelea ng'ombe wa kisasa), pili kwa ng'ombe wote, damu yao inaweza kuwa na vijidudu ambavyo si rahisi kufa wakati mwingine, maziwa ya ng'ombe yanabeba matatizo ya yule ng'ombe waliyemkamua pamoja na chakula alichokuwa analishwa, ni sawa na makuku ya kisasa, the same applies kwenye maziwa ya ng'ombe hawa wa indoors (hao wa masai na wasukuma hawasambazi maziwa mijini). watu wengi wanapata kansa kwasababu ya vitu artificial kama hivyo. nchi za wenzetu, maziwa ya soya ndo ya garama kuliko hata haya ya kawaida, hapa bongo sidhani kama yanapatikana labda kwa hao wasabato na watu wa sido. SOYA ni mmea safi sana, unarutubisha sana mwili, una madawa mengi na una virutubisho vingi sana. inashauriwa na kwa wanandoa kula soya, kuweka kwenye uji wa lishe, kutengeneza maziwa ya soya etc. I hope nimejibu swali lako. na wengine watatoa michango yao bila shaka.