Mazingaombwe ni fani kama Siasa?

Mazingaombwe ni fani kama Siasa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,253
Reaction score
44,591
Wazo la Kuanzia Wiki: Mazingaombwe ni fani; ni fani ambayo mtu hujifunza wengine hata toka utoto. Zamani nilidhani kuwa ni uchawi fulani hivi, kumbe ni fani ambayo inatumia sayansi ya kawaida tu ya udhaifu wa macho ya mwanadamu kuweza kulaghai. Macho ya mwanadamu siyo ya kuaminika sana kama watu wanavyojua. Yapo mazoezi mengi ambayo yameonesha jinsi gani watu hata wakiwa kwenye kundi moja wanaweza kabisa kukosa kuona kitu kinachotokea mbele yao hata kama walikuwa wanakodoa.

Ni kwa sababu hiyo mazingaombwe yanatumia udhaifu huu kufanya kile kitu kinachoitwa "kiinimacho" (Illusion). Kiini macho kinafanikiwa kwa kile kinachoitwa "wepesi wa mkono" (sleight of the hand).

Baada ya jina la Magufuli kutajwa nimeona baadhi ya watu wameshabadilika kabisa na kuamini. Wameamini mazingaombwe na wako tayari kabisa kuapa kuwa walichokiona ni kuwa mtu kweli kakatwa katikati! Macho yao yamewaonesha hivyo na ubongo wao umepokea hivyo na hivyo na wao wamekubali hivyo.

Hata watu wengine hawakuwa na imani na CCM masaa machache tu sasa wamekuwa na imani kabisa kisa macho yao yamewaonesha Magufuli!

Ni vigumu sana mtu anayeamini mazingaombwe kuweza kumfanya abadilishe mawazo kwa sababu atakuwa anakwenda kinyume na kile ambacho ubongo wake umetafsiri kutoka kwenye macho. Magufuli kabebwa, Magufuli mcheshi, Magufuli kamwaga namba kama kawaida, Magufuli kajenga barabara (utadhani hela alitoa mfukoni mwake!), Magufuli hivi Magufuli lile. Wanasahau kabisa CCM. Wengine wanasema "Hata kama mimi siipendi CCM lakini Magufuli namkubali".

Mazingaombwe ni fani. Angalia Smoothin!

​
 
Last edited by a moderator:
Kwani hata ujenzi wa barabara tunazotumia na ile meli aliyokamata ikivua kinyume na sheria kwenye bahari yetu ni mazingaombwe?

Ujenzi wa barabara zilizo chini ya kiwango ilhali bajeti zake ni kufuru? Ukamataji wa meli yenye vibali na vigezo vyote vya uvuvi wa kimataifa then mwisho wa siku tukaishia kupigwa faini ya mabilioni ya pesa? Hivyo vyote ni viini macho tu.

DELETE CCM ndo mpango mzima. Mkakati mzuri ni kukidhi uwiano wa safu ya mashambulizi Bungeni kwa kuingiza wabunge wengi na wapambanaji jamii ya J.J.Mnyika automatically Magamba mta step out Jumba jeupe.
 
Tunajua kabisa mwaka huu wa uchaguzi ni ngumu sana kwa UKAWA kuingia magogoni kwa CCM kumsimamisha magufuli,Ni nafuu kama angekuwa Lowassa au Membe jwa sababu watu wengi ambao ni wanaccm na hata wasio wanaccm wana imani na Magufuli...na sijui ni kutugani kita badilisha hiyo mindset...nafikiri labda baada ya miaka 5 ndiyo watanzania watakuja kugundua utofauti..ili 2020 wafanye maamuzi sasa..lakini kwa sasa itakuwa ngumu sana
 
Labda usichotaka kukielewa ni kwamba Watz wengi kwa wingi wao ni CCM ni wachache sana ndiyo wako Upinzani kiuhalisia, tatizo lililokuwepo ni kwamba Watz wengi walipoteza Imani na CCM na ndio baadhi yao waliacha kupiga kura na wengineo kujaribu bahati yao Upinzani.

Lakini pale ambapo CCM ilipoteua Mtu ambaye Watz wengi wanamkubali na ushahidi tulionao, ni utendaji wake peke yake na hatuhitaji Ushahidi mwingine, basi Imani imerudi na wengi wao hasa wale waliokata tamaa na CCM wamerudi, waliosusa kupiga kura wamerudi, waliohamia Upinzani wanaangalia tena msimamo wao.

Niko mitaani na watu wote hawa wawili na pale Magufuli alipotangazwa watu walishangilia mpaka nikawauliza lkn ninyi si ni CHADEMA? Majibu yao, ndiyo lakini jamaa tunamkubali sana! Wazungu wanasema go figure...

Uchaguzi ujao nakuhakikishia Upinzani wakifikisha asilimia 7% ya kura zote wamejitahidi sana, Oktoba siyo mbali!
 
Kwani hata ujenzi wa barabara tunazotumia na ile meli aliyokamata ikivua kinyume na sheria kwenye bahari yetu ni mazingaombwe?

Lizabon kwa uhakika ninajua ndani ya Moyo wako unajua kwamba Jamaa yetu aka Ma-Padlock hawezi kuondoa uozo,ubadhirifu wa mali za umma,wizi,rushwa,ufisadi na hasa ukizingati ule Muswada tata kupitishwa jioni bila kuzingatia akidi ya wabunge.

Lizaboni japo kwa mara ya kwanza weka utaifa pembeni uchama baadaye tunahitaji zaidi ya huyu anayetudanganya kwa kukremu number.Huyu ambaye mvua moja tu imenyesha hatuna barabara nchi nzima halafu mnamuitwa Semi-Muadailifu.
 
MMM, binafsi ninawashangaa sana WaTZ....tatizo sio mtu mmoja mmoja, tatizo ni mfumo CCM..... Tuamke jamani, Tatizo letu sisi sio mtu, ni Chama chote cha Mapinduzi

Delete CCM
 
Swali ni kwamba ni yupi mbadala wa Magufuli kwa sasa, ambaye hana doa na mwenye utendaji unaokubalika na Watz wengi?
 
Tunajua kabisa mwaka huu wa uchaguzi ni ngumu sana kwa UKAWA kuingia magogoni kwa CCM kumsimamisha magufuli,Ni nafuu kama angekuwa Lowassa au Membe jwa sababu watu wengi ambao ni wanaccm na hata wasio wanaccm wana imani na Magufuli...na sijui ni kutugani kita badilisha hiyo mindset...nafikiri labda baada ya miaka 5 ndiyo watanzania watakuja kugundua utofauti..ili 2020 wafanye maamuzi sasa..lakini kwa sasa itakuwa ngumu sana

2005 Ilikuwa tena hvyo tulimpa miaka 10 hamna alicho kifanya sasa tunampa tena huyu miaka mingine 10 ndiyo tuchukue maamuzi magumu! 2020 hali itakuwa ngumu sana atajitokeza tena mwingne tutampa miaka mingne 10 ccm du! hapana bora tufanye maamuzi magumu oct
 
Ajabu sana! Ujinga wa Watanzania wengi vimekuwa ni silaha na mtaji wa CCM, kwa kweli inasikitisha sana.

Kuna watu wameandika mada, na wengi watatoa mada kwa njia za redio, tv, magazeti, midahalo nk eti kusifia mazingaombwe hayo ya CCM. Kuna watu eti wameona na wanasifia ubunifu, mbinu na uwezo wa CCM na eti sasa CCM imerudi kwenye mstari (upi?) - hii ni aibu kwa utu wa mwanadamu yeyote.

Nashukuru kwa kupaza sauti yako mapema kwenye hili MMM.
 
Kwani hata ujenzi wa barabara tunazotumia na ile meli aliyokamata ikivua kinyume na sheria kwenye bahari yetu ni mazingaombwe?

Unauliza majibu?

SAMAKI WA MAGUFULI CASE: Govt is ordered to pay over 2bn/-, release fishing vessel

The High Court in Dar es Salaam has ordered the Ministry of Livestock Development and Fishers to release the ship ‘Tawariq 1' and 296.3 tons of fish worth more than 2bn/- properties of two Chinese nationals, Hsu Chin Tai and Zhao Haquing.

The Chinese nationals were charged for carrying out fishing activities in the exclusive economic zone (EEZ) in Tanzania.

