Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

bayanda abene nkoyi, abiswe dwandya imilimo kale no...nzugu gubiswe gubagalu na bagika ubone isingwanda siliponyiwa.....lekaga gete

Ngika nulu nghalu?
Nizoka kale sana ama kanza aba Maseyi umfumu oyo ali bariadi... Nkoyi e mbina a banho bagaponyaga malogho...m
 
............................creativity,well done Magulumagu🙂
 
Kuandamana siwezi,nguvu ya uma mi sina,
Kama vina huviwezi,heri kuwa maumuna,
Malengaze kuwa enzi,nipe jamvi wetu mwana,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Mzee Mwanakijiji,bonyeza hicho kitufe,
Poromosha kama uji,nipe tafu sije nife,
Masanilo mchungaji,Lukansola mwana ife,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,


Sugu wetu malaria,Aspirini dawa yake,
Babukijana silia,unga mkono babake,
Quinine sijetupilia,Field masha iwe mwake,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

mapenzi yalifuata,malenga walikuwepo,
mapicha mmeyafunta,Cereb kama upepo,
Inteligenti majita,siasa jukwaa lipo,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

byashara nayo spoti,malenga mmemnyonga,
elimu lugha si sapoti,eti ndani ya malenga,
utani sheria chati,dokita wote wachanga,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

La kitaifa jukwaa,hapo nakufagilia,
utaifa haujakwaa,malenga sikilizia,
malenga wote imezaa,kamwe sijakadiria,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

najua tupo wengi,vina kuvipangilia,
msukuma hata mangi,unguja vilianzia,
musoma na usangi,ujiji nakuhadhithia,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Kama vina vinagoma, Lizzy atakufundisha,
karamu haitagoma,hata uanzie insha,
usinitupe harama,mwenzio nimeshaisha,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

hapa ndipo mwisho wangu,nipe jukwaa nichane,
najifisha sina kwangu,leo huku kama chane,
nipe nichane mawingu,hata usiku manane,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Nimegundua kitu baada ya kusoma hapa na kufuatilia majibu ya watu:
Wakati mwanzisha mada ameonyesha ubobevu sana katika ujuzi wa vina na mizani, zaidi ya asilimia 80 ya majibu hayakuzingatia kanuni za mashairi ya kimapokeo. Imeonekana wazi kuwa wachangiaji walilenga aina hii ya mashairi lakini kwa bahati mbaya hawana ueledi wa kujua kugawa ile 8 kwa 8 katika ubeti. Matokeo yake ukiimba shairi haliimbiki. Hata wale walojaribu kulazimisha vina viendane wamejikuta wakiongeza silabi zaidi ya 16 au pungufu ya 16 katika ubeti mmoja. (NARUDIA KWA VILE WAMEJARIBU KUANDIKA MASHAIRI YA KIMAPOKEO. iNGEKUWA GUNI AU MAPINGITI NINGEBADILI MAONI). Lakini nawapa heko sana walojitosa umalengani.
Mimi sio mshairi au mtaalamu wa lugha au fasihi. Lkn ni mpenzi wa lugha tu.

Magulumangu sikia, umechokoza manyigu
Yakianza 'kurukia, kama madhara ya tegu
Dokita ukiendea, uende kwake Amigu
Umeweza kutukonga, nyoyoni mwetu malenga!
 
Judith umenishusha dear sijaona umenitupia angalau mistari minne hivi, hujasoma kilio changu kwa maxence? Unga mkono kwa mistari dada

kakangu sijakushusha, we ndo umepotezea,
sikutaka kukupasha, kichapo ungechezea,
kama cha kule Arusha, wameru walikolea
maxince kakuyeyusha, nguvu ya umma tumia
 
Nimegundua kitu baada ya kusoma hapa na kufuatilia majibu ya watu:
Wakati mwanzisha mada ameonyesha ubobevu sana katika ujuzi wa vina na mizani, zaidi ya asilimia 80 ya majibu hayakuzingatia kanuni za mashairi ya kimapokeo. Imeonekana wazi kuwa wachangiaji walilenga aina hii ya mashairi lakini kwa bahati mbaya hawana ueledi wa kujua kugawa ile 8 kwa 8 katika ubeti. Matokeo yake ukiimba shairi haliimbiki. Hata wale walojaribu kulazimisha vina viendane wamejikuta wakiongeza silabi zaidi ya 16 au pungufu ya 16 katika ubeti mmoja. (NARUDIA KWA VILE WAMEJARIBU KUANDIKA MASHAIRI YA KIMAPOKEO. iNGEKUWA GUNI AU MAPINGITI NINGEBADILI MAONI). Lakini nawapa heko sana walojitosa umalengani.
Mimi sio mshairi au mtaalamu wa lugha au fasihi. Lkn ni mpenzi wa lugha tu.

Magulumangu sikia, umechokoza manyigu
Yakianza 'kurukia, kama madhara ya tegu
Dokita ukiendea, uende kwake Amigu
Umeweza kutukonga, nyoyoni mwetu malenga!

hakika we mgeni, wa jamvi na jukwaa,
wenzio tuko makini, nane kwa nane sanaa,
kote hapa uwanjani, Judithi ndiye balaa
vina nayo mizani, twaimba kama twapaa
 
Back
Top Bottom