Mazimwi huwauwa waliyoyatengeneza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazimwi huwauwa waliyoyatengeneza!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tegelezeni, Apr 10, 2012.

 1. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama ukichunguza kwa mfuatano, tukio la hivi karibuni la Lulu kuhusishwa na mauaji ya Kanumba, siamini kama hilo linaweza kuzusha mshangao.

  Binti kama Lulu kwanza amelelewa na malezi ya upande mmoja, yaani kalelewa na mama yake tu……..na wakati bado akihitaji malezi ya karibu kutoka kwa mama yake, akavutwa na watengeneza filamu wa Bongo walioibuka kama uyoga……….tamaa ya fedha na kutafuta rasilimali watu rahisi inamkumba binti huyu kwa kigezo cha kuwezeshwa kujiajiri ili apate kusoma kwa ustawi wa maisha yake na familia yake.

  Binti huyu anafinyangwa kitabia na jamii hii ya waigizaji waliokimbilia cheap popularity baada ya kushindwa kuendelea na masomo au kufukuzwa shule kutokana na tabia zisizofaa.

  Taaluma ya filamu hapa nchini haiongozwi na watu wenye taaluma hiyo, bali wababaishaji na watu walioshindwa maisha……….na kutokana na ugeni wetu katika jambo hilo (Mkumbuke kwamba kwa takriban miaka 27 ya utawala wa chama kimoja tulikuwa hatujui TV ni kitu gani) tasnia hiyo ikajizolea umaarufu na ikawa ndio njia rahisi kwa wale wasio na elimu kujiingizia kipato si haba.

  Hao ndio tunaowaita kioo cha jamii ambao walimchukua binti huyu Lulu na kumuingiza katika mkumbo huo pasipo kumlinda, aliachwa huria akawa hashikiki na kuandikwa kwake magazetini sio kwa mema bali kwa mabaya anayoyatenda kukampa kichwa na kujiona yuko juu ya kila mtu.

  Kwa yaliyotokea ingawa inasikitisha lakini hilo ni funzo kwetu kwamba tunahitaji busara na hekima ya hali ya juu sana katika kukuza vipaji vya watoto wetu.
   
 2. Mandown

  Mandown JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 1,575
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,865
  Likes Received: 6,216
  Trophy Points: 280
  enough!
   
 4. M

  MADABADA Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nice advice!
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Neno, ingawa chungu kulimeza!
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  acha nipite tu, na uwezo wa kuponda hapa mwanzo mwisho.

  Just let them be, hakuna mtakatifu, kuna watakavitu tu.
   
 7. Buggy

  Buggy JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa, wasanii wetu wengi wao hawajasoma na hata hawajui kujieleza pale wanapokutana na vyombo vya habari! kujieleza tu kwao ni shida, hususan pale linapokuja suala la lugha ya kiingereza! wengi hawajasoma na uelewa wao wa masuala ya film industry ni mdogo mno! wanafikiri u-superstar ndio mwisho na mwanzo wa mafanikio, kumbe suala kubwa linalohitajika ni talent, discipline, creativity na kujituma!
   
 8. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Majungu Manjungu!!!

  Hivi wewe ulipenda iwe kama Nigeria? ambako wasomi hawana dili? Badala ushukuru hata hao vijana wameweza kutengeneza soko la ajira eti walishindwa shule? Wewe ni mjinga tena sana kwani mimi ni msomi, namheshimu kila mtu na kazi yake, kwani kusoma siyo kila kitu.
  Nakuuliza swali.
  1. Wewe na usomi wako umelifanyia nini taifa?
  Mchango wa wasanii unaonekana, wamekonga nyoyo za watu, wametoa burudani, na wameitangaza Tanzania.
  Kaa na mawazo yako ya kimasikini ukidhani usomi wako utakusaidia wenzako wataendelea kupeta kwa majina makubwa halafu wewe utabaki mdogo kama kimchanga na hakuna anayekutambua Tanzania zaidi ya wanao na mkeo tu.
  R.I.P kanumba! You were the great!
   
 9. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  @ Red ... You said it all!!!!
   
 10. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,454
  Trophy Points: 280
  you never miss a good thing till it is gone.
  RIP KANUMBA
   
Loading...