Mazingaombwe ni fani kama Siasa?

Mazingaombwe ni fani kama Siasa?

Unaambiwa tatizo sio mtu ni mfumo wa chama cha mapinduzi, sio mbadala wa mtu ni mbadala wa chama. Binafsi siamini hata malaika akigombea kwa CCM ataleta mabadiliko yoyote

Hao ndo watanzania wanaojaza vyeti na kujiita wasomi, utawezaje kuwaza kuichagua CCM bila critical thinking?
 
Labda usichotaka kukielewa ni kwamba Watz wengi kwa wingi wao ni CCM ni wachache sana ndiyo wako Upinzani kiuhalisia, tatizo lililokuwepo ni kwamba Watz wengi walipoteza Imani na CCM na ndio baadhi yao waliacha kupiga kura na wengineo kujaribu bahati yao Upinzani.

Lakini pale ambapo CCM ilipoteua Mtu ambaye Watz wengi wanamkubali na ushahidi tulionao, ni utendaji wake peke yake na hatuhitaji Ushahidi mwingine, basi Imani imerudi na wengi wao hasa wale waliokata tamaa na CCM wamerudi, waliosusa kupiga kura wamerudi, waliohamia Upinzani wanaangalia tena msimamo wao.

Niko mitaani na watu wote hawa wawili na pale Magufuli alipotangazwa watu walishangilia mpaka nikawauliza lkn ninyi si ni CHADEMA? Majibu yao, ndiyo lakini jamaa tunamkubali sana! Wazungu wanasema go figure...

Uchaguzi ujao nakuhakikishia Upinzani wakifikisha asilimia 7% ya kura zote wamejitahidi sana, Oktoba siyo mbali!

hizi asilimia hata upinzani ukiweka kivuli zitakuwa nyingi zaidi ya hizo....kuna mtu alikubalika kama JK 2005...Lakini mwisho wa siku hakuna la maana alilofanya......Watanganyika na Wazanzibar tu wepesi wa kusahau....MAGUFULI kikosi kazi chake sijui atakisajili kutoka wapi.......ni walewale wa JK,MKAPA,MWINYI na Wengine toka enzi Nyerere labda sura mpya zitakuwa chache sana.....
 
Huhitaji wazungu waje kukupa elimu ya kujitambua.
 
Huko upinzani kuna wengi wazuri zaidi ya huyo Magufuli,na kitu kilichobaki upinzani kutoka na mtu bora zaidi.

Kumbe na wewe ndio wale wale tu unasema hiki hakifahi lkn hutaki kusema kipi kinafaa! Mimi nilifikiri kumpinga kote kule Bw.Magufuli tayari una mtu/chama mbadala kumbe hauna lkn bado unasema Bw.Magufuli hafai, sasa hauwezi kushinda uchaguzi kwa kusema tu wapo wengi wanafaa wepi hao? CCM wameonyesha wao na tunamjua tunamchambua ktkna na kazi alizozifanya huko nyuma na mpaka sasa hivi Watz wengi wamempenda!
 
yaani ukawa mmepanic kweli, baada ya kuona ccm wamechagua jembe hakuna namna ya kumchafua mmeamua kuanza kudeal na mfumo wa ccm coz kumponda Magufuli mnaona raia hawawezi kuwaelewa. Mimi binafsi hadi leo hii huwa sijielewi niko chama gani coz huwa nadili na kichwa tu, nikifurahishwa na mgombea hata awe NCCR nachagua tu, kwa Magufuli CCM wamenishawishi kuwapa kura yao maana hakuna namna nyingine tena, kwenye ubunge ukawa msiwe na wasi kura yangu mtapata maana mbunge wetu wa ccm ni ----- sana
 
Umeambiwa tatizo sio Mapadlock bali mfumo, na hao uliowaohoji wamesema wanaimani na yeye na sio mfumo

Bado unazunguka tu kwenye duara, kama tatizo ni mfumo mbaya wa CCM, sasa mfumo mbadala kwako ni Upi? Na unaofatwa nani/ Chama gani hapa TanZania?
 
Bado unazunguka tu kwenye duara, kama tatizo ni mfumo mbaya wa CCM, sasa mfumo mbadala kwako ni Upi? Na unaofatwa nani/ Chama gani hapa TanZania?

Acha ligi za kitutusa, Nyerere aliposema watu wasipoyapata mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM ulimwelewa? unaelewa mantiki yake?

Kutokana na ugumu wako wa kuelewa, jibu lake ni kuwa mfumo mbadala ni ule usio wa CCM short and clear.

Yaani kilichofanyika ni kuweka maharage safi kwenye chombo kilichochachisha mengine ukitegemea kutoa maharage safi, utalumangia!
 
Kwa kuwa ni maoni yako nayaheshimu nikitegemea na wewe labda pia utaheshimu ya kwangu na ya WatanZania wengine ya kwamba mimi ya kwangu bado mfumo bora ni wa CCM na mpaka sasa hivi sijaona mbadala!
Tuishie Hapo!
​
 
Kumbe na wewe ndio wale wale tu unasema hiki hakifahi lkn hutaki kusema kipi kinafaa! Mimi nilifikiri kumpinga kote kule Bw.Magufuli tayari una mtu/chama mbadala kumbe hauna lkn bado unasema Bw.Magufuli hafai, sasa hauwezi kushinda uchaguzi kwa kusema tu wapo wengi wanafaa wepi hao? CCM wameonyesha wao na tunamjua tunamchambua ktkna na kazi alizozifanya huko nyuma na mpaka sasa hivi Watz wengi wamempenda!

Kaka soma between the lines.Ninachosema ni kuwa tunahitaji UPINZANI watuletee MGOMBEA ambaye atakuwa zaidi ya magufuli,

Mimi nipo upinzani,na bado nitatetea upinzani,na nina amini ndani ya CCM hakuwezi kutoka RAIS ambaye atatuvusha.

TUnahitaji RAIS atakayeweza kumudu maswali yote ya upande wa pili yaani CCM.Bado nasema na nitarudia kusema hatuhitaji RAIS kutoka CCM maana ni wale wale.Ni mvinyo ule ule ila umebadilishwa chupa tu.
 
kupata viongozi bora tanzania lazima azimio la.zanzibar life na kuwa na katiba ambayo ita wabana viongozi kuhusu maadili
 
Tunajua kabisa mwaka huu wa uchaguzi ni ngumu sana kwa UKAWA kuingia magogoni kwa CCM kumsimamisha magufuli,Ni nafuu kama angekuwa Lowassa au Membe jwa sababu watu wengi ambao ni wanaccm na hata wasio wanaccm wana imani na Magufuli...na sijui ni kutugani kita badilisha hiyo mindset...nafikiri labda baada ya miaka 5 ndiyo watanzania watakuja kugundua utofauti..ili 2020 wafanye maamuzi sasa..lakini kwa sasa itakuwa ngumu sana

ccm wanajua kuwa watanzania weng huwa hawafikirii kwanza na ni wajinga hata hiyo 2020 ccm watakuwa wamejpanga namna ya kuwadanganya na wa tz watakubali tu mziki'
 
Tatizo mnawaambia wananchi wasimchague Magufuli halafu hamuwapi alternative!.

Waambieni wamchague nani badala ya Magufuli. Au mnataka wasipige kura?
 
Hata watu wengine hawakuwa na imani na CCM masaa machache tu sasa wamekuwa na imani kabisa kisa macho yao yamewaonesha Magufuli!

Ni vigumu sana mtu anayeamini mazingaombwe kuweza kumfanya abadilishe mawazo kwa sababu atakuwa anakwenda kinyume na kile ambacho ubongo wake umetafsiri kutoka kwenye macho. Magufuli kabebwa, Magufuli mcheshi, Magufuli kamwaga namba kama kawaida, Magufuli kajenga barabara (utadhani hela alitoa mfukoni mwake!), Magufuli hivi Magufuli lile. Wanasahau kabisa CCM. Wengine wanasema "Hata kama mimi siipendi CCM lakini Magufuli namkubali".

Mazingaombwe ni fani. Angalia Smoothin!

​

Mkuu MKJJ-
Mtu yeyote anayetaja SERA zake kuwa nizile za CCM ambao ndizo zimepelekea nchi kufikia ilipo ni wa kuogopwa tu. Inajulikana wazi kwamba sera zilizotufikisha tulipo haziwezi na hazitaweza kututoa! Period. Angejitokeza mkweli akazinadi SERA zake kwetu tukazitafakari na kutofautisha na UJUHA uliozoeleka basi labda huyo tungemhukumu kisawasawa. Tofauti na hayo, yale tunayoyaona na kushuhudia leo havifananishiki na mazingaombwe kwa vile MACHO tunayo ila hatupendi KUTAZAMA na hata KUONA na kwa hiyo kutafakari. Inawezekana kabisa nchi hii ina WAJINGA WENGI KUPINDUKIA. PERIOD!
 
Last edited by a moderator:
Wazo la Kuanzia Wiki: Mazingaombwe ni fani; ni fani ambayo mtu hujifunza wengine hata toka utoto. Zamani nilidhani kuwa ni uchawi fulani hivi, kumbe ni fani ambayo inatumia sayansi ya kawaida tu ya udhaifu wa macho ya mwanadamu kuweza kulaghai. Macho ya mwanadamu siyo ya kuaminika sana kama watu wanavyojua. Yapo mazoezi mengi ambayo yameonesha jinsi gani watu hata wakiwa kwenye kundi moja wanaweza kabisa kukosa kuona kitu kinachotokea mbele yao hata kama walikuwa wanakodoa.

Ni kwa sababu hiyo mazingaombwe yanatumia udhaifu huu kufanya kile kitu kinachoitwa "kiinimacho" (Illusion). Kiini macho kinafanikiwa kwa kile kinachoitwa "wepesi wa mkono" (sleight of the hand).

Baada ya jina la Magufuli kutajwa nimeona baadhi ya watu wameshabadilika kabisa na kuamini. Wameamini mazingaombwe na wako tayari kabisa kuapa kuwa walichokiona ni kuwa mtu kweli kakatwa katikati! Macho yao yamewaonesha hivyo na ubongo wao umepokea hivyo na hivyo na wao wamekubali hivyo.

Hata watu wengine hawakuwa na imani na CCM masaa machache tu sasa wamekuwa na imani kabisa kisa macho yao yamewaonesha Magufuli!

Ni vigumu sana mtu anayeamini mazingaombwe kuweza kumfanya abadilishe mawazo kwa sababu atakuwa anakwenda kinyume na kile ambacho ubongo wake umetafsiri kutoka kwenye macho. Magufuli kabebwa, Magufuli mcheshi, Magufuli kamwaga namba kama kawaida, Magufuli kajenga barabara (utadhani hela alitoa mfukoni mwake!), Magufuli hivi Magufuli lile. Wanasahau kabisa CCM. Wengine wanasema "Hata kama mimi siipendi CCM lakini Magufuli namkubali".

Mazingaombwe ni fani. Angalia Smoothin!

​

Mzee naona umeishiwa hoja kabisa umehamia kwenye mazingaombwe...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom