Mkuu 1800 na Mkuu Chasha nawashukuru sana kwa kujali na kujibu swali langu. Mara baada ya kusoma thread hii niliingia kwenye mtandao, You tube, nikashuhudia ufugaji mkubwa huko Asia, yaani kwale wanafugwa kama utitiri! Ndipo nikaandika hapa kuulizia maana nilikuta hadi video clip ya mfugaji wa Kenya akilelezea faida ya mayai ya Kwale mbele ya banda lake. Lakini kama haitoshi nikasema hebu nisearch tena JF labda kuna thread nyingine ya Kwale, nikakutana na thread nyingine tena iliyoanzishwa na Mkuu 1800, ilibidi nikae vizuri nitulie maana kumbe hii kitu ilikuwa imeshaongelewa kwa kireeefu, na michango miingi, na mimi mara zote nilikuwa nikiangalia thread hii ya mayai ya kwale nilikuwa naipita tu, nilikuwa naona ni mzaha tu, hakika ukitaka kujua utamu wa ngoma ingia ucheze.
Pamoja na kumshukuru mleta thread hizi Mkuu 1800 na wachangiaji wengine wote kwa namna ya pekee nimpongeze sana Mkuu Chasha! Kweli Mkuu unamsuli imara katika kufuatilia ishu, umemwaga post nyingi kuhusu Kwale na kutoa uzoefu wako kadri nafasi ilivyokuruhusu na bado umeendelea kwa kirefu kunielimisha hapa! Mungu akuzidishie mafanikio kwa moyo wako wa kupenda kushea na waTz. Ila kusema kweli ishu ya vibali imenitia hasira na kujichukia kuwa Mtanzania, hakika walio nje ya Tanzania wanapotutazama watanzania nadhani tunaonekana kama tuko primitivu sana!
Wasomi wote watakaosoma maandishi yangu hapa watambue kuwa wengi wa wasomi Tz ni wasomi tu lakini hawajaelimika maana watu hawatumii elimu zao kuboresha maisha ya watanzania, wasomi wengi wanafanya kazi bila reasoning ya kitaaluma na kutumia common sense! Kwa mfano kuweka vibali vya ufugaji na biashara ya Kwale kundi moja na uzito uleule kama vibali vya simba hii ni nini? Kutoa vibali siyo ishu kama vibali hivyo vingekuwa vinapatikana kwa uwazi na uhakika, lakini kuweka utaratibu wa vibali usiotekelezeka, ambavyo undani wake ni kama hawataki mambo hayo yafanyike ni maendeleo gani haya!
Hata hivyo Mkuu Chasha inaelekea kuna ubaguzi na pengine ni mwendelezo wa tatizo letu sugu la rushwa Tz maana ninajiuliza yule aliyeleta Kwale kwenye maonyesho ya nane nane ujumbe wake kwa taifa ni nini iwapo vibali vyake haviwezi kupatikana?
Watanzania tunaweza kujivuna na kujipiga kifua sana tuwapo ndani ya nchi yetu kwamba tuko juu kwa hili na lile lakini ukitoka nje ya nchi ukichanganyika na watu wa mataifa mbali mbali unagundua wenzetu wako mbali sana. Nahisi nchi zote east africa Tz ndiyo ni usiku zaidi. Ndiyo maana kwa kuona hivyo Kenya, Uganda na Rwanda wameona watu-avoid waendelee na shirikisho lao maana ukitazama kuanzia janga la bandari ya Dar ni kwamba Tz bado tuko gizani sana. Simulizi lako la mizengwe ya vibali uliyoandika hapa Chasha umenilegeza kabisa najiona kama mtanzania bado siko huru!! Kenya wako mbali sana na kamwe tusijilinganishe nao sisi tulipouvaa ujamaa kisha tukautupa na kuanza upya wao tayari walishafika mbali sana kwenye kila jambo ndiyo maana wanaonekana wako aggresive sana kwenye business.