Mkuu Max, pole na matatizo.
Ondoa shaka bado tutaendelea kupigania haki ya kupata na kupashana habari na hii ni haki ya kikatiba bila kuvunja sheria.
Nilikwishasema kwamba vita hii ambayo polisi wameianzisha dhidi ya JF haitafanikiwa.
Ikiwa tayari tunao watu kama Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ambae nae anatumia haki hiyohiyo ya kupata taarifa kupitia JF na kuzijibu kama njia ya kupashana habari, basi JF imekubalika.
Tusubiri tarehe 29 pale hakimu atakaposikiliza madai ya mwendesha mashtaka na kuona hapa hakuna uzito wa kesi hii.