May be huyu binti alikuwa ni mkarimu?

May be huyu binti alikuwa ni mkarimu?

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,419
Reaction score
18,370
Wakati natoka Zenji leo kwenye boti nilikaa na mdada mmoja,mara ya kwanza ni kama anajishuku kunisemesha mi namcheki tu,tulipokaa vizuri akatoa noti ya sh 2000/= imeungua moto upande,akaniambia,'kaka nimeshikishwa hii noti bila kujua,nawezaje kuitoa?

Nikamwambia nenda kanunue chochote humu ndani watapokea tu,basi akarudi na chipsi zile zilizokaushwa na pili pili kibao.

Akaniambia kaka karibu tule ila pili pili nyingi sijui kama utaweza,unajua sometimes mtu akikukaribisha basi hata kuonja usimvunje moja,nikaonja.

Dah ndo ikawa kuonja onja,mara "kaka sijui hi chipsi itaishaje furaha yangu tule iishe maana ina pilipili"

Tukaendelea mdogo mdogo,mara "unakunywa soda gani siyo vizuri maana naona yenyewe kama haiendi" dah sasa hiyo lafudhi,aliporudi nikamwuliza we kabila gani,akaniambia mi mnyamwezi kwetu Ulyankulu Tabora.

Mara kasinzia gafla kaniwekea mkono,nilisisimka mwili na ninavyopenda black beauties,'memory ikanijia nikachukua ticket ya Azam nikaigeuza nikasoma makosa kwa wasafiri nikasoma namba 10 "(kufanya mapenzi fidia ni sh 50,000)"

Nikasimama,mara akagutuka "kaka sijui ndugu zangu watanipokea kweli sina uhakika" nikamwambia usijali wanaweza kwepo tu.

Sasa wakati Wa kutoka tukajikuta tumebaki wa mwisho.


Wakuu inaonekana huyu ni wife material anajali wanaume,wenye uzoefu please!
 
Picha tafadhalii hainog bila hiyo picha ya beuty Nyakusa..
 
Ila mkuu siku nyingine uspende kupewa vitu vya kula kwenye safari ukala utakujaga kuibiwa Siku nyingine au ukafanyiwa kitu kibaya, usiamin sana watu kwa kumwangalia tu
Ni kweli lakini haijakutokea,kuna that feeling unahisi ukikataa umeoffend,kama we mwenyeji wa kanda ya kaskazini ukienda kwa watu ukikataa kula basi utapewa maji ya kunywa
 
Oa huyo mkuu ili avatar yako ipate uhalisia..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom