Vyumba vizurii kuanzia elfu70-100,000 self kikubwa kuanzia semtema kushuka chuoni,ambavyo sio self ni elfu 50,mitaa ile ile ya chuoni mpaka juu juu semtema,na kule bwawani..kama unajiweza kwa nauli unaweza kusogea mpaka ngome,changalawe,kihesa,kwa beda,mwang'ingo...
Vimbweta vipo vya kutosha
Kitabu inategemea na course unayosoma ila upande wa law wapo vizuri..
Itunze boom yako nunua kiwanja kigonzile,zungushia uzio/miti ama ukuta.utakuja kunishukuru badae
ONYO: Mwezi wa 11 ikishanyesha tu mvua unaanza msimu ulanzi mpaka mweziwa 4 kaa nao mbali huu ndio unafanya wanafunzi wanafeli wanaanza kusingizia walimu..ulanzi litre 1=500 wa baridi kama umetoka kwenye fridge unashuka kooni kama bia laini..ukikaa kwenye kijumba hukumbuki kipindi kinacho endelea darasani mama muuza anaweza kuwapikia ugali hukohuko...iringa kumenoga na uhakika wa kupata DISCO upo ukiendekeza ulanzi