A letter signed by the High Court Registrar on December 17 last year, called on the government to refer to its promises via the affidavit issued by Godfrey Nanyaro and the Permanent Secretary of the said ministry Charles Nyamlundana.

The oath on the letter said that if the accused will not be convicted in court the government will pay the cost of the fish which is 2,074,249,000/- within 30 days from the acquittal of them after being found not guilty.

The letter also showed the copy of the order that directed the fish to be sold. The order was issued by Judge Radhia Sheikh on December 11, 2009.

Earlier September 1 last year, the defence advocates submitted the letter of the said evidence before the registrar of the said court. In the letter the advocates requested the court to give back the accused evidence submitted by the High Court in the case number 38 of 2009 before Judge Sheikh during the case.

In 2009 the two accused and other 36, were charged before the court with the offence of carrying out fishing activities in the exclusive economic zone of Tanzania and sentenced to 20 years imprisonment.

But they however appealed to the court of Appeal which reversed the decision of High court and set free the accused. Immediately thereafter they were arrested and charged before the Kisutu Resident Magistrate's Court on August 14, last year and the DPP withdrew the charges.
Source: The Guardian
 
MMM, binafsi ninawashangaa sana WaTZ....tatizo sio mtu mmoja mmoja, tatizo ni mfumo CCM..... Tuamke jamani, Tatizo letu sisi sio mtu, ni Chama chote cha Mapinduzi

Delete CCM

Mkuu uko sahihi kabisa.

Watu wanasahau kuwa anayeoga kwenye ziwa lililojaa tope hawezi kuwa msafi hata siku moja. Akitaka kutakata labda atafute maji masafi sehemu nyingine au ahamishe tope lote kwenye ziwa... zoezi ambalo si rahisi.
 
Halafu tum-paste nani? ndiyo swali linalohitaji Jibu!

Mkuu deletion inahitaji uweke new information...cut ndio itakupa option ya ku-peste....tukiwa wajinga kwa swali unaloliuliza, inaonyesha wewe maisha yako yoooote yako kimfumo CCM...badilisha...penda kuona mabadiliko....acha uoga wa kufanya changes.....change is what makes you that man....amka kakaa
 
Swali ni kwamba ni yupi mbadala wa Magufuli kwa sasa ambaye hana doa na mwenye utendaji unaokubalika na Watz wengi?

Tunatakiwa tuwashinikize wapinzani wamuweke MTANZANIA ambaye anauzika na kweli ukimuona kwa macho akikwambia nitapambana na RUSHWA au UFISADI basi tujue uso na mwenendo wake unaonyesha hivyo.

Kwa sasa achana na huyu Semi-Msafi,bado CCM kulikuwa na wasafi pure kabisa lakini siyo tu hawakuchaguliwa hawakuonekana sababu wanawaogopa wakiwaweka siri nyingi zitafichuka,pili kwa upande wangu pamoja na usafi wao kuliondoa JINI lililopo ndani yako si rahisi,wahitaji mchungaji,mganga au kusomewa na Shekhe toka nje,kama daktari hawezi kujiganga hata mchungaji hawezi kujiganga.

Tunatakiwa kuisafisha SYSTEM nzima ndani ya serikali,kulitoa SHETANI/JINI la ubadhirifu,Rushwa,uvunjifu wa katiab tunahitahitaji Mganga/Shekhe au Mchungaji toka nje ya System ya CCM iliyodumu kwa miaka 50+.ALiyeko ndani hawezi kutusaidia, na yeye kama hajala kapewa kumfungua mwenzie siyo rahisi.

Wapinzani tuleteeni Paka atakayemfunga PANYA kengele...
 
Swali ni kwamba ni yupi mbadala wa Magufuli kwa sasa ambaye hana doa na mwenye utendaji unaokubalika na Watz wengi?
Unaambiwa tatizo sio mtu ni mfumo wa chama cha mapinduzi, sio mbadala wa mtu ni mbadala wa chama. Binafsi siamini hata malaika akigombea kwa CCM ataleta mabadiliko yoyote
 
Labda usichotaka kukielewa ni kwamba Watz wengi kwa wingi wao ni CCM ni wachache sana ndiyo wako Upinzani kiuhalisia, tatizo lililokuwepo ni kwamba Watz wengi walipoteza Imani na CCM na ndio baadhi yao waliacha kupiga kura na wengineo kujaribu bahati yao Upinzani.

