Maziwa kwa mtoto

xenon

Senior Member
Nov 17, 2016
130
79
Habari zenu wana jf,naombeni ushauri kwa hili nina mwanangu leo ni siku ya pili tokea azaliwe na mama yake maziwa hayatoki na mtoto muda wote anaishia kulia kwa kuhitaji maziwa na huwa tunamrambisha asali tu ili kumpunguza makali.

Sasa nifanyaje ili mtoto aweze kula or nimpe maziwa yapi kwa mtoto wa siku 3 ili hii hali ipotee????
 
Habari zenu wana jf,naombeni ushauri kwa hili nina mwanangu leo ni siku ya pili tokea azaliwe na mama yake maziwa hayatoki na mtoto muda wote anaishia kulia kwa kuhitaji maziwa na huwa tunamrambisha asali tu ili kumpunguza makali.Sasa nifanyaje ili mtoto aweze kula or nimpe maziwa yapi kwa mtoto wa siku 3 ili hii hali ipotee????
Daah aisee poleni kwa majanga...Mshauri mke wako atafute ushauri kwa madaktari au Wamama wa makamo ambao wameshazaa na wanajua mambo ya uzazi wamsaidie
 
Ni kwamba hayatoki au yanatoka kidogo sana?

Kama yanatoka kidogo jaribu kukazania diet ya mama pamoja na maji kwa wingi..na pia anaweza kununua breast pump Ili maziwa yatoke kwa wingi.

Kama hayatoki kabisa hilo ni tatizo inabidi uende hospitali kubwa afanyiwe vipimo Ili sababu ya tatizo ijulikane maana siku zinavyodhidi kwenda mtoto atazidi kupungua kilo na atadhoofika.
 
Habari zenu wana jf,naombeni ushauri kwa hili nina mwanangu leo ni siku ya pili tokea azaliwe na mama yake maziwa hayatoki na mtoto muda wote anaishia kulia kwa kuhitaji maziwa na huwa tunamrambisha asali tu ili kumpunguza makali.Sasa nifanyaje ili mtoto aweze kula or nimpe maziwa yapi kwa mtoto wa siku 3 ili hii hali ipotee????
Asali hairuhusiwi kwa mtoto chini ya nwaka mmoja. Kwanza sukari yake ipo complex mtoto hawezi i digest kingine kuna uwezekano asali ikawa na vijidudu..kiutaalamu mtoto alipaswa kupewa glucose na si asali.. And i wonder kama huo ushauri mlipewa hospitali..

Kingine mama anatakiwa ajikande chuchu na maziwa yake kwa maji ya uvuguvugu maziwa yatatoka kwani kuchelewa ni jambo la kawaida..
 
Habari zenu wana jf,naombeni ushauri kwa hili nina mwanangu leo ni siku ya pili tokea azaliwe na mama yake maziwa hayatoki na mtoto muda wote anaishia kulia kwa kuhitaji maziwa na huwa tunamrambisha asali tu ili kumpunguza makali.Sasa nifanyaje ili mtoto aweze kula or nimpe maziwa yapi kwa mtoto wa siku 3 ili hii hali ipotee????

Mtoto chini ya mwaka mmoja sio vizuri kupewa asali.... Sembuse huyo mwenye siku kadhaa....!!!
 
lok kanunue formula halafu asali ni hatari kwa mtoto chini ya miaka 5
Matumizi ya formula hufanyika pale tu kwenye critical condition.. Mm naamini huyo mama anamaziwa ya kutosha na akijikanda vizur siku mbili tatu yatanza kutoka... Na kingine nibkutafuta breast pump zinauzwa kati ya 20000-100000
 
Asali ni mbaya kwa mtoto mchanga ndivyo nilivyokaririshwa na wakubwa zangu,acha mara moja...glucose nayo siyi nzuri kwa tumbo la kichanga inamuumiza sana tumbo pia atasumbua, hapo hamna ujanja tafuteni hayo maformula humo madukani mumpe mtoto ila pia kuwa makini tafuta yaliyo mazuri zaidi.
 
Tatizo la wazazi kukosa maziwa linazidi kuku siku hadi siku sijui tatizo hasa ni nini
 
Ni kwamba hayatoki au yanatoka kidogo sana?

Kama yanatoka kidogo jaribu kukazania diet ya mama pamoja na maji kwa wingi..na pia anaweza kununua breast pump Ili maziwa yatoke kwa wingi.

Kama hayatoki kabisa hilo ni tatizo inabidi uende hospitali kubwa afanyiwe vipimo Ili sababu ya tatizo ijulikane maana siku zinavyodhidi kwenda mtoto atazidi kupungua kilo na atadhoofika.
Hayatoki kabisaaa

Sent from my D6603 using JamiiForums mobile app
 
Asali ni mbaya kwa mtoto mchanga ndivyo nilivyokaririshwa na wakubwa zangu,acha mara moja...glucose nayo siyi nzuri kwa tumbo la kichanga inamuumiza sana tumbo pia atasumbua,hapo hamna ujanja tafuteni hayo maformula humo madukani mumpe mtoto ila pia kuwa makini tafuta yaliyo mazuri zaidi
Formula ni last option baada ya glucose..
 
Matumizi ya formula hufanyika pale tu kwenye critical condition.. Mm naamini huyo mama anamaziwa ya kutosha na akijikanda vizur siku mbili tatu yatanza kutoka... Na kingine nibkutafuta breast pump zinauzwa kati ya 20000-100000
sasa hapa mtoto hajala siku mbili si ni critical condition hii mkuu ama unataka hali iweje ndo mtoto apewe formular?
 
Back
Top Bottom