Mayalla: Walinilazimisha kukiri kosa

Mayalla: Walinilazimisha kukiri kosa

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,826
Reaction score
25,109
Katika video inayozunguka kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, inamuonyesha mwandishi wa habari nguli ambaye pia ni mwanasheria na mwanaJF ndugu Pascal Mayalla , akidai kuwa alilazimishwa kukiri kosa alipoitwa na JAB kujitetea kwanini ametoa maoni yasiyopendwa na utawala kuhusu tukio moja la kisiasa lililotokea hivi karibuni.

Katika video hiyo, ambayo Mayalla ameonekana amevaa miwani myeusi huku akihojiwa na mwandishi nguli wa DW, Sudi Mnede, ameonekana wazi kukerwa na wito alioitwa na mamlaka kujitetea kwanini ametoa maoni ya kuudhi watawala. Ukimwangalia usoni na jinsi anavyojibu utaona wazi kuwa hakupendezwa na kitendo cha kulazimishwa kukiri kosa kinyume cha sheria.
Soma
Kufuatia kukamiwa kwa jukwaa la JF na utawala, nimeshindwa kuambatanisha video hiyo kwani kila nikiweka inagoma kupakilika. Tafadhali kama kuna mods au mtu yeyote anayeweza kunisaidia kuweka video hiyo nitashukuru sana.

Nawasilisha
.
 
View attachment 3552709

Nawasilisha.
CHAWA PHILOSOPHY inapolazimishwa kwa kila mtu kuikubali.
Its against the Constitution.
Hawa JAB na TCRA wanalijua hilo?
 
Back
Top Bottom