Mazingatio ni kwenye herufi au maana ya maneno?

vampire_hunter007

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
1,034
2,616
Habari waheshimiwa,

Mi mgeni humu naomba kuuliza swali...

Katika maongezi huwa mazingatio ni katika herufi au maana ya maneno?

Najua kuna vilaza hawajaelewa, ngoja nifafanue...

Mfano mzuri ni kuhusu viungo vya uzazi, ukitaja uume, dushee, uke, papuchi, hambalulu, sehemu za siri. . .

Maneno yote haya ukiyataja kama mtu anaelewa manake lazma picha itamjia kichwani ya kitu ulichokitaja. Na ataelewa umemaanisha nini..

Hayo majina hapo juu ni mkusanyiko wa alphabets za kiingereza kama maneno mengine yote ninayoyaandika hapa.

Lakini kuna maneno mengine yakitumia mtu anaonekana hana adabu, katukana, kakosea, mhuni, nk japokuwa amemaanisha kitu kile kile. Na akitaja mtu anapata picha ileile.

Na ukiyataja humu jf unaweza ambulia ban au thread yako kufutwa...

Sasa tatizo huwa ni nini? Ni mpangilio wa herufi katika haya maneno? Au?

Mfano badala ya kuandika
Uume au dushee nikaandika mbo......
Au badala ya papuchi nikaandika kum...
Au badala ya mapenzi ya jinsia moja nikaandika kufir....na
Badala ya kufanya tendo la ndoa nikaandika kut...mbana

Japo nimefichaficha hayo maneno kuhofia ban, bado kuna watu wataona nimetukana..Tatizo ni nini?

Why mzazi aone sawa kumwambia mwanaye mdogo afiche dudu yake lakini ahofie kumwambia afiche mbo... yake?

Badala ya kumwambia mtoto wa kike afunike kwa bibi amwambie afunike k..ma..

Mazingatio ni herufi au maana na dhati ya kitu husika?

Karibuni
 
Andika kile ambacho dhamira na nafsi yako haikuhukumu huku ukizingatia kanuni, taratibu na sheria za JF.

No mkuu, nimetaja JF kama mfano tu. . Swali langu ni more general...

Yani mara nyingi mtu nafsi humsuta na kupata ugumu kutamka baadhi ya maneno kumaanisha kitu fulani, lakini yupo comfortable kutumia maneno mengine kumaanisha kitu kile kile,

Ndo maana swali langu likawa ni kwa nini? Ni mpangilio wa herufi katika maneno au ni nini?
Sjui hata kama naeleweka
 
Lugha haishii kwenye tafsiri ya maneno na maana. Lugha inabeba utamaduni, mila na desturi

Kwa mfano, kwa Waingereza kaka wa Mama ni Uncle sawia na Dada wa Baba Auntie, akiwa mdogo wa Baba watamwita Uncle pia.

Kwa Mswahili Mjomba au Baba mdogo inabeba maana kubwa ni zaidi ya Ndugu wa kawaida.

Wewe Mzazi wako akiongopa huwezi kumwambia moja kwa moja "wewe muongo"...kuna lugha ya adabu kumwambia na ambayo itakuwa karibu sawa na "wewe muongo".
 
Kipi kinachofanya neno kuwa kali? Mpaka ifikie hatua tupunguze ukali

Mkuu hata kwenye maelezo yako kuna sehemu umeweka nukta nukta, hicho kilichopelekea maneno mengine uyaandike yote na mengine nukta nukta ndio ni nafsi imekusuta.

Hadi unapofikia umri huu na maisha uliyoishi tayari umeshajifunza kwamba neno hili naweza kulisema popote na lingine siwezi. Ni mapokeo ya mazingira, tamaduni na mila za eneo tunaloishi ndio zinaamua maneno gani makali na yasisemwe hadharani.
 
Back
Top Bottom