Mazingaombwe ni ujuzi gani?

We uliona dalili gani ukajua kwamba hayupo
Hakuna uthibitisho wowote kwa kisicho kuwepo.

Hakuna dalili yeyote kwa kitu ambacho hakipo.

Kisichokuwepo hakipo kwa dalili yeyote ile wala kwa uthibitisho wowote ule.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.
 
Hakuwa na uhusiano wowote na huyo Mwanafunzi. Na ndizi kwa macho ya kawaida ilikuwa nzima, Na kila Mwanafunzi aliiona.
 
Toa hiyo elimu kuhusu namna unavyoweza kusoma majina yaliyokunjwa kwenye karatasi au kama haupo willing kuiweka public nicheki PM. Mana nipo interested walau kujua baadhi ya tricks.

Napenda kujifunza vitu vipya kila siku.
 
Ngoja leo akutokee jini live ndo utaanza kuamini ulimwengu wa ghaibu
Majini hawapo.

Majini ni viumbe ambavyo tumejitungia tu.

Tena wamepewa hadi na majina kabisa.

Kuna jini Makata.

Jini Maimuna.

Jini Subiani.

Hawa wote ni viumbe wa kufikirika tu.

imaginations just an illusion.

Hawapo.
 
Ukifa unaenda wapi
Hauendi mahali.

Ukifa unaoza na kuwa rutuba ya udongo ardhini.

Hukuwa na maisha kabla hujazaliwa Vivyo hivyo, Hutakuwa na maisha ukisha kufa.

You had no life before birth and you will not have life after death.

Are you there?
 
Ya kweli hayo Mkuu?
Bro alikua anapiga hizo mbanga kuweka makaratasi kwenye gazette lililokunjwa kisha inatokea misimbazi kadhaa kisha anairudisha ilipotoka michezo ya kucheza na kitambaa kisha linatokea ua (njiwa) lilikua sio jambo la hatari kwake na aliwahi kutuonyesha michezo ya kuleta ndizi, embe mpaka majani ya chai tena majani ya chai nakumbuka aliruhusu tupikie chai tunywe na tukafanya hivyo kutoka kusikojulikana ni ilikua jambo la kawaida kabisa, sasa alipomaliza shughuli zake town akarudi bush kule hawakumuelewa unajua siku zote nabii hakubaliwi nyumbani kwao na professional yake alikua ni Mwalimu wa Primary tu hadi anafariki ndio kazi alikua anaifanya kufundisha watoto kwa hio unafika muda humo humo class anapiga show ya bure anaingia bila chai kisha chaki inaletwa kutoka kusikojulikana, point ya kwanza walisema ni Mchawi point ya pili walisema vile vitu anavyoleta anaiba kwenye maduka yao yaan chuma ulete, kingine bro alikua hapendi kumfundisha mtu hizo mambo kabisa yaan hata ungemwambiaje akufundishe alikataa sababu yeye pekee ndio alikua anaijua hatari yake na hakuwahi kusema ni hatari kiasi gani kufanya vile
 
Hakuna uthibitisho wowote kwa kisicho kuwepo.

Hakuna dalili yeyote kwa kitu ambacho hakipo.

Kisichokuwepo hakipo kwa dalili yeyote ile wala kwa uthibitisho wowote ule.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Alikuwa na balaa lake.
 
Wewe umeshindwa kuelewa ni namna gani huyo jamaa anaweza kumeza hiyo hela, Halafu unasema ni uchawi.

Umejuaje ni uchawi na si maarifa ambayo wewe huyaelewi?
Mi nimehitimisha kuwa ni uchawi..wew unaebisha ndio uniambie ni maarifa gani anatumia kuamisha ela kutoka mdomoni hadi mfukoni?
 
Toa codes kuhusu hiyo elimu.

Au kama ni mwiko kuweka hadharani njoo PM unipe tips kidogo.
 
Early 1990's ,wanamazingaombwe walikuja kijijini kwetu na makutano yalikuwa ndani ya Godowns ya mazao zike alizojenga Hayati Ally Hassan Mwinyi ambayo kwa wakati huo ilikuwa siyo msimu wa kahawa,Baba alipiga marufuku sisi watoto wake kwenda kwenye event ile, lakini kwa demo waliyotuonyesha shule ya msingi kwangu ilikuwa ngumu kuto kwenda.Wale jamaa walifanya mengi ila nikiwa nazubaa zubaa pale mbele nikiwa dogo sana,alikuja na kuonekana ametoa shilingi kwenye pua,ikawa story kubwa kijijini na Baba akapata taarifa,kipigo nilichopata sijawahi sahau
 
Wachungaji wengi tu mbona Ni wanamazingaumbwe si mkawaulize!
Na kuna mtu anafundisha hayo mambo yupo pale mkata njia panda ya kwenda kwa msisi tanga!
 
Kunq huyo mwamba wa kuitwa chriss angel, mmarekani huyu, kama ni mazingaombwe basi labda yalizaliwa kwao, huwa ananiacha mdomo wazi.
Yule hamna kitu pale.
Nimeshamfatilia sana ni muongo, na ni tricks tu anatumia.
Hana mazingaombwe yoyote
 
Sawa,.Lakini nauliza ni elimu gani Ile?

Kwanini mtu awe kama amepumbazwa?
Inaitwa white magic hata mitume na manabii wa miujiza wanafanya hizi mambo ukisoma ujuzi huo utafundishwa vyote ikiwemo mind control, magic trick,nk.
Hizi ni elimu chache kwa wanaziitaji.
Kuna elimu za ujuzi mbalimbali hata wwe ukitaka unasoma unajifunza mfano.
Kuuita mtu mkubwa kama mwembe ukufuate au ukimbie na watu wanashuhudia,kuna kupotea ghafla watu wasikuone hii kwa wanaofanya ninja wanasoma, kuna kupenya kwenye ukuta wowote ukaingia au kutoka ndani ya jengo bila kubomoa ukuta,kuna kuzuia nguvu ya risasi kisu isipenye mwilini,kuna kusoma mawazo ya mtu ukajua anawaza nini.nk hizi ni elimu kama zingine tu unajifunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…