Maximo ndani ya filamu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maximo ndani ya filamu!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by TANMO, Aug 9, 2009.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars' Mbrazil Marcio Maximo, ameonyesha kipaji chake zaidi ya soka kwa kuigiza katika filamu ya ‘September 11' itakayozinduliwa baadaye mwaka huu.

  Kwa mujibu wa Mratibu wa Kampuni ya Vanedrick Film Production, Majuto Omary, mbali ya Maximo, katika filamu hiyo wamo nyota wengine kama aliyekuwa mtangazaji wa runinga, Ben Kinyaiya.

  Wengine ni Flora Mvungi aliyekuwa Miss Kanda ya Mashariki mwaka jana, ambaye sasa ni kinara katika igizo la Bongo Dar es Salaam, Mzee Magari, Yusuph Mlela, Mtanga, Mzee Chilo, Jacqueline Wolper, Farida Sabu, Delly Samson na Mzee Ulotu.

  Majuto alisema kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha filamu na baada ya hapo itazinduliwa kwa wadau wa tasnia ya filamu nchini katika tarehe itakayopangwa kabla ya kuingia sokoni.

  Maudhui ya filamu hiyo yanahusu msichana aliyepata mikasa mbali mbali siku ya sherehe za kuzaliwa na kupelekwa hospitali, ambapo baadaye anakumbana na tatizo kubwa hadi rafiki yake wa kiume kumkimbia na baadaye anakumbana na mfululizo wa matukio ambayo mengine yanayofurahisha na kusikitisha.

  Source: Bongo5
  Kweli Bongo ukiwa na jina tu, utapata dili kibao hata kama siyo za fani yako.
   
Loading...