Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

i see hongera malenga wetu

Mnyonge mnyongeni,ila haki yake mpe,
nasi haki twaombeni,kwa giza hata kweupe,
fesiti ledi jamani,sapoti yako unipe,
Asante mama asante,pamoja mpaka tufike,
 
du jamaa anavo flow.... Amekuja kivingine

mimi nataka jukwaa,la malenga ndumbayeye,
hata wewe umejaa,vina vilazi hayeye,
mwambie wako jamaa,kilio chetu makeye,
Jukwaa lazima liwe,la malenga si utani,
 
M bado nimekazana tuition kwa Lizzy, nakupa mstari mmoja nitamalizia kama home work...lol

Mvumilivu hula mbivu, ulimwengu wasasa hula mbovu... (To be cont...)

Naendelea
kama hutaki mbivu kula mbovu,ulimwengu ujao utakula mbivu
 
Kupendwa ni muhimu,hasa kwenye muhibu
hata nikiwa bubu,kamwe sitathubutu
magulumangu nibusu,nimekutegea shavu
hata kama ni safari,tutaishi tupendavyo?

ya mtende ni bahati,busu nishalitokea,
kamwe si msamiati, kuthubutu sitapotea,
nitende mi we wa ati,shanteli mwana hotea,
Tutaishi tupendavyo,mpaka mwisho wa safari,
 
Magulumangu mwenzio leo mistari haipandi kabisa....kila nikijaribu nagonga mwamba!!!Ila naona mwanafunzi wangu ananiwakilisha....
 
Magulumangu mwenzio leo mistari haipandi kabisa....kila nikijaribu nagonga mwamba!!!Ila naona mwanafunzi wangu ananiwakilisha....

Nimefurahi mwalimu huja mind sijamalizia.... Wkend leo,,, nimekaa pozi ya kujipa raha mwenyewe na haitaki kabisaa nitumie brain yangu zaidi ya level niliyopo....
 
Magulumangu mwenzio leo mistari haipandi kabisa....kila nikijaribu nagonga mwamba!!!Ila naona mwanafunzi wangu ananiwakilisha....

shule umeshaitoa,acha nayo ijitoe,
hata mwamba lishatoa,sasa gamba lijitoe,
kama bata shatotoa,mhanga mwana ajitoe,
Ila letu tuliombe,jukwaa la wamalenga,
 
Asante Shantel.... Kazi kubwa hii sijui huyu jamaa hukaa mda gani.....

hukaa ninapokaa,mistari isojaa,
sitamindi ukipaa,la malenga letu jukwaa,
njo hata kwetu kitaa,wote malenga hujaa,
Kazi ni kazi jamani,vina vishazi ni tunzi,
 
hukaa ninapokaa,mistari isojaa,
sitamindi ukipaa,la malenga letu jukwaa,
njo hata kwetu kitaa,wote malenga hujaa,
Kazi ni kazi jamani,vina vishazi ni tunzi,

Need I say mo.... Bravo M... Very impressive....
 
ya mtende ni bahati,busu nishalitokea,
kamwe si msamiati, kuthubutu sitapotea,
nitende mi we wa ati,shanteli mwana hotea,
Tutaishi tupendavyo,mpaka mwisho wa safari,
Busu umelitokea, nami nimelipokea
wengi walimezea, na mate kulitolea
tuendelee kulilia, jukwaa la kulengea
mwisho wa safari, tutafika tupendavyo?
 
Need I say mo.... Bravo M... Very impressive....

Nimelitaka jukwaa,kwa maana nia ninayo,
kamwe sitokuwa kinyaa,kama wimbo wa oyoyo,
asha d sema dinaa,haki yangu ndani moyo,
Mpeni changu kilio,maxence akisikie,
 
Busu umelitokea, nami nimelipokea
wengi walimezea, na mate kulitolea
tuendelee kulilia, jukwaa la kulengea
mwisho wa safari, tutafika tupendavyo?

avumaye baharini,papa kumbe wengi wapo,
acha denda watokeni,wameze kama wa mwipo,
tutafika umalengani,kwa vina vyetu simpo,
Tutafika tupendavyo,mwisho safari karibu,

umelipokea kwa mbembwe,bila mukini hiyana,
uko juu kama limbwe,uzuri wako bayana,
nipe nikupe na wewe,ujuzi wangu tisana,

mwanzo wa safari ni moja, haki nakuambia
upige kelele kama chura, na ubweke kama mbwa
malenga tadumisha, na jukwaa kuanzishwa
ujuzi wako tisana,nani anabisha?

Bado nahema kwa nguvu, busu nalisikizia
papa wengi nao nyumbu, katu wanachungulia
siwezi kukupa ujuzu, busara u heshimika
mwisho wa safari karibu, safari moja huanzisha ingine
 
shanteli we uko juu,hata mimi nimekwisha,
walahi sina makuu,kwa hili utadumisha,
watasema kwa juzuu,ntabweka bila bisha,
njoo mama wewe njoo,nimeandaa sherehe,

tutamwita masanilo,kanisani unajua,
judithi dada kanilo,maombi kuyatatua,
siku uwe wangu hilo,wenye macho kuumbua,
Njoo mama wewe njoo, nimeandaa sherehe,
 
vigezo na masharti zingatia, kabla ujatia nanga
nakuhaidi shazashaza, penzi bila kujutia
wapo wanaolegeza, shauri yao watajuta
tusimsahau asha, lizzy na mwenzake preta

Nitakwimbia mwimbo, wa mashairi yenye vina
usisahau urimbo, magitaa na vinanda
kwanza litutoke jasho, lianzishwe jukwaa
umeandaa sherehe, mahari umetoa?
 
Mkuu kumbe umo
Unaweza kumfunika Mpoto
Kaza buti bila kikomo
Safari bado nzito
 
Kwa heri magulumangu, muda wa kinywaji umewadia
ninatoka nyumbani kwangu, kwenda kusalandia
sisahau kipochi changu, starehe kwenda lipia
maisha ni safari, ishi upendavyo nakwambia
 
Yeah,ni shairi,..
ndo kazi zetu TRC siku hizi,si unajua tena treni zote zime kufa
mkuu,kipaji kinaokoa
Tanzania Railway Stesheni, ilimtoa baba ako kijijini
ikamleta mjini, kwa senti ishirini
kuikashifu ya nini, kwani imetutoa mbali
tusidharau mbachao, kwa msala upitao
 
Back
Top Bottom