Mazingira mazuri kwa upinzani

Mazingira mazuri kwa upinzani

mzee wa kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
947
Reaction score
690
Tangia kuwnzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992 na kupelekea kuanzishwa kwa vyama vingi, mazingira ya kuinuka na kustawi kwa upinzani hayajawahi kuwa bora kama ilivyo hivi leo.

Historia ya upinzani nchini Tanzania inaonyesha kuwa viongozi wengi wa vyama vya upinzani kamwe hawajawahi kuwa wapinzani hata siku moja. Wengj wao ni wale waliokosa fursa kwenye serikali au chama tawala na wakakimbilia kuanzisha au kujiunga na vyama vya upinzani kwa lengo la kuendelea kupata maslahi na nafasi za kiuongozi.

Ukiona viongozi wengi wanakimbilia upinzani hiyo ni dalili za wazi kuwa hakuna upinzani wa kweli. Kinyume chake ni kweli tupu, ukiona viongozi wengi wanahama kutoka. Upinzani kuingia serikalini au chama tawala ujue sasa mazingira ya kuinuka na kuwepo upinzani wa kweli ni mazuri.

Mazingira mazuri ya kustawi kwa upinzani kamwe si fare ground kama baadhi ya wapinzani wanavyoomba. Mazungira bora ya kustawi upinzani ni kipindi upinzani unapominywa unapobanwa unapodhibitiwa.

Niliwahi kumsikiliza mh Tindu Lisu akiongea na wana chadema mwaka 2010, naomba kumnukuu: ukiona mnafanya siasa mnafanya maandamano mnafanya mikutano na serikali haiwazui mjui bado mpo mbali sana na kuingia ikulu: Aliendelea kusema: mkitaka kujua sasa mmekaribia ikulu mtakutana na vitisho vya kila aina, wengi wetu hatutafika, baadhi yetu mtafika mkiwa mmeumizwa sana, wengi watashindwa na kujitoa na kutuacha tukipambana. Mwisho wa kumnukuu.

Nini kinachotokea Tanzania hivi leo?
Mazingira yanaonyesha wazi huu ndio wakati wa wapinzani na upinzani wa kweli kushamiri. Tunashuhudia wale wasio tayari kulipa gharama za kuwa wapinzani wakisalimu amri na kujiunga na serikali ama chama tawala, sii vibaya kufanya hivyo lkn ukweli ni huu kwamba hawa hawakuumbwa kuwa wapinzani.

Mpinzani wa kweli yupo tayari kukifia kile anachosimamia au anachokiamini.
Mpinzani wa kweli hataomba fadhila toka watawala ili wamruhusu kusema anachokiamini.
Mpinzani wa kweli hatishwi na vifaru wala mabomu.
Mpinzani wa kweli haogopi kufungwa, kukamatwa au kutekwa.

Ndio maana duniani kote wapinzani ni wachache/namaanisha viongozi/ na wananchi wakiwaona tuu wanawajua na kuwakubali bila kuhongwa wala kushawishiwa kuandamamana, wakitokea barabarani wananchi wanawafuata

Tunamshukuru sana Mungu kwa kutupa mtu mmoja sisi watanzania, hii ni zawadi kwa nchi yetu, nakuombea maisha marefu mpinzani wa kweli mh. Tindu Lisu.

Nini kazi ya waliomtangulia? Kuandaa njia kwa ajili ya ujio wake? Wengi watamsaliti bali wananchi kamwe hawatamsaliti. Viva Lisu.

Siku Lisu akitoka barabarani kudai haki hakuna mwanamke wala mtoto atakayebaki ndani wote watamfuata nyuma hadi anakokwenda. Ikulu?

Upinzani ni hali ya ndani ambayo mtu huzaliwa nayo, kama hali hiyo haipo kubali kuwaaunga mkono wenye nayo.
 
mtoa mada akili yko inaishi kwenye sahani moja na iliyobeba sahani ya ubongo wa TLS

Jamaa anamaono sana kuna speech alisema wakishatumaliza sisi watahamia kwenu ..napia ukichukua hayo maneno yake uliyomnukuu katka uzi huu uzi wako..NI MAONI YALIYOTUNGA MIMBA YA TASWIRA HALISI NA SASA YAMESHA ZAA...
vyombo mbali mbali vyahabari vinaishi kama shetani sasa nawanachi wanyonge hawana hats dalili zkuota mbawa ili waweze kuwa MALAIKA..ndio kwanza wanazidi kupauka nakupoteza ubora wawajihi wao ambao angalau walikuwaga nao hapo awali
 
Back
Top Bottom