Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,047
452
Kuandamana siwezi,nguvu ya uma mi sina,
Kama vina huviwezi,heri kuwa maumuna,
Malengaze kuwa enzi,nipe jamvi wetu mwana,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Mzee Mwanakijiji,bonyeza hicho kitufe,
Poromosha kama uji,nipe tafu sije nife,
Masanilo mchungaji,Lukansola mwana ife,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,


Sugu wetu malaria,Aspirini dawa yake,
Babukijana silia,unga mkono babake,
Quinine sijetupilia,Field masha iwe mwake,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

mapenzi yalifuata,malenga walikuwepo,
mapicha mmeyafunta,Cereb kama upepo,
Inteligenti majita,siasa jukwaa lipo,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

byashara nayo spoti,malenga mmemnyonga,
elimu lugha si sapoti,eti ndani ya malenga,
utani sheria chati,dokita wote wachanga,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

La kitaifa jukwaa,hapo nakufagilia,
utaifa haujakwaa,malenga sikilizia,
malenga wote imezaa,kamwe sijakadiria,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

najua tupo wengi,vina kuvipangilia,
msukuma hata mangi,unguja vilianzia,
musoma na usangi,ujiji nakuhadhithia,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Kama vina vinagoma, Lizzy atakufundisha,
karamu haitagoma,hata uanzie insha,
usinitupe harama,mwenzio nimeshaisha,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

hapa ndipo mwisho wangu,nipe jukwaa nichane,
najifisha sina kwangu,leo huku kama chane,
nipe nichane mawingu,hata usiku manane,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,
 
nahisi kama vile Shaban Robert kapata mrithi,kanyanga twende mwanawane Magulumangu zidi kuleta ala mpaka kieleweke!
 
Uwanja wa kujidai sio ee haya ngoja tusubiri aje mwenyewe akujibu, ila nimeipenda sana hii, big up
 
Mashalaaah ....

Magulumangu ukiahirisha ukataka kuandamana call me... :cell:
 
Maxence tunasubiri ujibu!!




haki yetu bado ipo,maxence awajibike,
mwanakijiji sipokuwepo,hahitaji ang'atuke,
la malenga naliwepo,itabidi shawishike,
Nipe uwanja nijidai,kwa vina hata vilazi,
 
Hahaha unataka uwanja ipi sasa???


Kama vina vinagoma, Lizzy atakufundisha,
karamu haitagoma,hata uanzie insha,
usinitupe harama,mwenzio nimeshaisha,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Nilidhani utaunga,kwa mikono hata miguu,
libeneke la malenga,lizzy kulipa ni juu,
naombeni kuniunga,zaidi hadi majuu,
Piga uwa garagaza,wa malenga nauomba,
 
Duuh
Kumbe shairi
Haya bana . . . .

Cpu mwana komputa,sapoti yako muhimu,
hata simu tu kuita,maxence ni muhimu,
siasa kitaa pita,wala kwao si muhimu,
Uwanja wetu malenga,jamani tuangaliwe,
 
nahisi kama vile Shaban Robert kapata mrithi,kanyanga twende mwanawane Magulumangu zidi kuleta ala mpaka kieleweke!

Kamwe mzaha haupo,ngome yetu ni ushindi,
si ndege mnyama popo,kumwelewa si ahadi,
anyonyesha yeye popo,aruka pia ka radi,
Bishanga kanyaga twende,uwanja lazima pata,

wengine hawakuomba,bure walizawadiwa,
mola wetu ye muumba,amewapa bila hinwa,
iweje si kirikimba,hewala si majaliwa,
Bishanga kanyaga twende,uwabja lazima pata,
 
Uwanja wa kujidai sio ee haya ngoja tusubiri aje mwenyewe akujibu, ila nimeipenda sana hii, big up

yeye asiponijibu,wapo walonipa tafu,
gaga wewe umetibu,mimi sasa si kipofu,
njiani kwa melikebu,wote ni watakatifu,
Maxence sipojibu,tegemea andamano,
 
Mashalaaah ....

Magulumangu ukiahirisha ukataka kuandamana call me... :cell:

vumilivu hula mbivu,asha d nakuambia,
la mgambo si potovu,likilia ashiria,
nimelipaka mapovu,tifu nitamtilia,
lazima kieleweke,uwanja wetu uwepo,

nimeanzisha mwenyewe,kamwe sitositisha,
lazima kwake mwewe,la kuku dua amsha,
sitopatwa kiwewe,wapo wanaopindisha,
lazima kieleweke,uwanja wetu uwepo,
 
naamu mama shanteli,uwanja mie nataka,
kamwe hatutafeli,iwapo wote tu mataka,
tuombe wote tusali,malenga wetu hilka,
Maisha ni safari ishi,upendavyo na upendwe,
 
Magulumangu mtu wangu, malenga twajua kulenga,jukwaa twalitaka kujikwaa si mawaa. Harakati umeanzisha tutakupa mikakati. Hata sie wachanga tujitoe michanga. Najaribu tu mkuu.
 
naamu mama shanteli,uwanja mie nataka,
kamwe hatutafeli,iwapo wote tu mataka,
tuombe wote tusali,malenga wetu hilka,
Maisha ni safari ishi,upendavyo na upendwe,
Kupendwa ni muhimu,hasa kwenye muhibu
hata nikiwa bubu,kamwe sitathubutu
magulumangu nibusu,nimekutegea shavu
hata kama ni safari,tutaishi tupendavyo?
 
vumilivu hula mbivu,asha d nakuambia,
la mgambo si potovu,likilia ashiria,
nimelipaka mapovu,tifu nitamtilia,
lazima kieleweke,uwanja wetu uwepo,

,



M bado nimekazana tuition kwa Lizzy, nakupa mstari mmoja nitamalizia kama home work...lol

Mvumilivu hula mbivu, ulimwengu wasasa hula mbovu... (To be cont...)



 
Back
Top Bottom