Lakini pale ambapo CCM ilipoteua Mtu ambaye Watz wengi wanamkubali na ushahidi tulionao, ni utendaji wake peke yake na hatuhitaji Ushahidi mwingine, basi Imani imerudi na wengi wao hasa wale waliokata tamaa na CCM wamerudi, waliosusa kupiga kura wamerudi, waliohamia Upinzani wanaangalia tena msimamo wao.

Niko mitaani na watu wote hawa wawili na pale Magufuli alipotangazwa watu walishangilia mpaka nikawauliza lkn ninyi si ni CHADEMA? Majibu yao, ndiyo lakini jamaa tunamkubali sana! Wazungu wanasema go figure...

Uchaguzi ujao nakuhakikishia Upinzani wakifikisha asilimia 7% ya kura zote wamejitahidi sana, Oktoba siyo mbali!

Uliokutana nao ni wale wasiojua kutofautisha number ikiwa -VE au +VE ni number mbili sawa sawa lakini kinachozitofautisha ni zilivyo umbwa HASI na CHANYA.

Bado Magufuli ni ile ile number haina tofauti na wengine ndani ya mtungu.

Sikuwahi kumuamini Magufuli na sitamuamini leo wala kesho.Huyu hana ubavu wa kutuondoa tulipo.Yupo juu kwenye ku-kremu tu.

Ni mwizi na fisadi kama wenzake tu,hakuwa na ubavu wa kusema hapana wakati wanajibinfsisha nyumba za serikali,hadi kumpa nyumba ya serikali girlfriend wake.

Leo Wizara yake imejaa rushwa na ufisadi mkubwa alioushindwa kuuondoa kwenye wizara ndogo tu. Leo unataka kutuaminisha Magufuli anaweza kwa Tanzania yote?

Hata kwa pesa Magufuli hatufai kabisaaa, huyu ni wale wale ,wa historia ile ile na utendaji kazi ule ule.

Ni shida lakini siwezi kuwasemea hao uliowa interview sababu sijui uliwapata maeneo gani pia.
 
Uliokutana nao ni wale wasiojua kutofautisha number ikiwa -VE au +VE ni number mbili sawa sawa lakini kinachozitofautisha ni zilivyo umbwa HASI na CHANYA.

Bado Magufuli ni ile ile number haina tofauti na wengine ndani ya mtungu.

Sikuwahi kumuamini Magufuli na sitamuamini leo wala kesho.Huyu hana ubavu wa kutuondoa tulipo.Yupo juu kwenye ku-kremu tu.

Ni mwizi na fisadi kama wenzake tu,hakuwa na ubavu wa kusema hapana wakati wanajibinfsisha nyumba za serikali,hadi kumpa nyumba ya serikali girlfriend wake.

Leo Wizara yake imejaa rushwa na ufisadi mkubwa alioushindw akuuondoa kwenye wizara ndogo tu.Leo unataka kutuaminisha Magufuli anaweza kwa Tanzania yote?

Hata kwa pesa Magufuli hatufai kabisaaaaaaaaaaaaaaahuyu ni wale wale ,wa historia ile ile na utendaji kazi ule ule.

Ni shida lakini siwezi kuwasemea hao uliowa interview sababu sijui uliwapata maeneo gani pia.

Sawa huo ni mtazamo wako labda sasa sijui yupi angefaa kwako ili tulimnganishe na Magufuli?
 
unaambiwa tatizo sio mtu ni mfumo wa chama cha magamba, sio mbadala wa mtu ni mbadala wa chama. Binafsi siamini hata malaika akigombea kwa ccm ataleta mabadiliko yoyote

Sawa basi huwo mbadala wa chama ni upi ambao unatufaa ukilinganisha na CCM? Na kwa nini unafikiri huwo mbadala ni bora klk CCM?
 
Inasikitisha waTz tusivyofikiri kuwa tatizo sio mtu bali system yote ya ccm. Wandugu elimu inahitajika hata kwa watu walioenda shule. Eti wanamsifia lakini yuko kwenye system mbovu. Inaudhi kuona watu unaoona wanauelewa wakishabikia huu uteuzi. S$$$$$$$.
 
Back
Top Bottom