MaxMalipo, kampuni iliyoshindwa kuinovate.

Oct 27, 2020
97
400
MaxMalipo ilikuwa moja ya kampuni zinazofanya vizuri kwenye tech space in Tanzania. Ila kwa sasa ni kama inaelekea kufa hivi.

The payment industry ni moja ya industry inayokua kwa kasi, hasa hasa ikichangiwa na ukuwaji wa internet, more specifically ecommerce.
Hii ni kampuni ambayo ilikuwa na first mover advantage kwenye industry ya malipo Tanzania. Moja ya kampuni za kwanza zilizoleta huduma ya kurahisisha malipo.

Shida yao moja ni kuwa walishindwa kudiversify their product offering, wao waliconcentrate kwenye POS systems.
Ambapo kwasasa matumizi yake yamepungua kwasababu kila kitu unaweza kufanya kupitia simu, whether ni kulipa bill mbalimbali, au kufanya manunuzi ya bidhaa.

Kitu ambacho naona kingeweza kuwasaidia kuendelea kukua na kusurvive ni kutarget wafanyabiashara wa mtandaoni. In short sasa hivi online merchants ni wengi sana, wether ni mahoteli, kampuni za utalii, wauza bidhaa na watoa huduma mbalimbali wa mtandaoni, watengeneza software etc. Wote hawa wangeweza kuwa their target customers. Sasahivi mtu ukitaka uaccept malipo mtandaoni inabidi uimplement kila kitu kimoja kimoja yani mpesa kivyake, tigo pesa kivyake, airtel money kivyake, visa/ mastercard kivyake etc. Kampuni pekee ambazo zinaweza kumrahisishia mtu kuaccept vyote hivyo under one roof nikampuni za nje, mfano pesapal, directpay online, ipay africa, jengapgw, na baadhi ya hizo kampuni zinaoffice hapa bongo. So mtu anabaki kuwa na option mbili either utumie hizo kampuni au uimplement your own custom solution mwenyewe.

We need our own stripe/ paystack. Hizi ni moja ya fintech companies zinazofanya vizuri kwenye industry ya malipo na ni very user friendly. Moja ni ya wamarekani(stripe) na nyingine ni ya wanaigeria(paystack). Je maxmalipo na other tech companies hawajaona fursa iliyopo. Iweje kampuni za nje ndo zije kuprovide hizi services wakati kuna kampuni za bongo ambazo zingeweza kuingia kwenye hii space na kuongeza competition. Nimetumia MaxMalipo kama mfano kwasababu am sure they had the resources and expertise za kuweza kuimplement hii kitu. Ila inaapply pia kwa other software development companies za bongo.

Inshort the online payment industry ni a billion dollar industry with almost unlimited opportunities. Na inaendelea kukua kila siku.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom