Mkuu naomba nirudi na feedback, Nashukuru kwa kweli wale vifaranga ulioniuzia wamekua sana na sasa baadhi wameanza kutaga,katika vifaranga 74 niliopata 8 walikufa na 66 ndio ninao mpaka sasa,naanza kufurahi ulaji wa mayai ya kwale kwa afya na tiba pia,na soon nitaanza kula nyama ya quail baada ya kutotoresha na mimi vifaranga vipya!wadau wengi wanaokuja kwangu wamevutiwa na ndege hawa,na nimeshapata order ya vifaranga na mayai baada ya baadhi kuzisoma na kugundua sifa na umuhimu wa mayai ya kwale!Kikubwa hapa ni kuleta SHUKRANI NYINGI KWAKO,kwa ushirikiano ulionipatia mwanzo mpaka sasa!Mungu azidi kukubariki