Mazishi ya Mabina-Ijumaa

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
495
250
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mwanza bwana Clement mabina atazikwa Ijumaa huu mazishi ya mtoto aliyepigwa risasi na mabina akizikwa leo, bwana mabina maarufu kama "Wembe" aliuawa na wananchi wenye hasira kali kufuatia hisia za dhuruma na ubabe zilizokuwa zinataka kufanywa na mabina dhidi ya wananchi hao.

Ikumbukwe kuwa, kesi ilikuwa mahakamani na imechukua miaka 15 hadi sasa hata haijaisha na kuna tetesi kuwa aliiweka mahakama mfukoni, wakazi wengi wa mwanza wanajiuliza inakuwaje kesi kama hiyo ichukue miaka 15 miaka ya mtu mzima? tatizo ni nini? ushahidi? mlima si upo?

Mabina anaelezwa kuwa alikuwa jambazi sugu na mbabe sana kabla ya kujificha ndani ya mwavuli wa chama, alipewa jina la "wembe" likiwa na maana kwamba mtu wowote anaweza kukukata.

Mabina ana mashamba mengi sana ya mpunga MAGU, na ana mashamba kule Lamadi, na anaaminika kuwa na vitalu vya madini hapa nchini.

Mlima uliosababisha mauti yake ulikuwa unatumiwa na wakazi wa eneo hilo kupasua mawe na kototo na kuyauza ili wajikimu kimaisha ikiwemo kusomesha watoto wao, kula, kuvaa, kujenga nyumba nzuri, na ajira.

Hakika ni mtikisiko sana ndani ya chama na serikali kwani kuuawa na wapiga kura wako tena ndani ya kata au eneo lako si kitu kidogo kwa chama.
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,979
2,000
Anasubiriwa na hili lijamaa kwa hamu sana;
 

By hair

Senior Member
Sep 6, 2013
141
0
Ujue ubabe wa namna hii tanzania upo sana.yeye alijua hakuna wa kumfanya lolote kwa vile Yuko Chama tawala.wababe wapo wengi Ccm.wananchi hawajaamua tu,siku wakiamua mbona mafisadi yote yatakimbia nchi
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,148
2,000
Mwache aende zake maana hawa watu wanajiona kuwa wao ndio wenye hatimiliki ya Nchi hii na pumzi yetu sisi wanyonge,na kaburi lake linatakiwa lichimbwe 20ft ili kusiwepo na uwezekano wakutoka kabisa huko,nyambafu.
 

M2.

Senior Member
Nov 27, 2013
160
0
Serikali imeteka mazishi ya kijana aliyeuwawa na Mabina, na vyombo vya habari vimeagizwa visiseme kuwa Mabina aliua kwanza ndo na yeye akauwawa!
 

cacico

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
8,377
1,250
aende mwana kwenda! bado yule anayekeketa meno tembo wetu! wauwawe tu kwa kweli, puuuuuuuuuuuuuuu!
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,252
2,000
Haya mabosi mnaopora mali za umma jifunzeni hapa!! mambo yamebadilika kabisa!! watendeeni haki mnaowangoza that is the only solution!! otherwise unaweza usipate hata muda wa kuandika wosia kama huyu ndugu yetu hapa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom