Maziwa ya soya na ya ng'ombe yapi bora?

Mwana wa Mungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2008
1,003
83
WAKUU, kwenu ninyi madaktari na wasomi wengine, hivi maziwa ya ng'ombe na ya soya, yapi yana virutubisho vingi zaidi, tangu nianze kunywa maziwa ya soya, yale ya ng'ombe naona kama siyapendi vile...na afya yangu naona safi zaidi. wataalam mnasemaje kuhusu hili?

point of correction! namaanisha maziwa ya kunywa watu wazima si ya watoto. au nyie watu wengine huwa hamnywi maziwa?
 
namaanisha maziwa ya kunywa mtu mzima, si maziwa ya kunywa watoto. mimi ninywe breast milk, vipi mzee?
 
Bwana mkubwa, maziwa ya soya ni bora kuliko hata ya ng'ombe, si unajua soya ni moja kwa moja mmea, unachukua chakula na madini moja kwa moja toka kwenye udongo, na sisi wanadamu tumeumbwa kutokana na udongo hivyo kitu kinachotoka mojakwamoja udongoni kinatufaa zaidi kuliko kile kinachotoka kwenye nyama. maziwa ya ng'ombe si mazuri, kwanza kwasababu ng'ombe wanalishwa madawa mengi sana kila siku ili watoe maziwa mengi ambayo ni artificial wala si natural (naongelea ng'ombe wa kisasa), pili kwa ng'ombe wote, damu yao inaweza kuwa na vijidudu ambavyo si rahisi kufa wakati mwingine, maziwa ya ng'ombe yanabeba matatizo ya yule ng'ombe waliyemkamua pamoja na chakula alichokuwa analishwa, ni sawa na makuku ya kisasa, the same applies kwenye maziwa ya ng'ombe hawa wa indoors (hao wa masai na wasukuma hawasambazi maziwa mijini). watu wengi wanapata kansa kwasababu ya vitu artificial kama hivyo. nchi za wenzetu, maziwa ya soya ndo ya garama kuliko hata haya ya kawaida, hapa bongo sidhani kama yanapatikana labda kwa hao wasabato na watu wa sido. SOYA ni mmea safi sana, unarutubisha sana mwili, una madawa mengi na una virutubisho vingi sana. inashauriwa na kwa wanandoa kula soya, kuweka kwenye uji wa lishe, kutengeneza maziwa ya soya etc. I hope nimejibu swali lako. na wengine watatoa michango yao bila shaka.
 
jinsi ya kutengeneza maziwa ya soya,
1. unaloweka soya ile inayochanganywa kwenye lishe ya watoto na sio maharage ya soya kwa muda wa masaa 12.
2. unatoa maganda (unamenya)
3. unasaga kwenye blender
4. kisha unachuja huku unaongeza maji kwa kutumia chujio la nazi then unatumia la chai
5. unachemsha na kuweka sukari kiduchu.

NOTE: 1 kg ya soya unatakiwa utoe lita 4 za maziwa so 1/2 kg lita 2 na 1/4kg lita 1.
 
wow, kumbe ndo yanapatikana hivyo? mimi hapa ulaya napata kwenye supermarket, euro 3.5 kwa lita moja, wakati ya ng'ombe ni euro 1.5 kwa lita.

ni mazuri sana, yana afya sana kuliko maziwa haya ya kawaida. nafikiri kwenye makuka ya hapo home kama ya imalaseko, shoprite, hasa pale mlimani city utaweza kupata haya. soya ni mmea wa ajabu na una dawa nyingi na virutubisho vingi ndani yake kuliko maziwa ya kawaida. na ni kweli kuwa, kwa wababa walioko kwenye ndoa, maziwa haya ni balaaa, sawa tu na pweza, yanaweza kukuletea afya na uwezo mzuri zaidi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom